Advertise here

Majimbo Mapya 8 ya Uchaguzi yatangazwa

Kasomi

JT Founder
Mkoa wa Dar es salaam yameanzishwa majimbo mawili ya uchaguzi, Mosi jimbo la Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jimbo la Kivule, Pili jimbo la Mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.

Mkoa wa Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo jimbo la uchaguzi l Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo la uchaguzi la Mtumba.

Mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo jimbo la uchaguzi la Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la uchaguzi la Uyole.

Mkoa wa Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la uchaguzi la Bariadi mjini.

Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili, Jimbo la uchaguzi la Busanda limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Katoro na pili jimbo la uchaguzi Chato na kuanzishwa jimbo jipya la uchaguzi la Chato Kusini.

Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambalo jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la uchaguzi la Itwangi"

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 amesema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini.
 
Back
Top