john achila mukumwa
Member
Fahamu Mtiririko wa Hatua za Ujio wa Yesu Duniani
Hili ni moja ya suala au somo lenye mtafaruku miongoni mwa wakristo. Wengi wameishia hadi kugombana. Wapo wanaoamini kuwa Kanisa litapitia dhiki kuu, ndipo linyakuliwe, na wapo wanaoamini kuwa Kanisa halitapitia dhiki kuu, yaani utaanza kwanza unyakuo ndipo dhiki kuu itafuata.
Kutokana na tofauti hizo, na kwa makusudi, SOMO hili LIMEELEZWA KWA KIREFU hapa, kwani kwa kutoa maelezo mafupi, linaweza lisieleweke inavyopasa kwenye sehemu zenye tofauti katika uelewa, kuhusu mtiririko wa matukio (sequence of events), na hivyo kufanya lengo la somo lisifanikiwe.
Kwa sababu hiyo, msomaji anashauriwa kutenga muda wa kutosha, ili kukamilisha, hata kwa awamu, usomaji wa somo hili hadi mwisho, somo ambalo linaangaza ujio wa Yesu, siku za mwisho.
Inaelekea kuwa kuna jambo moja katika maandiko ambalo halieleweki na wengi. Jambo hilo ni mgawanyiko katika ujio wa Kristo.
Ujio umegawanyika katika hatua kuu 3.
Mtu akishindwa kuzielewa hatua hizo, basi ataona kuwa biblia inamchanganya.
1. UJIO WA KWANZA WA KRISTO
Hii ni hatua ya ujio wa Kristo kuzaliwa duniani kwa lengo la kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye dhambi ya mauti. Huu ni ule wakati Kristo alipozaliwa na Bikira Maria, na kuishi kwa miaka 33 na nusu, kufa, kufufuka na kisha kupaa kwenda mbinguni alikotoka.
2. UJIO WA PILI WA KRISTO
Hii ni hatua ya unyakuo
Huu utahusisha Kristo kuwapokea wateule wake mawinguni katika tendo maarufu lijulikanalo kama unyakuo. Wakati huo, wafu waliopo makaburini watafufuka, na wataungana na watakatifu walio hai, na kwa pamoja watakwenda mawinguni kumlaki Bwana.
Katika ujio huu, Kristo hatashuka duniani, bali atabaki mawinguni. Tutakaponyakuliwa, hatutauliwa roho zetu na miili yetu na kuumbwa upya, hapana. Tutakuwa ni sisi sisi, isipokuwa tutavikwa miili mingine ya utukufu. Ile ya kwanza haitauliwa, hapana, bali tutavikwa miili mipya juu yake.
Ndiyo maana siku ile ya unyakuo, wafu watafufuliwa kwanza warudi katika hali zao walizokuwa nazo wakiwa hai. Kisha miili yao itakutana na ile miili ya mbinguni wafanywe kuwa bora zaidi. Siku hiyo ndiyo utajua lile neno Bwana alilolisema kuwa hautapotea unywele hata mmoja wa vichwa vyenu, litatumika wapi (Luka 21:18).
Watakaonyakuliwa, ndio watakaokwenda mawinguni kumfuata Yesu na kwenda naye mbinguni kwenye makao waliyoandaliwa. Huko mbinguni, ndiko kutakuwa na karamu ya Mwanakondoo. Katika hatua hii, ndipo pia litatimia lile neno la kwenye Luka 17, kuwa:
34 “Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”.
Vile vile, lile Neno kuwa Bwana atakuja ghafla, ndipo litatimia katika hatua hii.
Hiyo ni kama ilivyoandikwa katika 1Wathesalonike 5:1-3:
1 "Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, 2 kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku, 3 Wakati watu bado wanasema, Kuna amani na usalama, "Pengine utakuwa umelala na mume wako/mke wako aliyeokoka, na ghafla utapoamka asubuhi hutamkuta kitandani.
Huu hautakuwa ujio wa kila jicho kumwona Yesu, kwa sababu hatakuja kwa hukumu bali kwa ajili ya kuwachukua wateule wake na kwenda nao mbinguni kwenye karamu aliyowaandalia. Karamu hiyo itachukuwa muda wa miaka 7.
Hivyo, huo hautakuwa wakati wa kila jicho kumwona Yesu mawinguni. Wakati wa kila jicho kumwona utakuwa ni wakati wa ujio wa tatu.
