Kila mwaka ifikapo tarehe 15 october dunia inadhimisha siku ya kunawa mikono kwa sababuni kwa hakika hii ina maana kubwa sana kwa afya zetu.
Siku hii ni mahususi kwa ajili ya kuwahimiza wananchi juu ya umuhimu wa kunawa mikono yao kama sehemu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu ,kichocho ,kuhara na korona .
Je unajua ni nani alipendekeza kunawa mikono ili kuepuka magonjwa kuenea kwa kasi ?
Leo tutazungumza kuhusu mwanasayansi aliyegundua siri iliyopo katika kunawa mikono kuepuka magonjwa kuenea kwa kasi.
Ignaz Philipp Semmelweis alikuwa mwanasayansi na raia wa Hungary mwaka 1948 aligundua na kutoa wazo kuwa moja ya njia ya kuzuia magonjwa yasienee kwa kasi ni kunawa mikono.
Lakini wataalamu wengine walilipinga vikali wazo hilo na kutaka Semmelweis akapimwe afya ya akili yake kwani walidai wazo lake halikuwa na maana.
Semmelweis alizaliwa Julai 1 mwaka 1818 huko Budapest nchini Hungary anafahamika kama baba wa kunawa mikono na kudhibiti maambukizi, shujaa wa kunawa pia anafahamika kama The Savior of Mothers yaani mwokozi wa akina mama.
Semmelweis alipata shahada ya udaktari kutoka katika chuo cha Vienna kilichopo nchini Austria mwaka 1844.
Mwaka 1846 alijiunga na kliniki ya uzazi katika hospitali kuu ya Vienna yaani Vienna General Hospital akiwa amebobea katika magonjwa yote ya uzazi kwa wanawake na maendeleo ya mtoto pindi anapokuwa tumboni kwa mama yake.
Kwa wakati huo kulikuwa na wimbi kubwa la ugonjwa uliowakumba wanawake na watoto wachanga ugonjwa huo ulijulikana kama Childbed Fever yaani , Homa ya Kitanda na kwa jina jingine ulikuwa ukiitwa ugonjwa wa mtoto watalaamu walifanya kila njia kuhakikisha ugonjwa huo hauchukui maisha ya watoto wengi zaidi lakini juhudi zao hazikuzaa matunda .
Inasemekana kuwa Moja ya sababu zilizochangia ugonjwa huo kuwa tishio kwa wanawake na watoto ni baadhi ya wanawake kuwa na aibu pale wanapofanyiwa uchunguzi na madaktari wa kiume.
Inaelezwa kuwa Ugonjwa huo ulikuwa ukiambukizwa pindi mtoto anapokuwa anazaliwa.
Jambo hilo lilimuumiza kichwa sana Semmelweis hapo ndipo alipoamua kuchunguza ni nini chanzo cha vifo vya akina mama na watoto wachanga .
Alifanya uchunguzi wake katika wodi mbili moja zilizokuwa zinahudumiwa na wanaume pamoja na wanafunzi wa udaktari na pili alichunguza wodi zilizokuwa zinahudumiwa na wanawake .
Baada ya uchunguzi kukamilika aligundua kuwa wodi zilizohudumiwa na wanaume na wanafunzi vifo vilikuwa vingi inaelezwa kuwa ilikuwa mara tano zaidi ya zile wodi zilizokuwa zikihudumiwa na wanawake.
Mwanzoni walifikiri kuwa wanawake walipoteza maisha baada ya kujifungua kwa sababu kuna kasisi alikuwa akitembelea wodi za wanawake huku akiwa amebeba kengele yake baada ya mwanamke kupoteza maisha.
Wanawake wengine walipokuwa wakimwona kasisi huyo walikuwa wakiingiwa na hofu wakidhani kuwa na wao wamepata maambukizi hivyo waliugua na kupoteza maisha.
Ikumbukwe kuwa katika utafiti alioufanya Semmelweis alibaini kuwa katika wodi zilizohudumiwa na madaktari wa kiume vifo vilikuwa vingi kuliko wodi zilizohudumiwa na wakunga.
Pia alibaini kuwa kuna chembechembe za bacteria alizokuwa akiambukizwa mwanamke wakati wa kujifungua, na bacteria hao walikuwa wanapatikana kwenye mikono ya madaktari waliokuwa wakiwahudumia akina mama hao.
Hivyo Semmelweis aliamuru wafanya kazi wote kuanza kusafisha mikono yao na vifaa wanavyotumia kwa sabuni na dawa ya kuua viini vya magonjwa.
Baada ya wazo hili kufanyiwa kazi kwa ufasaha vifo vya akina mama na watoto vilipungua lakini madakatari wenzake hawakufurahia suala hilo.
Madaktari walikasirika kwa sababu dhana ya Semmelweis iliwafanya waonekana wao ndio wanaowaambukiza ugonjwa wa mtoto kwa wanawake.
Pia Wataalamu wengine hawakukubaliana na jambo hilo kwa sababu Semmelweis hakuwa na ushahidi wa kisayansi juu ya kile alichokuwa amependekeza kuhusu ugonjwa wa mtoto.
Suala hilo lilisababisha mgogoro kati ya Semmelweis na madaktari wengine ambao walikuwa wakiwahudumia wanawake waliokuwa wanajifungua ,hivyo ilipelekea uadui kati yao madaktari waliacha kunawa mikono pindi wanapojiaanda kumhudumia mgonjwa hivyo Semmelweis alipoteza kazi katika hospitali hiyo na kuamua kurejea nchini Hungary.
Akiwa nchini Hungary aliendelea kuwahamasisha madaktari sehemu mbalimbali kunawa mikono kwa kutumia dawa ya kuua viini vya magonjwa ili kuepuka maambukizi lakini kwa bahati mbaya hakuna aliyeweza kumuelewa kwa wakati huo.
Aliendelea na kuhamasisha watu kunawa mikono yao ili kuzuia magonjwa na aliweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Mwaka 1850 alianza kuandaa kitabu juu ya ugonjwa wa mtoto , kitabu hicho kiliitwa The Etiology, Concept, and Prophylaxis of Childbed Fever kilichochapishwa mwaka 1861.
Semmelweis alimuoa Maria Weidenhoffer kwa pamoja walifanikiwa kuwa na watoto watano.
Baada tu ya kuchapisha kitabu chake Semmelweis alianza kupata matatizo ya akili yaliyomfanya akae mbali na familia yake na kazi yake pia hivyo alipelekwa kwenye kituo cha watu wenye matatizo ya akili kilichopo Vienna nchini Austria.
Mwaka 1865 alipokuwa akijaribu kutoroka katika kituo hicho, alikamatwa na kupigwa vibaya na kupelekea kifo chake wiki mbili baadaye.
Uchunguzi uliofanywa juu ya kifo chake ulibaini ya kuwa Semmelweis alipoteza maisha kwa sababu ya jeraha kubwa alilokuwa nalo katika mkono wake lililosababishwa na kipigo alichokuwa amepewa.
Na huo ndio ulikuwa mwisho wa mwanasayansi Ignaz philipp Semmelweis aliyefanya mambo makubwa katika sekta ya afya ambayo mpaka sasa yanahimizwa dunia nzima ili kupunguza na kuepuka maambukizi ya magonjwa.
Ignaz Semmelweis aliokoa maisha ya watu wengi kwa maneno matatu tu Osha Mikono Yako yaani kwa kizungu tunasema Wash Your Hands.