Kwa Nini Snapchat Inashindwa Kukua Wakati TikTok na Facebook Zinapanda Kwa Kasi

Kasomi

JT Founder
Kwa Nini Snapchat Inashindwa Kukua Wakati TikTok na Facebook Zinapanda Kwa Kasi
250px-Snapchat_logo.svg.png

Snapchat bado inatumiwa na vijana wengi duniani, lakini ripoti mpya zinaonyesha kuwa ukuaji wake wa mapato unasuasua, hasa ukilinganisha na TikTok na Facebook ambao wanaendelea kuimarika kwa kasi.

Tofauti kubwa ipo kwenye matumizi ya kila jukwaa. Snapchat hutumika zaidi kutumiana ujumbe binafsi kati ya marafiki, huku TikTok ikitoa burudani ya video na Facebook likiwa jukwaa la matangazo na mawasiliano. Watangazaji hupendelea majukwaa yenye hadhira ya watu wazima zaidi (miaka 25 hadi 54), wakati Snapchat lina watumiaji wengi wa umri mdogo – kundi lisilo na mvuto mkubwa kwa matangazo.

Aidha, sheria mpya nchini Australia inayopiga marufuku mitandao kwa watoto chini ya miaka 16 huenda ikaathiri sana Snapchat, kwani wengi wa watumiaji wake ni vijana.

Je, Snapchat litajipanga vipi kukabiliana na mabadiliko haya?
 

Similar threads

Back
Top