Wakati wa kila jicho kumwona Kristo, biblia inasema mataifa yote yataomboleza, na milima itahama, na visiwa, kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi, na jua litazima na mwezi utakuwa mwekundu kama damu. Kwa ufupi mwisho wa dunia utakuwa umefika. Sasa kama mambo hayo yote yatatokea katika siku ile ya unyakuo, ni nani atakuwa amelala kitandani, au yupo shambani analima, katikati ya dhiki kubwa namna hiyo? Huyo mpinga Kristo atatokea wapi na atawapa watu chapa muda gani?
Hii inadhihirisha kuwa siku ya unyakuo ni nyingine na siku ya ujio wa Kristo ambapo kila jicho litamwona, nayo ni nyingine. Haiwezekani siku ya unyakuo ndiyo iwe siku hiyo hiyo ya kila jicho kumwona, na visiwa na milima kuhama.
Siku ya unyakuo hakutakuwa na ishara yoyote angani, wala jua halitazima. Kutakuwa na ukimya tu kama wa siku zote za kawaida.
3. UJIO WA TATU WA KRISTO
Hii ni hatua ya kutawala dunia kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana
Katika ujio huu, lengo ni kuja kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana (Ufunuo 2:26; 5:10; 11:15).
Baada ya unyakuo kupita katika ujio wa pili, baadhi ya watu watatoweka, hawatakuwepo duniani, na dunia haitaelewa chochote. Wengi watahisi watu wamepotea tu, kama ilivyo kawaida ya watu kupotea-potea na kupatikana.
Na wengine wengi watajua ni habari za kuzusha tu. Taarifa chache zitafika vituoni, lakini mwisho zitaishia kupuuziwa, kama baadhi ya taarifa za watu kupotea zinavyopuuzwa leo, pasipo kujua kuwa Kristo tayari amekwishalinyakua kanisa lake (kundi dogo).
Katikati ya hicho kipindi hicho cha miaka 7 ya karamu ya Mwanakondoo mbinguni, ndiyo utakuwa wakati wa mpinga Kristo kunyanyuka.
Hatua hii imegawanyika katika hatua ndogo 4.
1. Mpinga Kristo kunyanyuka
Ndani ya miaka mitatu na nusu ya kwanza, utakuwa ni wakati wa mpinga Kristo kuwadanganya watu waipokee chapa yake. Wengi wataipokea chapa pasipo kujua, wakidhani ni mfumo mpya tu wa kimaendeleo umezuka, ambao utasaidia watu kutambulika kirahisi. Utakubalika duniani kwa muda mfupi sana, kiasi kwamba mtu atakayeukataa atakuwa anaenda kinyume na serikali, hivyo atatafutwa na kusingiziwa mambo yasiyofaa.
Wachache sana wataipokea kwa kujua kabisa kwamba hii ni chapa, lakini wengi hawatajua, kwa sababu mpinga Kristo hatakuwa mtu mwenye mapembe kama watu wanavyofikiri, bali atakuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana wa kisiasa, kidini, kiuchumi na kijeshi. Na atakuwa ni mtu anayeshika biblia.
Hivyo, hatajulikana na wengi kuwa ndiye mpinga Kristo mwenyewe, kwa sababu ataheshimika kama kiongozi wa dini, atakayeleta amani, hivyo atapewa nguvu na dunia nzima.
2. Mpinga Kristo kuanza dhiki kuu
Dhiki na dhiki kuu ni nini?
Dhiki ni kipindi cha wakati ujao ambapo Bwana atatimiza angalau mambo mawili ya mpango wake:
1. Atakamilisha nidhamu Yake kwa taifa la Israeli (Danieli 9:24)
2. Atawahukumu wasioamini, wenyeji wa dunia wasiomcha Mungu (Ufunuo 6-18).
Urefu wa Dhiki yote ni miaka 7.
Dhiki Kuu ni nusu ya kipindi cha Dhiki, yaani miaka mitatu na nusu ya mwisho.
Kinatofautishwa kutoka kipindi cha Dhiki kwa sababu Mnyama, au Mpinga Kristo, atafunuliwa, na ghadhabu ya Mungu itaongezeka sana wakati huu. Kwa hiyo, ni muhimu katika hatua hii kusisitiza kwamba Dhiki na Dhiki Kuu siyo visawe (synonyms). Dhiki inahusu kipindi kamili cha miaka saba, ambapo "Dhiki Kuu" inahusu nusu (miaka 3 na nusu) au sehemu ya pili ya kipindi cha ile miaka 7 ya dhiki.
