Uzi Maalumu wa Je, Wajua?

Kasomi

JT Founder
Huu ni Uzi Maalumu wa kuweka na kujuzana Mambo tusiyo yakua na kufahamishana.
====

Je, wajua Mkoa wa Dar es salaam una idadi kubwa ya Watu kuzidi Nchi ya Croatia?
Mkoa wa Dar es Salaam una watu wengi zaidi, 5,282,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini Tanzania wakati Croatia ina idadi ya Watu 4,284,889 kulingana na sensa ya mwaka 2011
Hr-map.png
 
Je, wajua Mwaka 2007, serikali ya Australia ilitumia zaidi ya $84M (Tzs. Bilioni 196) kwaajili ya kuunda mfumo wa kuchuja video za ngono mtandaoni.

Baada ya kuachiwa, kijana wa miaka 16, Toom Wood ndani ya dakika 30 tu aliweza kuudukua mfumo huo!
 
Mwezini kuna uwepo wa gesi ya Helium-3 ambayo kama itawezekana kuchimbwa na kuletwa Duniani, itaweza kuzalisha nguvu ya nishati yenye nguvu sawa na nishati ya Nyuklia na kutumika Dunia nzima kwa zaidi ya miaka 1,000.
 
Je, wajua kuhusu haya? Fahamu Leo

→Itakuchukua Muda zaidi kutamka neno ‘WWW’ kuliko kirefu chake ambacho ni 'World Wide Web'.
→Mr.bean ana Master's degree ya Umeme.
→Koala, hawa Viumbe hutumia 99% ya Maisha yao Kula&Kulala, na 1% iliyobaki hutumika kutafuta Mwenza😊 ambapo kama asipompata hurudi na Kulala tena.
→'Kicheche' ni mnyama ambaye hufanya mapenzi angalau Mara ‘66’ kwa Siku.
→Ice land ndo nchi Pekee isiyo na mbu yoyote , nyoka na reptile wengine.

→Biblia iliandikwa Kitambo sana hata kabla ya kuweko kwa kalamu na karatasi!
→Ni watu Watatu tu Duniani ambao hawakuzaliwa kwa jinsi ya mapenzi ya kimwili, –Adam, Eva na Yesu.
→Nuhu alikua na Miaka 600 pindi anamaliza kujenga Safina.
→Yohana mbatizaji alikua Nabii mkubwa japo hakuwahi kufanya muujiza wowote.
→Samson aliua watu Wengi zaidi wakati wa kifo chake kuliko enzi za uhai wake.
→Aliyekata nywele za Samson sio Delilah kama wengi wanavyodhani, Delilah alimfanya alale tu {Waamuzi 16:19}
→Sara na Ibrahim walikua watoto wa Baba mmoja {Mwanzo 20:12}.
→Kipi kilianza, Kuku au Yai? Jibu liko wazi kwenye Biblia {Mwanzo 1:20-21}. Kuku ndo alianza!
→Biblia inaonyesha sehemu pekee Yesu aliandika ni ardhini {Yohana 8:6,8}
→Dunia ilifunikwa kikamilifu na Maji Mara mbili tu.
o1: Katika mwanzo wa Uumbaji.
o2: Katika kipindi cha Gharika.
→Dunia mpya haitakuwa na Bahari {Ufunuo 21:1}.
→Hakutakua na Kuoana wala ⁿdoa kule Mbinguni! { Mk 12:25 }
→Kitabu cha mwisho kuandikwa kwenye Biblia, sio ‘Ufunuo’ bali ni ‘3 Yohana’.
→Kitabu kikongwe au cha Zamani kwenye Biblia sio ‘Mwanzo’ bali ni ‘Ayubu’
→Biblia haijasema tunda alilokatazwa Adam na Eva kula lilikua ni Apple.
→Soma,Yohana 3:16 inaonyesha wakati (uliopita, uliopo na Ujao).
→Mungu aliifanya punda kuongea {Hesabu 22:28}.Lakini pia tusisahau kwenye kitabu cha ‘Mwanzo’, nyoka aliongea pia.
→Biblia inazungumzia wanawake watatu wazuri zaidi ya wote Dunia nzima {Ayubu 42:15}
→Je wajua, Siku 40 hupita(embryo kuwa fetus), Wiki 40 hupita ili mtoto kuzaliwa(= Miezi 9), Siku 40 hupita pia kuanua matanga pale mtu anapokufa.
 
Back
Top