Advertise here

Hii ndio mikoa 10 masikini zaidi Tanzania mwaka 2023

Kasomi

JT Founder
Picsart_25-09-23_20-31-29-192.jpg

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupitia ripoti ya National Accounts of Mainland Tanzania 2024, pato la wastani la mtu mmoja (GDP per capita) Tanzania Bara ni Tsh 3,058,847 kwa mwaka 2023.

Hata hivyo, mikoa kadhaa bado ipo chini ya kiwango hicho ikionesha changamoto za maendeleo ya kiuchumi, uwekezaji, na huduma za kijamii.

👇 Hii ndio mikoa 10 masikini zaidi Tanzania mwaka 2023:

1️⃣ Kagera — kiwango cha chini zaidi nchini
2️⃣ Simiyu — uchumi mdogo unaotegemea kilimo
3️⃣ Katavi — changamoto za miundombinu na uwekezaji
4️⃣ Rukwa — uzalishaji mdogo na usafirishaji mgumu
5️⃣ Singida — uchumi unaotegemea kilimo cha msimu
6️⃣ Tabora — uwekezaji mdogo wa viwanda na biashara
7️⃣ Dodoma — ongezeko kubwa la watu limepunguza wastani wa pato
8️⃣ Pwani — bado haijafikia wastani licha ya ukaribu na Dar es Salaam
9️⃣ Mara — shughuli ndogo za viwanda na huduma
🔟 Kigoma — uchumi mdogo wa biashara na uzalishaji

💬 Mikoa hii inatajwa kuwa chini ya wastani wa kitaifa kwa pato la mtu mmoja, ikionyesha tofauti kubwa ya maendeleo kati ya mikoa.

📉 Sababu kuu zinazotajwa ni:

▪︎Ukuaji mkubwa wa idadi ya watu
▪︎Uwekezaji mdogo wa viwanda
▪︎Changamoto za miundombinu
▪︎Kutosambaa kwa shughuli za kiuchumi

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) – National Accounts of Mainland Tanzania 2024
 
Hiyo mikoa aliyeifanya kuwa masikini ni serikali ya CCM, huko katavi ni wazalishaji wakubwa wa mahindi, lakini wamepakizana na ziwa rukwa, lakini mkoa haujafunguka kwa sababu ya miundo mbinu
 
Singida, Tabora na Dodoma hiyo mikoa inachangangamoto kubwa ya maji, ni jambo la kushangaza viongozi wanapeleka makao makuu ya nchi Dodoma sehemu ambayo mji ni shida kwa wananchi wangetatua hizo changamoto za maji hiyo mikoa ingekua
 
Hiyo mikoa aliyeifanya kuwa masikini ni serikali ya CCM, huko katavi ni wazalishaji wakubwa wa mahindi, lakini wamepakizana na ziwa rukwa, lakini mkoa haujafunguka kwa sababu ya miundo mbinu
Sahihi kabsa mfumo ndo shida
Pwani ni wavivu wanapenda umwinyi kuliko maendeleo, na utaona wachakarikaji ni watu kutoka mikoa mingine lakini wenyeji wameshikilia mambo yasiyo na tija
Watu wengine kutoka mikoa mingine ndio huchungulia fursa Katika mikoa ya pwani
Singida, Tabora na Dodoma hiyo mikoa inachangangamoto kubwa ya maji, ni jambo la kushangaza viongozi wanapeleka makao makuu ya nchi Dodoma sehemu ambayo mji ni shida kwa wananchi wangetatua hizo changamoto za maji hiyo mikoa ingekua
Nazani waliangalia eneo ambalo ni rahisi kufikika ukiwa Tanzania ndo maana wakaangalia eneo la katikati
 
Back
Top