Advertise here

SIMULIZI: MAMA MKWE MCHAWI

Simulizi

Member
SIMULIZI: MAMA MKWE MCHAWI
SEHEMU YA KWANZA (01)


"Hivi we mwanamke mie kila siku niwe naongea tu, naongea ili unifanye nionekane mbaya kwa majirani sindio?" Bwana Brison Aidan aliuliza kwa ukali punde baada ya kufunua Hotpot ya chakula alicholetewa na mke wake Bi Paulina, mkewe alistaajabu kwa swali lile aliloulizwa na mume wake hivyo alirudi nakusimama amsikilize tena.

"Mume wangu umesemaje?" Aliuliza Paulina kwa upole huku akimtizima mume wake aliekuwa amekasirika na kukunja sura yake wazi wazi.

"ET MUME WANGU UNASEMAJE?? NA WEWE UNAULIZA KABISA NASEMAJE?? HIKI NINI KWENYE HICHI CHAKULA?? HIZI SI MENDE HIZI! NA UNANIAMBIAGA ETI NAFUNIKAGA, WE UNANIPENDA KWELI UNITENGEE CHAKULA KINA MENDE HIVI?!" bwana Brison aliuliza kwa ukali huku akiibana pua kwa dharau, licha ya kuwa majirani zao walishazizoea kelele zile lakini siku hiyo zilipenya sana hata jirani yake mmoja aliposikia maneno yale alisongea akalitege sikio, ingawaje ilikuwa ni usiku wa saa mbili ambapo bwana Brison alikuwa amerudi kutoka kazini kwake.

"Lakini mume wangu mie siwezi kukutengea mende kwa lipi baya mume wangu ulilolifanya mpaka mimi nikulipe kwa baya kiasi hicho! nisamehe mume wangu sikujua kama waliingia mende kwenye hotpot ya chakula" Paulina alishuka chini na kupiga goti akimuomba mumewe amsamehe kosa lake kwani alihisi kuwa ni udhaifu wake ndio umepelekea vile.

"UNITOKEE HAPA KWANZA UMENINYIMA WATOTO HADI LEO HUZAI WEWE MWANAMKE GANI SASA! YANI NAJUTA HATA KUKUOA KABISA UMEKALIA KULIA TU INAFAIDA GANI KULIA? UKITAKA KULIA LIAA MWANA KULIA NA WE NGOJA TU!" Brison aliongea kwa hasira na. kuisukuma Hotpot ya chakuka kwa hasira kisha akanyanyuka mezani na kwenda zake chumbani.

Alimuacha mkewe bi Paulina akilia maskini kutokana na ugumba alionao kutopata mtoto tu ndio chanzo cha mume wake kumuona hafai, kwani ni miaika takribani mitatu toka wafunge pingu za maisha mbele ya kanisa kubwa kabisa liliohudhuriwa na waumini kibao siku hiyo, Toka wafunge ndoa hiyo hakufanikiwa kupata mtoto au hata mimba kuharibika licha ya kuwa mumewe alijitahidi kumtimizia hitaji la ndoa kila siku, alilia sana Hidaya huku akinyanyua mikono yake juu na kumuomba mola wake amjaalie apate japo mtoto hata mmoja ili ndoa yake iwe na furaha isiwe kama hivyo anavyotaabika, aliongea kwa huruma huku machozi yakiuchakaza uso wake wa urembo na kuiweka sura nyekundu kwa simanzi.

"Eeh! Mungu wangu niondolee balaa hili, kisa ugumba wangu mume wangu ananisimanga! hanipendi tena, eeh! Mungu nionee huruma na mie nifanye niitwe mama mungu wangu!! Nitaishi hivi hadi lini? najua Mungu unaniona na kunisikia nijibu Mungu wangu" Aliongea Paulina huku akilia sana alishusha maombi mazito Mungu amjaalie angalau abahatike hata kupata mtoto mmoja ili amfurahishe mume wake, Akiwa amebaki mwenyewe sebleni alisikia sauti ya mlango ukipigwa kwa nje huku ikifatia na sauti ikiita.

"Wa humu! Paulina! Paulina" taratibu alifuta machozi na kujikongoja kwenda ulipo mlango na kuufungua, na hapo alikutana na sura ya mzee aliekuwa pale mlangoni.

"Aah!! mjumbe!!" Paulina aliguna na kujibaraguza mjumbe asigundue kama alikuwa analia.

