Advertise here

Maoni ya wadau na uchambuzi juu ya kisiwa cha maajabu cha buchosa

Kasomi

JT Founder
Haya ni baadhi ya Maoni ya wadau kuhusu kisiwa hicho;

"Hakuna cha ajabu hapa wala hiki si kisiwa halisi ni imani tu za watu. Hii ni sehemu ya ardhi inayojitengeneza kwenye ghuba ya ziwa kwa kukusanya uchafu kwa muda mrefu ikijumuisha udongo, tope, nyavu za wavuvi n.k kisha mimea kama nyasi na miti huota juu yake. Mimea hiyo baada ya miaka mingi hushikamana na kulifanya lionekane kama ni nchi kavu.

Lakini kiasila na kijiografia eneo hilo huwa halikushikamana na ardhi kwa chini yake huwa linaelea juu ya maji kama meli. Kwa kiwango kikubwa mimea yake huwa ni aina ya mabingu bingu, malutende, majani na vichaka vidogo vidogo, magugu maji na hata wanyama wadogo wadogo kama kenge, fisi maji n.k hupatikana humo.

Kwa hiyo ukitokea upepo mkali kama kimbunga au ule unaoitwa na wakazi wa maeneo ya ziwa Victoria MSOKE hulisukuma kwa nguvu eneo hilo kwenda majini ambako likiwa ni kubwa huonekana kama kisiwa. Mara upepo na mawimbi ya ziwa yanapotulia, eneo hilo hubaki likielea ingawa huwa linasogea taratibu kwenda huku na kule. Hatimaye kisiwa hicho bandia hupotea kwa kutawanyishwa na maji baada ya udongo wake wote kufyonzwa na maji ya ziwa na mimea yake kubaki haina pa kujishikisha.

Miaka na miaka tangu visiwa bandia vya aina hii vinatokea hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuonesha kisiwa hai hata kimoja kilichoibuka kwa njia hiyo hakuna.Hata hiki cha leo hakitakuwa mahali hapo baada ya siku kadhaa ama kitasukumwa sehemu nyingine au kitasambaratika".
~kutoka kwa wadau

Video ya kisiwa hicho

Zaidi soma
Kisiwa cha maajabu Kahunda Buchosa wilayani Sengerema
 

Similar threads

Back
Top