Advertise here

Kama una Dakika 7 hebu niazime nikufundishe namna ya kuishi na MWANAUME ambaye anapenda kulalamika lalamika!

Simulizi

Member
Kama una Dakika 7 hembu niazime nikufundishe namna ya kuishi na MWANAUME ambaye anapenda kulalamika lalamika!

Kuishi na mwanaume ambaye anapenda kulalamika kila kitu kidogo kunaweza kuwa changamoto kubwa na kama ni ndoa basi ukaiona chungu hatakama hakupigi wala kukutukana.

Mara nyingi wanawake ndiyo hupenda kulalamika na ishazoeleka hivyo sasa ikitokea kwa mwanaume kunakua na ukakasi kidogo! Hapa kuna baadhi ya vidokezo ambavyo unaweza kuvifuata ili kuhakikisha unaweza kuishi na mwanaume huyo kwa amani na furaha:

1) Elewa sababu ya kulalamika kwake: Kuelewa sababu ya kulalamika kwake kunaweza kukusaidia kuelewa jinsi ya kuwasiliana naye vizuri. Jaribu kuzungumza naye na kumuelewa vizuri kabla ya kumhukumu. Kuna sababu nyingi za mwanaume kufanya hivyo, inaweza kuwa ni kweli anachokulalamikia, labda unakera kweli ila kwake hawezi kuongea bila kulalamika.

Inaweza kuwa ni malezi, namna alivyolelewa kwoa ilikua ni kulalamika, labda alinyanyasika sana huko nyuma, aliumizwa sana na mambo kama hayo. Muhimu jua halalamiki tu, kuna sababu, hembu kabla ya kujitesa au kumhukumu angalia, chunguza sababu hizo vizuri.

2) Wasiliana vizuri: Ili kuepuka migogoro, ni muhimu kuwasiliana kwa njia nzuri. Jaribu kutumia maneno mazuri na ya kujenga wakati wa kuzungumza naye. Epuka kutumia maneno ambayo yanaweza kumfanya ajisikie vibaya. Kwa mfano,a cha kumtukana, kumjibu kwa hasira hata kama unjakereka, kumuambia una kisirani, kumsonya na kumdharau, kumnunia, kumuambia acha mambo ya kike, nimekuchoka.

Kumjibu vibaya kunazidisha tatizo kwani kunakua hakuna kusikilizana. Kua mpole sio uwe mjinga hapana kuwa mpope, usimnunie au kumnyamazia bali jibu vizuri bila kupaniki. Ukijiona unapaniki kabla ya kujibu, pumua kwa nguvu mara 5 au hesabu mpaka 10 kichwani kwako ndiyo ujibu!

3) Tambua mipaka yako: Ni muhimu kutambua mipaka yako. Usikubali mtu akupuuze au kukutendea kwa dharau. Hakikisha unaweka mipaka yako na kuheshimu mipaka ya mwanaume huyo.

Hapa namaanisha hivii, ni mume wako lakini ni lazima uwe na kiwango cha uvumilivu, labda angee lakini aiskutukane mbele za watu, sikutukanie Mama yako,a sikupige na mambo hayo. Weka kiwango cha vitu unavyoweza kuvumilia na kuambie kabisa, akizidisha kasirika, nuna au onyesha tu kuwa hujafurahia bila kujali anachukuliaje.

4) Onesha upendo na huruma: Mwanaume huyo anaweza kuwa anahitaji upendo na huruma. Jaribu kumwonyesha upendo wako na kumtia moyo. Kuwa na uvumilivu na subira naye. Kuna wengine hata sio wababe, analalamika kwakau anahitaji kupendwa, anahitaji kuonewa wivu, kujaliwa, kuulizwa umekulaa nini, kuambiwa nimekumiss, kuulizwa ulikua na nani, ushamsoma kama anahitaji upendo mpe bi8la kujali kama ataupokea au atakujibu vizuri!

5) Zingatia mambo mazuri: Kuna mambo mazuri ambayo unaweza kuzingatia. Fikiria kuhusu mambo mazuri ambayo mwanaume huyo amewahi kukufanyia. Hii itakusaidia kuepuka kuzingatia tu tabia yake ya kulalamika. Kwmaba pamoja na kisirani chake, kulalamika kwake lakini labda anahudumia familia, ukiumwa anajali, ndugu zako anawasiadia, anapenda watoto. Hapa utajua kuwa huyu ana madhaifu haya kama binadamu ila ana hiki na kile, itakusiadia kumpenda na kuchukulia kulalamika kwake kama kitu cha kawaida.

6) Chukua hatua za kujitunza mwenyewe: Kama kulalamika kwa mwanaume huyo kunakusumbua sana, jaribu kuchukua hatua za kujitunza mwenyewe. Hii inaweza kujumuisha kuwa na muda wako binafsi au kuzungumza na rafiki yako.

7) Kumbuka kuwa huwezi kubadilisha tabia ya mtu mwingine: Ni muhimu kukumbuka kuwa huwezi kubadilisha tabia ya mtu mwingine. Jaribu kuzingatia mambo ambayo unaweza kubadilisha, kama vile jinsi unavyowasiliana naye, lakini usijaribu kubadilisha tabia yake.

Mjue yuko hivyo ishi naye kihivyo hivyo,. Isijitese kumbadilisha
 

Similar threads

Back
Top