Kasomi

JT Founder
Vijana wanne kati ya 600 wameibuka Washindi wa Shindano la “CyberChampions” lililoandaliwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (@tcra_tanzania), likihusisha Vyuo zaidi ya 40 kutoka Taasisi mbalimbali za elimu ya juu Nchini.
1739004619458.jpg

Washindi hao ni Amani Nsemwa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyeshika nafasi ya kwanza, John Mange kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) aliyeshika nafasi ya pili, Julius Mpagama kutoka Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) aliyeshika nafasi ya tatu na Rebeca Kubanda kutoka UDOM aliyeshinda kwa upande wa Washiriki wa kike.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari amewakabidhi Washindi hao zawadi ambazo ni kompyuta mpakato pamoja na kufadhiliwa gharama za mafunzo (professional certification) pamoja na zawadi iliyotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ya kufanya internship katika kituo cha utafiti na ubunifu e-GA Februari 6, 2025 katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, Shindano hilo lina lengo la kuibua vipaji, kuimarisha uelewa wa usalama mtandaoni na kuwaandaa Vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijiti.

Mwaka huu idadi ya Washiriki imeongezeka ikilinganishwa na miaka iliyopita.
 

Similar threads

Back
Top