Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania)

Kasomi

JT Founder
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (kwa Kiingereza: Open University of Tanzania) ni chuo kikuu kinachotoa kozi za cheti, stashahada na shahada kupita masomo ya mbali (Distance Learning). Makao makuu yako Dar es Salaam, Tanzania. Chuo Kikuu Huria kina takribani wanafunzi 70,000 kutoka ngazi mbalimbali za kitaaluma.

Historia

Kilianzishwa mwaka 1992 kwa kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. Sheria hiyo ilipata nguvu ya utendaji rasmi tarehe 1 Machi 1993 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 55 ya gazeti lake rasmi.

Mwaka 1994, Januari 19 Makamu Mkuu wa kwanza wa Chuo alishika madaraka na mwezi huohuo walisajiliwa wanafunzi wa awamu ya kwanza.

Mwaka 2007 kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilianza kutumia sheria na taratibu zake za ndani ya chuo toleo la mwaka (2007) katika shughuli zake za kiutawala.

Taaluma

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa stashahada, diploma na shahada mbalimbali kupitia elimu ya kimtandao au elimu ya masafa ya juu kwa njia ya tehama au nyenzo nyingine mbalimbali za kiteknolojia. Shughuli za chuo zinafanyika na kutoa huduma katika viwango vya utendaji na usimamiaji wa baraza la vyuo vikuu Tanzania (TCU). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa programu takribani 125.

Vituo

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina vituo kwenye mikoa zaidi ya 30 nchini Tanzania; hii ni kujumlisha na vituo vya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (Unguja na Pemba), Kenya vituo viwili (Chuo cha Egerton na Njoro), Rwanda (eneo la Kibungo), Uganda na Namibia (Chuo cha Triumph).

Vituo vingine vya mashirikiano ya ndani ni ACDE-TCC (African Council for Distance Education- Technical Collaboration Committee), CECED (Centre for Economics and Community Economic Development), SADC ODL CoS TE (SADC Centre of Specialization in Teacher Education).

Chuo Kikuu Huria kina vituo vya kusomea takribani 69 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitivo

Ina:

•Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii

•Kitivo cha Elimu

•Kitivo cha Sheria

•Kitivo cha Uongozi wa Biashara

•Kitivo cha Sayansi, Teknolojia na Masomo ya Mazingira

•Taasisi ya kuyaendeleza masomo

•Taasisi ya Teknolojia ya Elimu

•Kurugenzi ya Huduma za Mikoa

•Kurugenzi ya Utafiti na Masomo ya baada ya Shahada
 
Ni kweli hata mimi ni mnufaika wa chuo hiki.
 
Ada zake zikoje?
Ada za masomo katika Chuo kikukuu huria (OUT) hutofautiana kulingana na kozi, ngazi za masomo, na mwelekeo wa kielimu. Hapa ni muhtasari wa muundo wa ada:

Certificate Programmes: Ada ni ya chini, na huanzia Tsh 300,000 hadi Sh 600,000 kwa mwaka kulingana na kozi. Ada hii ni pamoja na ada ya usajili, mafunzo na huduma mbalimbali za chuo.

Diploma Programmes: Ada ya diploma inaanzia Tsh 1,000,000 hadi Tsh 2,500,000 kwa mwaka kulingana na kozi. Ada hii hufunika ada ya mafunzo, vitabu, usajili, na huduma za maktaba.

Bachelor's Degree Programmes: Ada kwa shahada ya kwanza ni kati ya Tsh 2,000,000 hadi Tsh 4,500,000 kwa mwaka kulingana na mwelekeo na idara. Ada hii inajumuisha huduma za chuo kama vile usajili, mafunzo, maktaba, maabara, na ushauri wa kitaaluma.

Masters Programmes: Ada za masters ni kubwa zaidi kutokana na gharama za utafiti, na huanzia Tsh 3,500,000 hadi Tsh 7,000,000 au zaidi kulingana na kozi. Ada hizi hufunika masomo ya nadharia, utafiti, na huduma za kitaaluma.
 
Similar threads

Back
Top