john achila mukumwa
Member
Maombi Yetu kwa Mungu Hupitia Madarasa Yake
Madarasa ya Mungu ni nini
Haya ni mafunzo ya kiroho katika ulimwengu wa roho, yanayofanywa na Mungu mwenyewe.
Hebu tuangalie Ezekiel 36:26-27: 26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Pia, tuangalie Mithali 1:32: “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”. Kwa hiyo, moyo wa mtu hugeuzwa kwa madarasa ya Mungu.
Maombi yetu kwa Mungu
Yapo mambo ambayo watu wa Mungu wanatamani kuyapata au kuyafanya kwa muda waliopanga wao, lakini pasipo kujua pia kuwa upo muda wa Mungu kuruhusu mtu wake apate anachokitaka, au afanye analolitamani. Ni muhimu sana kujua hilo.
Yapo pia mambo ambayo tukimwomba Mungu, ni rahisi kupokea majibu papo kwa papo, lakini yapo ambayo yatachukua muda kujibiwa. Si kwa sababu Mungu hawezi kujibu hapo hapo. Hapana. Anaweza, kwa sababu hakuna kinachomshinda. Lakini anapoyachelewesha, wakati mwingine ni kwa faida yetu.
Katika hali ya kawaida, pale tunapokuwa tumeokoka, na Kristo amekaa ndani yetu, basi tunapompelekea Mungu maombi yetu, au haja zetu au mahitaji yetu, basi anakuwa anayasikia na siku ile ile anayajabu kama tumeomba sawa sawa na mapenzi yake. Lakini, matokeo ya majibu hayo yanaweza kuwa ni tofauti na mategemeo yetu. Wengi tunatamani Bwana Mungu atupatie jambo fulani na tunataka saa hiyo hiyo tukipate kile tulichoomba, pasipo kujua kuwa Mungu hataki tuangamie katika yale tunayomwomba, kama Mithali 1:32 inavyosema: “….Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.
Kwa hiyo, Mungu kabla hajakupa kile ulichomwomba, ni lazima kwanza aondoe upumbavu ndani yako. Na upumbavu mwingi tunakuwa tunazaliwa nao, kutokana na udhaifu wa mwili, na mwingine tunaupata kutokana na maisha ya dhambi tuliyokuwa tunayaishi, au tunayoishi. Hivyo, Mungu hawezi kutupa kitu kizuri halafu hatimaye kije kituharibu, vinginevyo atakuwa siyo Baba mzuri na mwenye hekima.
Mtu kubadilishwa Roho ya jiwe kwenda Roho ya nyama si kitu cha siku moja. Si kitu chepesi wala hili neno lisichukuliwe kirahisi. Hizo ni hekima ambazo Mungu anazitumia, pindi anapotaka kututoa katika hatua moja ya kimaisha kwenda nyingine.
Kiasili, nafsi zetu sisi wanadamu zinapenda kupokea majibu ya maombi mara tu tunapoomba. Lakini hekima ya Mungu wakati mwingine si kutupa kile tunachokiomba wakati ule ule tunapoomba. Wakati mwingine inaweza kuchukua muda mrefu kupokea majibu, na bado ikawa ni mapenzi ya Mungu.
Kwa hiyo, kipindi cha kuondolewa kwanza upumbavu hadi kupokea majibu ya maombi, ndicho kinaweza kuchukua muda mrefu kuondolewa upumbavu. Pia, kutoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wako, na kuweka moyo wa nyama, inahitaji muda wa kutosha, na hutofautiana baina ya mtu na mtu.
Mifano kuhusu maombi kujibiwa baada ya muda mrefu
1. Ombi la mtoto kupewa gari na mzazi wake
Tuchukulie kuwa wewe ni mzazi mwenye uwezo, na mtoto wako anayesoma chekechea anaomba umpe gari. Kwa mzazi mwenye upendo na hekima, huwezi kuchukua gari na kumpa pale pale, bali utampa ahadi ya gari. Hii ni kwa sababu bado hajajua hata kusoma na kuandika, wala hajajua kuhesabu, atawezaje kuendesha gari barabarani? Hivyo utakachofanya ni wewe kumpeleka kwanza shule ili upumbavu uondoke kichwani mwake, ili ajifunze gari ni nini. Na vile vile ajue kanuni za kuendesha gari, hadi sheria za barabarani ili asisababishe ajali. Hali kadhalika akajifunze matumizi ya gari kuwa si kwa ajili ya anasa, bali ni kwa ajili ya usafiri na kwa ajili ya kazi.
Wakati ambao umemwahidi gari hadi siku ya kumpa hilo gari, inaweza kuchukua hata miaka 15. Maana yake ni kuwa kama aliliomba akiwa na miaka 5, atakuja kulipata hilo gari akiwa na miaka 20. Sasa jiulize. Kama sisi wazazi tuna hekima kama hiyo, Mungu ni zaidi mara ngapi?
