Mchungaji ajinyonga kisa Msongo wa Mawazo

Mtata

Member
1752685903383.jpg

HABARI Mchungaji Zakaria Mbyopyo wa kanisa la Bethel power of God ministry International lililopo kata ya makambini Halmshauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe amekutwa amejinyonga ndani ya ofisi yake huku sababu ikitajwa kuwa ni msongo wa mawazo.

Wakizungumza na EATV Mashuhuda wa tukio hili wanaeleza sababu za mchungaji huyo aliyewahi kuwa kiongozi wa serikali ya mtaa wa Makambini kuchua maamuzi haya magumu.

Viongozi wa kanisa wamesikitishwa na kitendo alichofanya mchungaji huyu huku wakitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia maamuzi yasiyofaa kwakuwa wao ni viongozi wa jamii.

Chanzo: East Africa TV
 
Back
Top