Mwanamume aliyepachikwa jina la utani la "mtu mchafu zaidi duniani" kwa kutooga kwa miongo kadhaa amefariki

Kasomi

JT Founder
Mwanamume mmoja wa Iran aliyepachikwa jina la utani la "mtu mchafu zaidi duniani" kwa kutooga kwa miongo kadhaa amefariki akiwa na umri wa miaka 94. Amou Haji, ambaye hakuoga kwa zaidi ya nusu karne alifariki siku ya Jumapili katika kijiji cha Dejgah katika jimbo la kusini la Fars. Inasemakana kuwa Haji aliepuka kuoga kwa hofu ya "kuugua". Lakini "kwa mara ya kwanza miezi michache iliyopita, wanakijiji walikuwa wamempeleka bafuni kuoga.

1667030604623.jpg
1667030596489.jpg
 
Back
Top