Rais wa FIFA Gianni Infantino amemtaja rapa Drake ku performe World Cup Halftime Show 2026

Kasomi

JT Founder
Rais wa FIFA Gianni Infantino amemtaja rapa Drake ku-performe World Cup Halftime Show 2026 baada ya kuvutiwa na alichokifanya Kendrick Lamar kwenye Super Bowl.
Untitled-design-41.png

Infantino anasema idea ya kumleta Drake kuburudisha fainali ya World Cup ni nzuri sababu mshindani wake Kendrick Lamar amefanya vizuri na kumdiss kwenye Super Bowl.

"Nina wazo zuri la World Cup Halftime, ulikuwepo The Super Bowl Kendrick Lamar akim-diss Drake, kwa hiyo tunaweza kutengeneza ushindani kidogo" amesema Gianni Infantino

World Cup inayofuata mwakani 2026 itachezwa katika nchi 3 (USA,Canada na Mexico) na mechi ya ufunguzi itachezwa jiji la Toronto, Canada anapotokea Drake.
 
Back
Top