Jina langu lilikatwa Miaka 2 iliyopita - Mpina

Kasomi

JT Founder
1755171110423.jpg

UPDATES "Kumekuwa na mabadiliko mengi ya viongozi ndani ya miaka minne, najiuliza kama mabadiliko haya shida ipo kwa watumishi au kwa anayebadili. Alikuwa akinipongeza tena kwa barua n azote ninazo. Nilikuwa naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na mwaka 2017 akanirecommend niwe Waziri. Mwaka 2022 niliona tunaanza kuwa mbalimbali, na hata baadhi ya mawaziri. Ilifika kipindi nikasukiwa mipango ya kuuawa na kuna wakati nilisimamishwa uwakilishi wa wananchi wangu bungeni kisa niliibua hoja ya sukari.

Nimeanza kusikia,wewe unampiga vita Mama, wewe unampiga Rais.Nimeomba appointments ya kukutana na rais lakini haikuwezekana. Taarifa za jina langu kukatwa zimetangazwa miaka miwili iliyopita,kitu ambacho ni kinyume Cha Sheria na Chama.

"Ninagombea urais ili niende kukomesha mifumo ya kidhalimu iliyopo ndani ya chama Cha CCM. Mwalimu Nyerere alisema "Msipoyapata mabadiliko ndani ya CCM,mtayapata nje ya CCM". Hivyo kupitia ACT Wazalendo naenda kuyaleta mabadiliko haya.Sisi na ACT-WAZALENDO tunakwenda kuwashughulikia mafisadi”Mgombea urais kupitia chama Cha ACT-Wazalendo akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini leo tarehe 14 Agost, 2025 katika Jengo la Maalim Seif, Dar Es Salaam.
 
Majaji wanatakiwa washughulikie hii kesi mapema iishe Jamaal apate walau wiki mbili za kampeni kabla ya uchaguzi mkuu!walau anogeshe uchaguzi coz was mwaka huu umepoa sana!!!

KAZI na utu tunasonga mbele!
 
Majaji wanatakiwa washughulikie hii kesi mapema iishe Jamaal apate walau wiki mbili za kampeni kabla ya uchaguzi mkuu!walau anogeshe uchaguzi coz was mwaka huu umepoa sana!!!

KAZI na utu tunasonga mbele!
Walitoa siku 5 lakini naona bado Tu ila wafanye haraka kweli walau uchaguzi uwe na radha
 
Back
Top