Advertise here

Kumbukizi ya Miaka 5 ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli (1959 - 2021)

Kasomi

JT Founder
Kumbukizi ya Miaka 5 ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli (1959 - 2021)
2019-12-13-iss-today-magafuli-banner.jpg

Miaka mitano imepita tangu ulipotutoka, lakini alama ulizoacha bado zinang'ara. Uongozi wako wa uadilifu, uzalendo, na bidii vitadumu mioyoni mwetu. Ulisimama imara kwa maendeleo ya taifa, ukahamasisha uchapakazi kwa kauli yako maarufu ‘Hapa Kazi Tu!’

Leo tunakuenzi kwa upendo na heshima, tukikumbuka maono yako kwa Tanzania yenye uchumi imara na maendeleo kwa wote. Daima tutakuenzi na kuendelea kuthamini mchango wako.

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Katoma tarafa ya Bugando wilayani Geita jimbo la Geita vijijini.

Alifariki March 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam

Na alizikwa tarehe 26 Machi 2021 nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Pumzika kwa amani, Kiongozi wa Wanyonge.

Soma historia ya Magufuli hapa

Tazama video ya historia yake hapa
 
Back
Top