Advertise here

Watumiaji wa Windows watalazimika kulipia app ya Notepad ili kupata features mpya

Kasomi

JT Founder
Watumiaji wa Windows watalazimika kulipia app ya Notepad ili kupata features mpya.
1741335347505.jpg

Kwa zaidi ya miaka 42, app ya Notepad ni app ya bure ambayo imekuwa ikipatikana ndani ya mfumo wa kompyuta ambazo zinatumia Windows. Ni app ya kuandika notes, codes, texts na kazi simple za maandishi.

Microsoft itaiweka Notepad katika huduma zake za kulipia za Microsoft 365 hivyo watumiaji watalazimika kulipia ili kupata features za kuandika kwa kutumia AI. Kwa matumizi ya kawaida na limited words bado itakuwa bure lakini kupata features nyingi na kuwa na uhuru wa kuitumia, watumiaji wa Windows watalazimika kuilipia.

Akili Bandia imekuwa sababu kubwa ya apps nyingi kuongeza gharama za kuzilipia na imekuwa sababu ya app nyingi ambazo zilikuwa zinapatikana bure zinaanza kuwa na huduma za kulipia. Mfano Adobe imeongeza gharama kwa sababu ya AI, kitu ambacho kinapingwa na wengi.

Apple ni kampuni pekee ambayo imeamua akili bandia yake itakuwa inapatikana bure kwenye vifaa vyake vyote. Microsoft haijaweka AI ya bure, lazima mtu alipie kupata features nyingi za AI. Watumiaji wa macOS wanapata ofa nyingi za AI bure kuliko watumiaji wa Windows.
 

Similar threads

Back
Top