Advertise here

Tangazo La Kubadilika Tarehe Ya Usaili Wasimamizi wa uchaguzi na Makarani Jimbo la Kakonko

Kasomi

JT Founder
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kakonko anapenda kuwajulisha kuwa tarehe ya Usaili kwa Wasimamizi wa Vituo, Wasimamizi wasaidizi na Makarani Waongozaji imebadilika kutoka tarehe 08/10/2025 badala yake usaili utafanyika tarehe 10/10/2025 kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Aidha, vituo vya kufanyia usaili kanda za usaili hazijabadilika. Msailiwa anatakiwa kufika kwenye usaili akiwa na nyaraka zake zinazomtambulisha ikiwa ni pamoja na mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo;- Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya udereva.

Mabadiliko haya yamefanyika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
IMG-20251007-WA0001.jpg

Pia soma hapa

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA, WASIMAMIZI WASAIDIZI NA MAKARANI WAONGOZAJI
 

Similar threads

Back
Top