Advertise here

Hapakuwa na sababu ya kutoijua historia ya kweli ya tanu na uhuru wa tanganyika

HAPAKUWA NA SABABU YA KUTOIJUA HISTORIA YA KWELI YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA

Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwa na historia ya kweli ya harakati za kuamka kwa Watanganyika katika kujileta pamoja kwa maslahi ya nchi yao lakini naweza kusema akaipoteza kwa makusudi.

Nishakieleza kisa hiki mara kadhaa.

Mara baada ya uhuru kupatikana katika mazungumzo ya kawaida tu kati ya Abdul Sykes, Nyerere, Mwalimu Kihere na Dossa Aziz, Mwalimu Kihere alitoa wazo la kuandika historia ya TANU.

Wazo hili Nyerere alilipenda na akatoa ushauri kuwa kazi hiyo aifanye Abdu Sykes na Dr. Wibard Klerruu awe msaidizi wake.
Nyerere alisema kuwa katika waasisi wale 17 wa TANU hakuna anaeijua historia ya TANU kumshinda Abdul na sababu ni kuwa baba yake ni mmoja wa waasisi wa African Association 1929 na ana nyaraka na taarifa nyingi za chama.

Haya kanieleza Dossa Aziz mbele ya Ally Sykes nyumbani kwake Mlandizi.

Kleist mtoto wa Abdul Sykes ananihadithia anasema yeye kamuona baba yake pale TANU Office akifanya kazi hii akiwa na Dr. Klerruu.
Walikuwa kila wakikamilisha sura wanampa Mwalimu kuiangalia.

Hiki kikawa chanzo cha matatizo katika uandishi huu.

Abdul yeye alianza historia ya TANU na historia ya baba yake Kleist Sykes (1894 - 1949).

Hii ilikua historia ya miaka 25 ya uhai wa African Association/Tanganyika African Association ambayo Kleist Sykes alikuwa kiongozi kisha mwanae akawa kiongozi pia kuanzia mwaka wa 1950.

Lakini si hili tu katikati ya uongozi huu kulikuwa na uongozi wa Thomas Abdulkarim Plantan wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945).
Hawa akina Sykes na Plantan ni ndugu na walikuwa na sauti kubwa Dar-es-Salaam na walimiliki gazeti na hili gazeti likawa ndiyo sauti ya Waafrika wa Tanganyika.

Historia hii ina mengi sana.

Katika haya mengi ni kuwa Schneider Abdillah Plantan yeye ndiye aliyesimama kidete kuwa uongozi wa TAA uliokuwa madarakani uondolewe na vijana wachukue uongozi ili TAA ianze juhudi za kuikomboa Tanganyika kutoka utawala wa Waingereza.

Baada ya uchaguzi wa 1950 uliowatoa madarakani ''Wazee wa Kijerumani,'' ndipo ukaingia uongozi wa Dr. Vedasto Kyaruzi President na Abdul Sykes Secretary.

(Hawa akina Plantan pamoja na ndugu yao Kleist walikuwa watu wa aina yao si mchezo.

Wakisema Kijerumani ''fluently'' na wote walivaa uniform ya jeshi la Kijerumani katika WWI na wakapigana dhidi ya Waingereza.
Hata baada ya vita wao siku zote wakijiona kuwa ni wanajeshi katika jeshi la Kijerumani.

Walikuwa wakiwa pamoja wanazungumza Kijerumani na wakawachukia Waingereza).

Hiki ndicho kipindi TAA ilichukua mwelekeo mpya kabisa TAA ikiwa na wasomi wa Makerere kama Hamza Mwapachu, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Joesph Mutahangarwa kwa kuwataja wachache.

Viongozi hawa walifanya makubwa.

Mwaka wa 1952 ndipo Julius Nyerere alipofika nyumbani kwa Abdul Sykes.
Kalamu ya Abdul Sykes ilikuwa ikieleza historia hii.

Inaelekea Nyerere hakupenda hii ndiyo iwe historia ya TANU.
Abdul akajitoa katika mradi huu.

Mradi huu haukutoa kitabu wala haifahamiki mswada huu uko wapi.
Nadhani sasa inaeleweka imekuwaje leo tunahangaika na historia ya TANU na historia ya Nyerere.

Ilipokuja kuandikwa historia ya TANU mwaka wa 1981 hawa wote niliowataja hapa na wengine sikuwataja lakini ndiyo walikuwa mstari wa mbele hawakutajwa katika kitabu kile.

Lakini jambo la kushangaza Nyerere inalekea hakuona tatizo katika historia hii kuwa haiko sawa.

Mzee Saidi ww unaijua vizuri sana historia ya Tanzania mm nakuombea kwa Allah uendelee kuwepo tuweze kufaidi hazina uliyokuwa nayo.
 
Similar threads

Back
Top