Kasomi
JT Founder
Elon Musk
Kampuni ya akili bandia ya Elon Musk, xAI, imechukua umiliki wa X, mtandao wa kijamii uliokuwa ukijulikana kama Twitter, katika dili lenye thamani ya dola bilioni 45. Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye X, Musk alisema: “Mustakabali wa xAI na X unahusiana kwa karibu. Leo, tunachukua hatua rasmi ya kuunganisha data, mifano, kompyuta, usambazaji, na vipaji.”
Musk aliongeza kuwa muungano huu utafungua fursa kubwa kwa kuchanganya uwezo wa hali ya juu wa akili bandia wa xAI na upeo mpana wa X. Hatua hii inaashiria zama mpya za mtandao huo, huku ikitarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika teknolojia na mawasiliano.
Powered By: @lapexproperties & @maembe_motors