Kasomi
JT Founder
UPDATES " Nimezaliwa katika familia ya CCM akiwemo baba yangu ambaye ni mwanzilishi wa Chama Cha TANU,lakini licha ya kuzaliwa katika chama hicho chama Cha mapinduzi kimepoteza mwelekeo na kukiuka misingi iliyowekwa na waasisi wake.
CCM imesaliti adhima na misingi iliyowekwa na waasisi wa Chama hicho, CCM imekuwa na misingi ya kujisahihisha. CCM ilijisahihisha mwaka 2015 baada ya Mwalimu Nyerere. Hii ya sasa imechoka, haina wazee wa kuisahihisha. Hii ya sasa ni kama vyuma chakavu.
Upendeleo umehalalishwa, vitabu viko sawasawa ila genge linaloiendesha sasa hamna kitu. Pia vitendo vya wizi wafedha za wavuja jasho. Watu wamekula hela kutokana na urefu wa kamba zao. Watu wamekuwa wakihangaika kulipia hospitali kutokana na CCM kushindwa kuwajibika na kuruhusu watu wacheche kula kutokana na urefu wa kamba yake.
Pia upotevu wa mali za umma na hakuna aliyewajibishwa. Mchakato wa uchujaji wa mwaka huu 2025 umevunja katiba ukiwa na upendeleo. Tumeshuhudia kikao Cha kuwaengua watia nia wakikikesha usiku kucha kuwaondoa wakina Mpina,lakini kukaa hata kikao kimoja kujadili ripoti ya CAG juu ya upotevu na wizi wa fedha hakuwahi kujadiliwa hata siku moja?" Luhaga Mpina Mgombea urais kupitia chama Cha ACT-Wazalendo akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini leo tarehe 14 Agost, 2025 katika Jengo la Maalim Seif, Dar Es Salaam.