"Kuna usalama hapa?" mjumbe aliuliza huku akipitisha macho kwa ndani.

"Ndio mzee wangu tena wakutosha tu" Paulina alijikakamua na kuficha maumivu yake kisha akamjibu kama vile hakuwa analia mda mfupi uliopita.

"Nimesikia kelele kelele nikajua labda usalama utakuwa mdogo nikaona bora nije nichungulie jirani" Mjumbe aliongea huku safari hii akimtizama Paulina kuanzia juu mpaka chini.

"Usalama upo wa kutosha mzee wangu yani usiwe na wasiwasi" Paulina alijibu bado akiendelea kuweka siri kwa tukio liliotokea.

"Basi kama kuna usalama mie nirudi kwangu" Mjumbe aliongea kisha akamuaga Paulina nae mjumbe akaelekea kwake.

"Nfyuuu!! Baba zima ovyo umbea tu mambo ya watu we yanakuhusu nini kwenda huko" Paulina alifyonya kisha akaufunga mlango na kwenda moja kwa moja kwa mumewe, Brison alikuwa amejitupia kitandani na nguo zake zile zile alizovaa na kushinda nazo kazini, hakuwa na mda wa kufikiria kuvua viatu au kubadilisha nguo zile, Paulina alipomuona mumewe yuko katika hali ile hakupenda kabisa, na moyo wake ulimuua sana kwani hakupenda kumuona mumewe akiwa hana furaha.

"Mume wangu usiwe mnyonge kiasi hicho unanitia simanzi na mimi, mtoto ni rehma za Mungu tutampata tu isikupe..."

"NITOLEE KELELE ZAKO HAPA USHANICHOSHA, TUTAPATA TUTAPATA MBONA HATUPATI SASA, IMEKUWA KILA SIKU NYIMBO ILE ILE TUTAPATA USINIGUSE TENA!" Brison aliongea kwa ukali kisha akageukia pembeni na kumtegea mgongo Paulina, Paulina alitizama hali ile alichukulia ni sehemu katika maisha yake na mume wake ndio hivyo alivyoamua, alitingisha kichwa na kushuka kitandani kisha akabadilisha nguo zake na kurudi tena kitandani ili amvue zile nguo mumewe, lakini siku hiyo Brison alikuwa mkali kupitiliza hakutaka hata kuguswa na mkewe ingawaje ni mke halali wa ndoa.

"WE UPENDO WAKO NIKUNIBADILISHA NGUO? NIACHE UKINIGUSA TENA NITAKUPASUA" alisema Brison.

"Sawa mume wangu ni hayo tu basi ulale salama" Paulina aliongea na kuuvuta upande wa shuka na kumfunika mumewe lakini mumewe aliufunua na kukaa kitandani hakutaka kabisa kujumuika nae kwa siku hiyo.

"Unaenda wapi mume wangu?" Paulina alishtuka baada ya kumuona mume wake akibadilisha shati na kuvaa lingine kisha juu yake akavalia sweta.

"WE HAIKUHUSU!!" Brison alijibu na kutoka ndani, Paulina aliamka na kumuangaza mumewe hakumuona tena alilia sana maskini! alikaa nje kumsubiri mumewe arudi hadi saa saba kasoro akiwa chakula cha mbu nje lakini wapi Brison hakulala kabisa nyumbani hapo, Paulina alirudi ndani kwa unyonge na kuufunga mlango akajifunika shuka huku akiwa amekumbatia picha ya mumewe aliempenda kwa dhati Brison.

"Eeh! Mungu wangu uangazie mkono wako wa ulinzi kwa mume wangu arudi salama" licha ya kupitia misuko suko mingi kwenye ndoa yake lakini Paulina alizidi kumpenda mume wake hakuona sababu ya kumrudishia baya ingali anahaki kama mume, alimuombea dua mumewe kisha akajilaza, akiwa amekumbatia picha iliopigwa siku ya harusi yao.

Baada ya bwana Brison kutoka Nyumbani kwake alikodi boda boda hadi Mtaa wa Marimbe, moja kwa moja alifikishwa kweye nyumba ndogo alioitenga Brison na kwenye nyumba hiyo alimpa hifadhi mwanamke wa nje (Hawara) mwanamke huyo aliitwa Ziada, Ziada ni mwanamke tu waliefahamiana kwa mda mfupi tena bar ambako Ziada alikuwa akifanya kazi ya uhudumu, lakini si! uhudumu tu alikuwa anacheo pia kwenye bar hiyo baada ya mda alipewa cheo nakuwa 'Kaunta' kabla ya kuwekwa kimada na Brison, usiku huo Brison alifika kwa Ziada na kumgongea mlango nae Ziada hakuwa amelala hivyo aliamka na kufungulia kwa bashasha, "wow! mume wangu umerudi?" Ziada alimlaki hawara wake akimuonyesha mapenzi ya kweli, nae Brison alijiona kutulia kabisa akiwa na Ziada mwanamke wa nje kuliko hata Paulina mke halali kabisa.

