Watumiaji wa WhatsApp wataweza kuweka nyimbo kwenye status

Kasomi

JT Founder
1728631288645.jpg

Kampuni ya Meta, ambayo ndio kampuni inayomiliki Instagram, Facebook, WhatsApp, Threads na vifaa mbalimbali; imeingia mkataba mkubwa na kampuni ya Universal Music Group (WMG).

Mkataba mpya wa Meta na WMG utaruhusu Meta kuweka mfumo wa nyimbo kwenye Status za WhatsApp. Watumiaji wa WhatsApp watakuwa na uwezo wa kutafuta na kuweka nyimbo kwenye Status zao; kama inavyofanyika kwenye Instagram Story.

Meta na WMG zilianza ushirikiano mwaka 2018, zikaboresha mkataba mwaka 2020 na mwaka huu zimeboresha zaidi na kuweka mkataba mkubwa wa miaka mingi na ambao utaruhusu na WhatsApp kuwa na miziki.

WhatsApp imeingia katika orodha ya platform ambazo zitapata nafasi hii. Kama ilivyo kwenye Instagram na Facebook, unaweza kuchagua wimbo kwenye Insta Story; watumiaji wa WhatsApp watakuja kupata uwezo huo wa kuweka nyimbo kwenye Status zao.
 

Similar threads

Back
Top