Kasomi
JT Founder
Yoweri Museveni aliwahi kusema "Tatizo la Afrika kwa ujumla, na hasa Uganda, si watu bali ni viongozi wanaotaka kuzidi kukaa madarakani milele." Alisema kauli hii yeye mwenyewe wakati wa hotuba yake ya kwanza siku aliyoingia madarakani Januari 29,1986
Huku akidai kubadilisha tatizo Hilo.
Lakini kufikia mwaka 2005 maoni yake yalionekana kubadilika na katiba ya Uganda ikafanyiwa marekebisho, na kuondoa ukomo wa mihula mingapi ambayo rais anaweza kuhudumu.
Mnamo 2017, ukomo wa umri wa wagombea urais pia uliondolewa - hatua iliyosababisha wabunge kurusha viti katika rabsha bungeni.
Museveni pia amekabiliwa na madai kwamba amedhoofisha uhuru wa taasisi muhimu.
Hasa, mahakama ya Uganda imeshutumiwa kwa kuajiri wale wanaoitwa "majaji wa kada" ambao uaminifu wao upo kwa serikali.
Majaji wanapokwenda kinyume na serikali, wakati fulani wamejikuta wakizozana na mamlaka.
Kwa mfano, mwezi Desemba 2005, maafisa wa usalama waliokuwa na silaha walivamia Mahakama Kuu katika mji mkuu, Kampala, na kuwakamata tena washukiwa wa kundi la waasi, ambao walikuwa wametoka kuachiliwa kwa mashtaka ya uhaini.
Vyombo vya habari pia vimetishiwa uhuru wake. Kwa juu juu, Uganda ina tasnia ya habari iliyochangamka, lakini vyombo vingi vimevamiwa na wanahabari kuzuiliwa.
Pengine jambo muhimu zaidi katika maisha marefu ya Museveni ni kupunguzwa kwa nguvu za upinzani.
Ilipodhihirika kuwa Museveni hakukusudia kuondoka madarakani, baadhi ya washirika wake wa zamani walianza kujitenga. Walipofanya hivyo, vyombo vya usalama vilielekeza macho yao kwao.
Kwa mfano, Kizza Besigye wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change, ambaye wakati mmoja alikuwa daktari wa Museveni, aligombea kwa mara ya kwanza dhidi ya rais mwaka 2001.
Tangu wakati huo, amekamatwa na kufunguliwa mashtaka mara kadhaa. Mnamo 2024, alitoweka kwa njia isiyoeleweka jijini Nairobi, na kufikishwa siku nne baadaye katika mahakama ya kijeshi ya Uganda. Anasalia gerezani kwa mashtaka ya uhaini, ambayo anakanusha.
Bobi wine kwasasa Ndiye mpinzani wake mkuu ambaye amekuwa akizongwa na vikwazo Mbalimbali ikiwemo Kuwekwa gerezani mara kadhaa.
Je maoni yako ni yapi hasa katika hili