Advertise here

ANGALIZO: Kama Unataka Account yako ibaki Salama, epuka hili

Kasomi

JT Founder
⚠️ ANGALIZO: KAMA UNATAKA ACCOUNT YAKO IBAKI SALAMA, EPUKA HILI.
FB_IMG_1738597560359.jpg

Kwa sasa kumekuwa na wimbi kubwa la watu kuibiwa account zao za facebook tena kupitia account za watu wao wa karibu, kupitia njia ya Messenger au Facebook Post.

Nitakuja kuwapa makala kamili juu ya kinachofanyika ila kwa sasa epuka kujihusisha na mambo haya ili kulinda account yako.
1. Epuka kuchat Messenger na mtu ambaye una wasiwasi nae.

2. Epuka kurespond kwa mtu anayekupa mchongo wa pesa kwa kujiunga na promosheni, msaada wa kifedha n.k kwa mfano fedha kutoka WHO, UNICEF, WORD FUND n.k

3. Epuka kucomment kwenye post zinazoelezea njia ya kupata pesa kutoka kwenye mashirika kama niliyotaja hapo juu Namba 2, mikopo kutoka kwa taasisi au watu maarufu kama vile wabunge, wakuu wa wilaya au vyombo vikubwa vya habari kama Azam Media.

4. Epuka kuomba mikopo kutoka kwenye online platform ambazo zimekuwa zikijitangaza sana hasa facebook.

5. Ukipata ujumbe wowote wa OTP kwenye simu yako au email yako wa kutaka kubadili password usihangaike nao. Jua upo hatarini.

Hapo juu nimesema kuwa wengi wanaibiwa account zao kupitia account za watu wanaojuana nao au wanaofahamiaana humu Facebook. Cha kukujuza tu ni kuwa hiyo account inakuwa tayari imeshaibiwa na huyo unayechat nae si yule unayemjua wewe bali ni mdukuaji anafanya hivyo akijua kuwa utaingia mkenge kutokana na wewe kuamini kuwa anayekupa mchongo ni jamaa yako.

Mfano mzuri ni kwenye hiyo picha ya pili hapo unaweza angalia huyo alijaribu kunitext Messenger na Account ya mtu wangu wa karibu sana ili aniingize mkenge.
 

Similar threads

Back
Top