Baada ya miaka mitatu na nusu ya kwanza kwisha, wale wachache ambao wataikataa chapa ya Mpinga Kristo, ndio watakaoanza kuipitia DHIKI KUU.
Wengine hawataguswa, wataendelea na shughuli zao za KUUZA NA KUNUNUA vitu bila usumbufu. Lakini, waliokataa, watajaribu kujificha, lakini watakamatwa na kupewa shutuma za uongo na hivyo kukusanywa katika magereza maalum ya mateso. Wakiwa humo, watateswa mateso ambayo hayajawahi kutokea tangu dunia kuumbwa, na watamani kufa lakini wale waliowafunga hawatawaua mapema.
Lakini, mwisho wa siku, watakufa wote. Na karibia na mwisho wa hiyo miaka mitatu na nusu ya mwisho, wataisha wote.
3. Mungu kuadhibu wanadamu waliopokea chapa
Ndipo Mungu ataanza kuwapiga wanadamu wote waliopokea chapa ya mnyama kwa yale mapigo ya vitasa saba, yaliyoandikwa katika Ufunuo 16.
Hii itafanyika ndani ya siku 75 za nyongeza, BAADA ya ile miaka 3 na nusu ya dhiki kuu.
Hapo ndipo Danieli 12:12 anaposema: “Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano (siku 1,335)”. Yaani, heri watakaokuwepo baada ya ile miaka 3 na nusu ya dhiki kuu, pamoja na zile siku 75 za nyongeza.
MATESO YA VITASA SABA
Kitasa ni nini
Kitasa ni kifaa kinachozuia kitu, kama vile mlango, kufunguliwa, na kinaweza kufunguliwa kwa ufunguo. Hivyo, vitasa saba vikikuwa vimefunga hifadhi za adhabu au ghadhabu ya Mungu.
Kitasa cha kwanza
Ufunuo 16:1 “Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi”. 2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake".
Kitasa cha pili
Ufunuo 16:3 “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa".
Kitasa cha tatu
Ufunuo 16:4-7 “Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu".
Kitasa cha nne
Ufunuo 16:8-9 “Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
Kitasa cha tano
Ufunuo 16:10-11 “Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, 11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao".
Pigo hili linamuhusu sana sana yule mnyama aliyewakosesha wanadamu wote kuipokea ile chapa.
Kitasa cha sita
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa WAFALME WATOKAO KATIKA MAWIO YA JUA".
Vita vya Harmagedon
Kitasa cha sita ndicho kinahusu vita vya Harmagedon (Ufunuo 16:12-16), ambayo itapiganwa katika taifa la Israeli, mahali panapojulikana kama Megido.
Wakati huo mataifa yote ulimwenguni yakiongozwa na MATAIFA KUTOKA MAWIO YA JUA, yaani China, Korea, Japani, nchi za Kiarabu, na mengineyo, yakiongozwa na Urusi, yatakusanyika kwenda kufanya vita na taifa la Israeli (Ufunuo 16:14, Ezekieli 38:1-23).
Akilini mwao watadhani wanapambana na Israeli, kumbe wanapambana na Bwana Yesu Kristo mwenyewe, pamoja na watakatifu wake ambao watakuwepo kwa mfumo wa kimalaika wakati huo.
Lakini, baada ya muda mfupi sana, vita vitakwisha, kwa sababu Yesu Kristo siyo mwanadamu. Atawaua wote mara moja kwa Neno Lake, na damu nyingi sana zitachurizika kama mto maeneo yale. Watashangaa tu kuona maiti zilizochinjika chinjika zimelala chini, na aliyewaua haonekani.
Itakuwa kama ilivyokuwa katika kipindi cha mfalme wa Ashuru katika (2Wafalme 19:35), ambapo alimtukana Mungu wa Israeli, na malaika wa Bwana akashuka kwenye kambi ya jeshi lake, akaua wanajeshi wote ambao idadi yao ilikuwa ni watu 180,000. Walipoamka asubuhi, walikuta maiti tu, bali aliyewaua hajulikani.
Ndivyo itakavyokuwa katika vita vya Harmagedon. Biblia inataja majeshi ya wapanda farasi watakaoanguka siku hiyo watakuwa ni elfu ishirini mara elfu kumi. Hiyo ni sawa na watu milioni 200, watakutwa wamechinjika vibaya sana na damu yao nyingi kutiririka. Ndipo ndege wote wanaokula mizoga watakusanyika kuja kula nyama zao (Ufunuo 19:11-21).
