Kasomi
JT Founder
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, ametupwa nje ya mbio za kuwania tena ubunge kupitia CCM mwaka huu!
Taarifa kutoka vikao vya chama ngazi ya wilaya ya Meatu na mkoa wa Simiyu zinasema jina la Mpina halikupendekezwa kuendelea na mchakato wa uteuzi. Hii ni baada ya kamati ya siasa ya CCM kumwondoa kwenye orodha ya wagombea.
Mpina, ambaye amejulikana kwa miaka ya hivi karibuni kwa msimamo wake mkali na kuibana serikali Bungeni, sasa amewekwa pembeni.
Majina matatu Waliopitishwa kwenda hatua ya juu ya mchakato ni:
Hata hivyo, bado kuna nafasi ya mwisho, kwani Kamati Kuu ya CCM Taifa inaweza kuamua kurudisha jina lolote iliyoona linafaa—ikiwemo la Mpina.
Credit: Halisimax