john achila mukumwa
Member
Wana wa Mungu na Binti za Wanadamu kwenye Maandiko ni Nani
Kitabu cha Mwanzo 6 kinasema: 1 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua".
Vile vile, katika Luka 17:26, maandiko yanaposema "kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, Ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu".
Yapo mambo mengi yanapaswa kuchunguzwa, yaliyokuwa yanatokea katika siku za Nuhu.
Tutaangazie jambo moja ambalo ndilo lililopelekea wakati ule dunia yote kuangamizwa. Jambo lenyewe si lingine zaidi ya kuchanganyikana kwa mbegu kati ya wana wa Mungu na binti za wanadamu.
Ni muhimu kufahamu kuwa wana wa Mungu wanaozungumziwa pale sio malaika, kama baadhi ya watu wanavyofikiri. Biblia inasema malaika hawaoi wala hawaolewi, na sisi watakatifu tukishakwenda mbinguni tutafanana na wao (Marko 12:25). Pamoja na hayo, malaika hawana miili ya kidunia, bali wao ni roho watumikao. Biblia inasema hivyo katika Waebrania 1:14; 1Wafalme 22:21-22; 18:10. Wale wanaotajwa pale kama wana wa Mungu ni wanadamu watakatifu wa Mungu, na binti za wanadamu ni binti za wana wa ulimwengu huu. Ndiyo maana unaona baada ya tukio lile, walioadhibiwa kwa gharika ni wanadamu na siyo malaika. Hii ina maana kuwa waliotenda dhambi walikuwa ni wanadamu na siyo malaika.
Je, kwa nini kulitokea makundi hayo mawili wakati huo?
Biblia inatuonesha kuwa tokea mwanzo, kulikuwa na tofauti kati ya zao mbili kuu. Yaani uzao wa Kaini, na ule uzao wa Sethi.
Uzao wa Kaini ulikuwa na tabia zake tofauti kabisa. Kwanza, ulikuwa haumchi Mungu wala hauna habari na Mungu, tofauti na Adamu alivyokuwa mcha Mungu. Pili, ulikuwa ni uzao wa uuaji. Utaona mtoto (uzao) wa Kaini anashuhudia kuwa alikuwa muuaji hata zaidi ya baba yake (Mwanzo 4:23-24). Tatu, ulikuwa ni uzao wa kuoa nje ya utaratibu wa Mungu, kuoa wake wengi (Mwanzo 4:19). Nne, ulikuwa ni uzao wenye ujuzi na maarifa mengi sana ya kidunia. Utaona mwanzoni tu, walishagundua vyuma, chuma, vyombo vya miziki na kuvitumia isivyopasa (Mwanzo 4:20-22).
Uzao wa Sethi, ulikuwa ni uzao mtulivu, walikuwa ni wafugaji tu, na baada ya kuona dunia imeharibika sana na kujitenga mbali na Mungu, wao walienda kinyume na kuanza kuliitia jina la Bwana. Hii ikiwa na maana kuwa walikuwa ni watu wanaomtafuta Mungu, watu wa ibada, watu waliojitenga na mambo maovu, n.k. Hayo tunayaona katika Mwanzo 4:25: “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana”.
Hivyo, dunia ilikuwa inajulikana wazi, kuwa kuna uzao wa Sethi, uliokuwa unajulikana ni uzao wa watu wanaojishughulisha na kumtafuta Mungu kwa bidii na wenye msimamo (kwa sasa tunaweza kusema ni walokole). Aidha, kulikuwa na uzao wa Kaini ambao kwa sasa tuseme ni watu wa ulimwengu huu wasioamini hata kama kuna Mungu, wenye elimu na sayansi na teknolojia ya hali ya juu; na kwa ujuzi wao huo wote, hawamtaki Mungu.
Kwa hiyo, ilikuwa ni rahisi Mungu kuivumilia dunia maadam anaona bado kuna uzao wake unamtafuta yeye na kujitenga na uovu duniani, na unajishughulisha na mambo ya imani. (Kama alivyomwambia Ibrahimu wakati fulani kwamba endapo wakipatikana wenye haki 10 hatateketeza mji Mwanzo 18:32).
Lakini ilifikia wakati, uzao wa Mungu, ambao ndio wale wanaoitwa wana wa Mungu, wakakengeuka, wakajisahau, wakashindwa kuvumilia, walipoona dunia inavutia, watu waovu wanasitawi ulimwenguni, wakaanza kuwaona hao binti wa wana wa kibinadamu jinsi wanavyoishi kidunia. Jinsi wanavyovaa kizinzi, wakikatiza mitaa yao wakiwa na vimini, migongo wazi, wakiwa wamevaa suruali za kubana, wakiwa wamejipamba na mahereni ya dhahabu na kucha za bandia, na mawigi, wasio na aibu wala haya, wakiwa wamejichubua, nk. Wakaingiwa na tamaa. Hapo ndipo na wao wana wa Mungu wakaenda kuoa watu ambao Mungu alishawalaani.