Kitasa cha saba
Hiki ndicho hasa kinaizungumzia ile siku ya Bwana.
Ufunuo 16:17-21 “Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta (sawa na kilo 34), ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno". Hili ni pigo la mwisho, na katika hili, ghadhabu ya Mungu imetimia.
Kwa hiyo, katika dhiki kuu, Mpinga Kristo atatesa wale waliokataa chapa, na ndani ya siku 75 baada ya ile miaka 3 na nusu ya pili, Mungu atawaadhibu wale waliokubali chapa.
Mwisho kabisa, miaka hiyo 7 ya dhiki na vitasa itakapoisha, biblia inasema, jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, ishara ya mwana wa Adamu itaanza kuonekana mbinguni.
Ujio rasmi wa tatu
Bwana Yesu mwenyewe, Mfalme wa wafalme, atatokea mawinguni pamoja na jeshi kubwa na watakatifu.
Hilo jeshi kubwa ni la watu wote, siyo tu walio hai, bali hata waliokufa katika Kristo, katika vizazi vyote vya nyuma. Ni pamoja na wakina Petro waliokatwa vichwa, wakina Stephano waliopigwa mawe, wakina Perpetua waliopitia dhiki za kuwekwa kwenye maarena na kufunguliwa wanyama wakali kuwala, wakina Polikapi waliochomwa moto, wakina Antipa, na wengine wengi, na hata wakristo wote wanaopitia dhiki za kiimani hata ambao watakuwa hai hadi ile siku ya kunyakuliwa.
Yesu atakuwa ameshuka kwa ajili ya vita vya Harmagedoni, kwa ajili ya Taifa Teule. Atashuka pia, kwa ajili ya utawala wa miaka 1,000 duniani.
4. Yesu akusanya wateule wake
Taifa la Israeli wakati wa kuja kwa Yesu
Wana wa Israeli au Wayahudi, watabadilisha kabisa msimamo wao kuhusu Masihi Yesu Kristo. Watalia kwa uchungu na kuomboleza huku wakijilaumu kwa nini walimkataa na kumchoma kwa mkuki ubavuni. Kisha, watamkubali kuwa masihi na mwokozi wao (Ufunuo 1:7; Zekaria 12:10-14; 13:6; Isaya 13:9). Ndipo hapo Israeli kama Kondoo, watabaguliwa na kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Sasa unaweza kuuliza, kuwa hao wateule ambao Bwana atawakusanya wakati wa kutokea mawinguni kwa utukufu mwingi ni wakina nani?
Hao watakuwa ni Wayahudi 144,000, waliotiwa muhuri wa Mungu baada ya kuisikia ile injili ya manabii wawili wa kwenye Ufunuo 11. Hao WALIFICHWA MBALI WASIONEKANE NA MPINGA KRISTO, WALA WASIGUSWE NA DHIKI KUU YA VITASA 7 (Ufunuo 12:14-17). Kundi hili la Wayahudi 144,000 ambao walifichwa, ili wawe mbali na yule joka, ndio wanaoitwa wateule. Hawa wakati Kristo atakaokuja ndio watakaokusanywa kutoka pepo nne, na kuletwa juu ya mlima Sayuni uliopo pale Israeli.
Ufunuo 14:1: “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwanakondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, mahali pale pale alipopaa kwenda mbinguni wakati alipotoka duniani mara ya kwanza (Matendo 1:10-12; Zekaria 14:4-5), akiwa na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao”.
Swali la kujiuliza: kitu gani kinachowafanya watu wachanganye mambo? Ni kwa sababu ya kutoelewa kalenda ya Neno la Mungu.
Inaelekea ni wachache wanalijua na kulielewa andiko katika Warumi 11:11-24, linalozungumzia Upofu waliopigwa Wayahudi (Waisraeli). Upofu huo walipigwa wasimwamini Masihi, Yesu Kristo, ili sisi watu wa mataifa tupate Neema.
Kutokana na upofu waliopigwa, iliwafanya wasimwamini kabisa Yesu, na kujikuta wakimtazamia Masihi mwingine.
Na sisi watu wa Mataifa ikawa ni fursa kwetu kumwamini, kwani wale mitume ambao walipaswa watumwe kwa Wayahudi walikuja kwetu, na sisi tukamwamini Yesu. Macho yetu yakafunguliwa, tukaipokea hiyo neema.
