Advertise here

Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Yatoa Taarifa kuhusu habari zinazo sambaa

Mtata

Member
JWTZ WAJIBU KAULI YA CAPTEN TESHA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuchapisha maudhui yanayochochea kuliingiza jeshi hilo katika mambo ya kisiasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Bernard Masala Mlunga baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, wengine wakijinasibisha na JWTZ bila uhalali, na baadhi yao ni wale walioachishwa jeshi kutokana na tabia na mwenendo usiofaa au kujihusisha na siasa na uanaharakati.

JWTZ limeeleza kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uaminifu, utii na uhodari, likizingatia kiapo chake.
1759604668105.jpg
 
Back
Top