Fahamu kuhusu Google data center (sehemu ya kuhifadhi data za Google)

Kasomi

JT Founder
1666127355545.jpg

1666127359952.jpg

Hiyo ndio sehemu ya Google ambayo hutumika kuhifadhia data zote za internet inaitwa Google data center.

Unaambiwa hapo kwa kila sekunde wanapata maombi zaidi ya watu 63,000 na 5.6 bilioni kwa siku wanaotafuta data fulani kutoka sehemu zote Duniani

Ata hii post au hiyo comment yako tayari ipo apo na imeshaifadhiwa, izo memes zote kwenye account yako zipo hapo.

Sehemu hiyo ipo Marekani jimboni California, katika jiji la san jose na san Francisco, maarufu kama silicon valley.

Unaambiwa hiyo silicon valley ndio kiini cha teknolojia ya juu na ufumbuzi duniani.

Ndio sehemu tajiri zaidi duniani yani ingekuwa nchi basi ingekuwa nchi yenye uchumi wajuu zaidi.

Ndio nyumbani kwa watu wenye akili unaambiwa katika kila watu 20 utakao Kutana nao, 8 ni mainjinia , 7 ni wafanyakazi wa nafasi zingine 2 ni wakurugenzi/C.E.O wa kampuni fulani, 2 watalii au wamekuja kujifunza na 1 ndo raia mzaliwa wa hapo.

Ndio sehemu wananchi wake wana uchumi mkubwa duniani baada ya Zurich na Norway yani kwa mwananchi wa kawaida huwa na kipato cha si chini ya tsh million 800_1b kwa mwaka.

Silicon valley ndio sehemu ambayo unaweza kwenda hotelini ukakutana na mmliki wa facebook , mack zuckeberg, jeff bezos, elon musk, bill gate na wengine.

Apo ndio nyumbani kwa makampuni makubwa kalibia yote duniani ya teknolojia ya juu unayo yajua.

Apo unakutana na wafanyakazi wenye vitambulisho vya facebook, apple, Microsoft, Google, Amazon,adobe, Tesla, Intel, Oracle, Netflix, YouTube, Uber, zoom, Twitter, Instagram & whatsapp n.k

Ndio sehemu ambayo hawana majivuno kuhusu elimu yao, kwani asilimia 85 ya wafanyakazi hapo wamesoma katika vyuo 10 bora duniani, Kila utakae muuliza utasikia nimemaliza Havard university, MIT, Stanford University, CIT, Oxford University n.k.

Apo hata mfuta vioo ni mbobezi na anaelimu na utakuta ana futa vioo lakini pembeni ana project yake ya kuvumbua njia nzuri ya kufuta vioo ,kila mmoja hapo anaubunifu.
 
Back
Top