Na tumekaa na hiyo neema sasa kwa zaidi ya miaka 2,000. Ndiyo maana huoni ugumu leo kuhubiri injili ya Yesu na watu wakamwamini kirahisi. Neema hii haipo kwa Waisraeli unaowaona leo.
Ukienda Israeli, ukiwaeleza habari za Yesu, wanakuona ni mwendawazimu, wanakupinga kabisa. Ni wachache sana wanaomwamini, na zaidi ya asilimia 90 ya Waisraeli wanamkataa Yesu. Hiyo ni kutokana na upofu waliopigwa. Yaani, neema waliyopokonywa ili tupewe sisi.
Biblia inasema katika Warumi 11, kwamba, hawatakuwa katika hiyo hali ya kutomwamini Yesu, milele. Itafika siku ambapo macho yao yatafumbuliwa. Siku hiyo itakuwa ni zamu ya watu wa mataifa kupitia ukame wa rohoni kama wanayoipitia sasa, Waisraeli.
Siku hiyo itakuwa ni siku ya Neema ya wokovu kuondoka kwa watu wa Mataifa milele, na kuhamia Israeli.
Neema hiyo itahitimishwa na tukio la unyakuo. Kristo atakapolinyakua tu kanisa lake, na mlango wa Neema siku hiyo hiyo utakuwa umefungwa kwa watu wa mataifa, na kubakia kwa Waisraeli peke yao.
Kwa watu wa mataifa, itakuwa hata mtu aombe vipi, hakutakuwa na rehema. Roho Mtakatifu atahamia kwa Waisraeli. Waisraeli watahuzunika sana na kujilaumu ilikuwaje mpaka wakamkataa Masihi kwa miaka yote hiyo.
Kwa kupitia injili ya wale manabii wawili, ndio watapatikana idadi ile 144,000. Idadi hiyo ni kutokana na watu 12,000 kutoka kila kabila miongoni mwa yale makabila 12 ya Israeli (Ufunuo 7:4-8).
Hao ndio wateule 144,000 watakaokusanywa katika Mlima Sayuni.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa mataifa uwasili. 26. Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Hivyo basi, siyo kanisa ambalo litakusanywa kutoka pembe nne, bali ni Wayahudi hao 144,000, ambao waliisikia ile injili iliyohubiriwa na wale manabii wawili (Ufunuo 11:4-12), na kutiwa muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.
Kanisa lilikwishanyakuliwa katika ujio wa pili, lilikuwa kwenye utukufu, na ndilo lililorudi na Kristo duniani baada ya ile miaka 7.
MATUKIO BAADA YA ILE DHIKI KUU
1. Kufungwa kwa Shetani na roho waovu
Baada ya vita hivi, Shetani atashikwa na kufungwa miaka elfu moja (Ufunuo 20:1-3) na hapo ndipo utakapoanza Utawala wa miaka 1,000 wa Yesu Kristo duniani.
Biblia inaonyesha malaika atamtupa Shetani na roho waovu katika “abiso,” yaani, watakuwa katika hali ya kutotenda, kama ya wafu (Ufunuo 20:1-3).
2. Ufalme wa Mungu kuanza utawala wa miaka 1,000
Utawala wa miaka 1,000 ni utawala ambao utakuja kuanza hapa duniani, ambapo Kristo atatawala na wateule wake. Maandiko yanasema mbinguni hatutakaa milele. Tutakaa kule kwa kipindi cha miaka 7 tu, kisha baada ya hapo tutarudi duniani kutawala pamoja na Yesu kwa miaka 1,000.
Huu utakuwa ni utawala wa amani. Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana kondoo. Chui atalala pamoja na mwana-mbuzi. Ndama na mwana-simba watakuwa pamoja na mtoto mdogo atawaongoza. Simba atakula majani kama ng'ombe. Mtoto anyonyaye atacheza kwenye tundu la nyoka (Isaya 11:6-9).
Ufalme wa Mungu utaanza utawala wake wa miaka 1,000, ambao utawaletea wanadamu baraka nyingi (Ufunuo 5:9-10; 20:4, 6). “Umati mkubwa” ambao hauwezi kuhesabiwa ‘utatoka katika ile dhiki kuu,’ na kuanza kuishi duniani wakati wa ile miaka elfu moja (Ufunuo 7:9, 14; Zaburi 37:9-11).
