Claudia Lubao Maarufu kama Chemical Atunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD)

Kasomi

JT Founder
Claudia Lubao Maarufu kama Chemical ambaye ni Msanii pamoja na Staa wa Rap kutoka nchini Tanzania, Jana April 30,2025 ameweka wazi kuhusiana na Historia ya Maisha yake Kwa kufanikiwa kupata (PhD) ya uzamivu baada ya kufaulu mtihani wake wa mwisho kwenye masuala ya sanaa
1746079382549.jpg

Hivyo kwasasa Claudia lubao, Rasmi ataitwa Dr. Lubao.. Chemical amehitimu shahada hiyo katika Chuo Kikuu cha St Andrews, nchini Uingereza ambako alikwenda kusoma baada ya kupata ufadhili wa kimasomo kufuatia kufanya vizuri na kuwa Mshindi wa kwanza wa tafiti bora Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) 2020/2021 alikosoma shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya sanaa za maonesho, baadaye shahada ya uzamili (Masters) ya sanaa katika usimamizi wa urithi wa kitamaduni.

Chemical amethibitisha hivyo Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuonesha furaha yake Kwa kutimiza ndoto yake pamoja na kuwashukuru wale wote waliompambania wakiwemo marafiki, ndugu na wasimamizi

"I once had a dream… and today, I woke up as Dr. Lubao!I’m beyond excited to share that I’ve officially passed my PhD Viva! I’m truly honoured and deeply grateful for the incredible support I’ve received from my supervisors, affiliated departments, reviewi " ameandika Chemical
 

Similar threads

Back
Top