Tukumbuke kuwa Mungu aliwakataza hata wana wa Israeli wasioe binti za mataifa mengine. Jambo hili aliliona pia wakati wa Nuhu, ambayo ni kugeuzwa mioyo. Tukumbuke pia kuwa Sulemani hakulitii, pamoja na kuwa alikuwa ni mtu mwenye hekima na aliyependwa na Mungu sana, lakini wanawake wa mataifa mengine walimgeuza moyo hadi akaenda kufanya ibada za miungu wengine na kufarakana na Mungu.
Kitabu cha Nehemia 13:25 kinasema: "Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. 26 Je, Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli. Lakini, wanawake wageni walimkosesha hata yeye".
Vivyo hivyo, na hawa wana wa Mungu (uzao wa Sethi) walipooana na binti za wanadamu (uzao wa Kaini) kwa kuona kuwa ni warembo na wazuri, wakabadilika tabia moja kwa moja. Na wao pia wakamsahau Mungu, hivyo dunia nzima ikafanana na kuwa kitu kimoja. Wote ni waovu.
Mungu alipoangalia hakuona wa kumuhurumia. Hapo ndipo Mungu alipofikia hatua ya kughahiri na kuiangamiza dunia nzima kwa maji.
Kitabu cha Mwanzo 6 kinasema: 1 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. 5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”.
Unaona, leo hii, mambo yale yale yaliyokuwa yakifanyika wakati wa Nuhu yanajirudia duniani. Je, wana wa Mungu, na binti za wanadamu, ni wakina nani leo?
Wewe kama ni mwanamke, muonekano wako unakutambulisha wewe ni binti wa nani? Kama wewe ni binti wa Kaini, wewe ndiye unaowakosesha wana wa Mungu wengi, kuwapeleka kuzimu. Unategemea vipi adhabu yako siku ile isiwe kubwa zaidi ya wote? Kuambiwa hivyo, siyo kuhukumiwa (Mathayo 18:6 na Marko 9:42). Hujali leo nani anakutamani na nani hakutamani. Siku ile utalia na kuomboleza na hakutakuwa na nafasi ya kurekebisha makosa.
Vile vile, wewe unayejiita mwana wa Mungu, unajichanganya na mambo ya ulimwengu huu. Unaona kuzini kwako ni jambo la kawaida, disko unakwenda, kwenye starehe upo, hujui kuwa unachanganya mbegu yako na mbegu za Kaini. Nawe pia utaangamizwa pamoja na wao, ukifa leo hii: Ezra 9:2 “Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili”.
Kumbuka hili neno “kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu”. Hizi ndizo siku hizo. Urembo na udunia uliopo leo hii ndio uliokuwa katika siku za Nuhu. Udunia upo katika viwango vya juu. Huwezi kupita katika kona mbili-tatu, ukakosa kuona duka au kituo cha kuuza urembo wa wanawake. Mambo haya hayakuwepo wakati wowote kipindi cha nyuma. Shetani anasoma mazingira na kuendana nayo. Fasheni, ni moja ya silaha kuu ya ibilisi katika wakati huu.
Hivyo uwezo wa kubadilishwa na kuwa mtoto wa Mungu kutoka kuwa mtoto wa Kaini, ule uzao wa nyoka, hauji hivi hivi kwa nguvu zako, bali kwa kuzaliwa mara ya pili. Na kuzaliwa mara ya pili ni pamoja na kutubu na kukubali kubatizwa, sawa sawa na Yohana 3:5: "Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu".
Kwa hiyo, wana wa Mungu wanaozungumzwa katika Mwanzo 6:1-2 ni wanadamu wa uzao wa Sethi. Hakuna malaika waliohusika. Malaika ni roho.
Pia, mabinti wa binadamu wanaozungumzwa katika Mwanzo 6:1-2, ni mabinti wa wanadamu, uzao wa Kaini.
Kwa jumla, katika wana wa Mungu na binti za wanadamu walioandikwa katika kitabu cha Mwanzo 6, hakuna ambapo malaika alihusika, bali ni wanadamu wenyewe kutoka makundi mawili yenye maadili tofauti: kundi la Sethi na kundi la Kaini. Sethi na Kaini, wote walikuwa ni watoto wa Adamu.