Watoto watakaozaliwa katika utawala huo wa miaka 1,000, biblia inasema tutakaowatawala hao, ndio watakaoitwa mataifa, wakati huo. Wale watakaorudi na Bwana kutoka mawinguni watakuwa wafalme juu yao, na Yesu Kristo atakuwa Mfalme wa Wafalme.
Hawatakuwa na miili kama ya kwao ya asili, kwa sababu wameshavuka huko, na kupewa miili ya utukufu wakati wa unyakuo, miili ambayo ipo kama ya malaika, isiyozeeka, isiyo na tamaa, isiyosikia njaa, isiyochoka.
Kutakuwa hakuna kuoa wala kuolewa wala kuzaliana, watakuwa kama malaika katika hii dunia, utukufu wao utakuwa mbali sana na hawa watu watakaozaliwa katika utawala huo.
3. Shetani atafunguliwa kwa kitambo kidogo
Mwishoni mwa hiyo miaka 1,000 kwisha, Bwana Yesu atamruhusu shetani afunguliwe kwa kitambo kidogo.
Kwa nini aruhusiwe? Ni ili awajaribu mataifa, awajaribu hao watoto waliozaliwa ndani ya huo utawala. Maana, ni sheria ya Mungu, kila kiumbe chake kijaribiwe (Ufunuo 20:7-10). Hata sasa tunajaribiwa na huyo huyo shetani. Hivyo, ni sharti na wao wajaribiwe.
4. Jaribio la mapinduzi juu ya utawala wa Kristo
Shetani atakapofunguliwa, wapo baadhi watakaodanganyika naye na wachache watakaomkataa na kudumu katika kuutii utawala wa amani wa Bwana Yesu Kristo.
Wengi watadanganyika kama tu shetani anavyowadanganya wengi leo, wasimwamini Bwana Yesu Kristo na uweza wake.
Kwa hiyo, wataungana pamoja na kutaka kuleta mapinduzi juu ya utawala wa Kristo. Magugu na ngano vitajitenga. Kabla hawajajaribu kufanya lolote, litatokea kama lililotokea Harmagedon.
Moto utawateketeza pale pale walipo na uwingi wao. Hatapona hata mmoja. Wachache waliokataa kujiunga na hilo jeshi kushindana na Bwana, watahifadhiwa na watakuwa wameshinda (Ufunuo 20:7-10).
Ufunuo 20:7 “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele".
5. Hukumu ya ulimwengu
Baada ya hilo jaribio kwisha, kutakuwa hakuna tena kizazi kingine cha wanadamu kilichosalia kwa ajili ya kujaribiwa.
Wakati uliobakia ni wa hukumu. Kila mtu kulipwa kama kazi yake ilivyokuwa.
Kuanzia mwanzo wa wanadamu wote mpaka mwisho wa ile miaka 1,000, watafufuliwa. Walioko kuzimu watafufuliwa. Vitabu vitafunguliwa (kila mtu ana cha kwake).
Kitabu kimoja cha uzima kitafunguliwa, na endapo mtu hakuonekana jina lake kwenye kitabu cha uzima, atatupwa katika lile ziwa la moto (Ufunuo 20:11-15).
Siku hiyo watu wengi wataona sababu ya wao kupelekwa katika ziwa la moto. Itakuwa ni uchungu usioelezeka. Kwa sababu kila kitu kitawekwa wazi mbele ya mashahidi wengi.
6. Mbingu mpya na nchi mpya
Na baada ya hukumu kwisha, itakuja mbingu mpya na nchi mpya. Mbingu mpya na nchi mpya ni hii hii dunia, isipokuwa itavikwa na utukufu usioelezeka. Itakuwa ni sehemu nzuri ajabu.
7. Muda kuondoka na umilele kuanza
Baada ya hiyo miaka 1,000, ndipo kitu kinachoitwa MUDA kitaondoka, na UMILELE, ambao hauna muda, utaanza. Huko kutakuwa hakuna tena muda, ni mambo mapya, wala hakuna bahari tena (Ufunuo 21:1-8).
MASWALI KWA MSOMAJI:
1. Kwa kuwa unyakuo wa Kanisa lazima utokee kabla ya Mpinga Kristo kufunuliwa, je, tunakaribia mwisho wa enzi hiyo?
2. Kama unyakuo wa Kanisa ungetokea leo,
je, wale unaowapenda, ambao wataachwa
nyuma, wangejua kwa nini una kosa?