Advertise here

Dagaa ni watamu kama hutozingatia harufu ya mishikaki kwa jirani

Kasomi

JT Founder
Anaandika Emmanuel Minga

Dagaa ni watamu kama hutozingatia harufu ya mishikaki kwa jirani.

Wengi wetu huwa tunachanganywa na harufu za mishikaki na tunazila kula dagaa tulizopika na kutamani mishikaki ambayo hatuna uwezo wa kuinunua kwa wakati huo.

Hiki ndicho kinachowashawishi wengi waende kula kwa jirani zao ingawa kwenye nyumba zao kuna vyakula.

Ni kwamba hawataki kukubaliana na hali zao na wanataka kukimbilia kwenye viwango ambavyo wao hawajafikia.

Na kumbuka ukienda kwa jirani kufuata mishikaki hiyo usishangae na ujiandae kuwa mtumwa wao watakutumia muda wowote wanaotaka na kukutuma kokote wanako taka Kwa sababu umejipeleka mwenyewe na pua zako zinazotamani vitamu usivyovigharamia.

Cha kwako una uhuru nacho, cha jirani ni utumwa hata kama ni kitamu.

Cha kwako unauhakika nacho vile unakiandaa , lakini cha jirani hujui amekiandaaje, hujui ndani kuna nini, harufu inakuponza.

Dagaa zako unajipangia muda wa kula, mishikaki ya jirani yako unapangiwa muda wa kula.

Kwenu "unakula kazi ya mikono yako , ni jasho lako unastahili", kwa jirani yako "amelaaniwa alaye jasho la mtu mwingine".

Asomaye na afahamu????

HEKIMA YA MAHUSIANO

E .M✍️

letchangeourworld
 

Similar threads

Back
Top