2. Darasa la kuondoa jiwe la kiburi na dharau
Mungu hapa mara nyingi humshusha mtu au humfungia vibali vyake vyote. Yaani, kama alikuwa juu, humshusha chini kabisa. Na Mungu huwainua wale waliokuwa chini na kuwafanya kumsaidia huyo aliyekuwa juu. Maumivu ya hilo tukio yatakufanya uwe mtii, mnyenyekevu na mwenye heshima, na kumheshimu kila mtu. Kiburi chote na dharau yote hapa husuguliwa. Na maumivu ya kushuka chini kuwa mavumbini kabisa. Unakuta unaenda zero kabisa, halafu Mungu anakuacha hata miaka kadhaa, halafu anapandisha maadui zako wote, na waliokuwa chini yako wote. Ukishaiva, unaweza kupatiwa ulichoomba.
3. Darasa la unyenyekevu
Mungu akigundua huna moyo wa unyenyekevu, huweza kukuletea ile hali ya kutamani kuwa na kitu fulani. Halafu huo uwezo Mungu hukuondolea. Kwa mfano, kuna ile ya kutamani kuwa na mume bora, kuwa na maisha mazuri, kuwa na vitu vizuri. Kiasi kwamba ukiviona moyo hukulipuka, na huo uwezo huna, unabaki kimya tu. Mungu anaweza kuruhusu hali iendelee ndani yako kwa muda mrefu. Inapoendelea kwa muda mrefu, yale maumivu ya kutokuwa nacho unaanza kuyazoea taratibu. Unaanza kujipa moyo unasema: “hata nisipo kipata, nina Mungu wangu”. Kwa hiyo hali itakulazimisha ujifunze kushukuru kwa hicho ulicho nacho. Hiyo hali itasababisha ukubaliane na unachokipata. Itafikia wakati utatambua kuwa Mungu Ndiye hugawa kila kitu kwa kila mtu. Ile hali kukubali sina na niendeleee kusubiri, unyenyekevu huzaliwa ndani yako. Hapo sasa Roho wa unyenyekevu huja kukaa ndani yako. Na hapo ndipo utapimwa kama upo tayari kupewa ulichoomba.
Kwa hiyo, moyo wa mtu hugeuzwa kwa madarasa ya Mungu. Mungu hawezi kukupa roho yake ndani yako ikiwa wewe hauko tayari. Ndiyo maana Mungu akiona mtu hamsikii, huwa anaachia mapigo kwanza yampige, yamtandike mtu vizuri, Akija kutulia, sasa Mungu ndipo huanza kutenda.
Huwezi kumwomba Mungu akupe jambo fulani kubwa halafu akakupa papo hapo, kwa hali na akili uliyonayo hapo. Ni lazima akutengeneze kwanza. Akufinyange. Yaani, akupitishe kwenye madarasa yake. Na kutengenezwa kunaweza kukugharimu hata miaka kadhaa, hadi utakapokidhi vigezo anavyovitaka yeye, ndipo akupe kile ulichokiomba. Ukiona bado hujakipokea kile ulichokiomba, ujue bado hujamaliza madarasa. Endelea kumngoja Bwana.
Huwezi kumwomba Mungu akupe mali nyingi na halafu akili yako inawaza anasa. Hawezi kukupa kwa wakati unaoutaka wewe, itakugharimu kwanza upumbavu uondolewe ndani yako, ndipo akupe.
Huwezi kumwomba Mungu akupe nyumba na huku kichwani unawaza kuwakomoa watu au kuwaonyesha watu fulani au kujivuna au kudharau, hawezi kukupa kwa muda huo, kwani utakuwa bado unao upumbavu ndani yako, ambao utakuharibu wewe endapo atakupa hiko kitu kwa muda huo. Atakachofanya kwa ajili yako ni kuondoa kwanza upumbavu ndani yako kupitia madarasa yake (na wakati mwingine hata kukupitisha kwenye umaskini), ili ujue kuwahurumia wengine, na siku utakapopata chako uweze kuwasaidia wengine. Kama ni mwepesi wa kumwelewa Mungu na upumbavu ukawahi kutoka ndani yako, basi ahadi utaipokea mapema, lakini kama ni mgumu, basi ndivyo ahadi yako itakavyozidi kuchelewa.
Huwezi kukwepa hayo madarasa ya Mungu hata ufanye nini, kwa sababu ni tathmini na maamuzi ya Mungu mwenyewe.
Utakapomwomba Mungu, fahamu kuwa ni lazima akuandae ndipo akupe ulichomwomba, kwani yeye ni Baba mwema ambaye hapendi kutupa vitu ambavyo mwishoni vitatuangamiza sisi wenyewe.
Tutafute kuyajua mapenzi ya Mungu
Hii ni kwa sababu unapoyajua mapenzi ya Mungu, ni rahisi kupokea majibu ya maombi yako pale unapoomba, kwani kunakuwa hakuna upumbavu mwingi ndani yako. Lakini kama huyajui mapenzi ya Mungu na huyafanyi, basi majibu ya maombi yako yatakawia. Haijalishi utaombewa na watumishi wote ulimwenguni, bado kanuni ya Mungu itabaki kuwa ile ile: kupitia madarasa yake.
Kitabu cha Yakobo 4:2-3 kinasema: 2 “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi, 3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.
Tujue kuwa MAOMBI YETU HUPITIA MADARASA ya Mungu kabla ya kujibiwa.
Tujue pia kuwa MAMBO MENGI TUNAYOPITIA NI MADARASA ya kutolewa mawe ndani yetu.