"Aagh! lile limwanamke lishenzi kweli limenikera huko we acha tu" Brison alijibu huku wakivuta meza na kukaa pamoja kisha Ziada akaleta chakula na kukitenga pale Mezani.

"Yaani niliwaza sana kama utalala huko! nisingeweza kula kabisa" Ziada aliongea na kuchukua jagi la maji ya uvugu vugu na kumwagilia Brison anawe mikono ili wapate chakula, Brison alinawa na baada ya yote Hotpot ikafunguliwa na wakaanza kuumega ugari wa baridi na dagaa, Brison alivutika sana na ugari aliopata kwa Ziada kuliko chakula alichoandaliwa na mke wake Paulina, hakukumbuka kabisa kama ni mke wake wa ndoa, kule mwenzake alimuacha analia huku yeye anasherehekea na hawara aliemkwapua bar majuma matatu yaliyopita.
***********************
Walipomaliza kula walipanda kitandani kulala, huku stori za hapa na pale zikiwatawala wapenzi hao.

"Daah! hivi lini nitakuwa mke wako?" Ziada alianza kwa kuuliza huku akikichezea kifua cha Brison, Brison alikuwa kimya kwa mda kisha akamjibu.

"aahgh! hilo niachie mimi yani ni siku yeyote ile nataka kwanza nimtimue yule, mwanamke gani hajitambui" Brison aliongea na kumponda mke wake mbele ya hawara wake.

"Si umfukuze tu kama hajielewi" Ziada aliongea kumchochea hasira Brison, aliposikia kauli ile Brison aliona ni wazo zuri alilopewa na Ziada.

"Halafu kweli ngoja sikulijua mapema yule natimua halafu nakuoa wewe tunaishi kwa amani kabisa" Brison aliongea na kumpa matumaini Ziada ya kumuoa, walilala kwa kukumbatiana kimahaba mpaka asubuhi ya Jumamosi ilipofika, kama kawaida ya siku hiyo wafanyakazi wengi hupumzika katika siku hizo mbili, hivyo siku hiyo bwana Brison Aidan hakwenda kazini.
********************************
Aliamka asubuhi nakutoka nje huku ndani akimuacha Ziada bado akikumbatia shuka kwa ubaridi ule wa Asubuhi, alikaa kwenye msingi wa Nyumba hiyo huku akiwa ni mwingi wa mawazo, na kubwa zaidi lililomuumiza kichwa ni juu ya muafaka juu ya mke wake Paulina.

"Hazai! kweli kama hana mbegu mie wanini huyu? mie sio muislam kusema nioe mke wa pili, sasa ni hivi namtimua arudi kwao, acha nimuoe Ziada kwanza isitoshe Ziada ana mtoto mmoja hivyo nitapanda nae mbegu" aliwaza Brison kwa mda, alipokamilisha mipango yake alikung'uta vumbi na kurudi ndani, alimkuta Ziada akiwa ameshaamka na tayari alikuwa anamalizia kutandika kitanda, alisogea taratibu na kumkumbatia kwa nyuma huku mikono yake ikikutana kati kati tumboni.

"Aah!! mi naona niondoke niende huko nikamtimue huyo mwanamke" Brison alizungumza huku kichwa chake akiwa amekilaza juu ya mgongo wa mwanadada huyo.

"Kweli???" Ziada aligeuka haraka na kumuuliza kwa mshituko huku sura na moyo wake vikitandwa kwa furaha ya kusikia lile.

"Ndio natimulia mbali na wewe ndio utashika usukani wote" Brison aliongea na kumpa uhakika Ziada.

"Ndio maana nakupendaga mwaaaaah!!" Ziada aliongea kwa furaha na kumpiga busu Brison busu lilimchanganya zaidi na kumfanya awaze maamuzi mabaya tu mbele yake, alimkumbatia Ziada kwa nguvu kisha wakaachana, alitoka nje na kupanda boda boda tena iliomuokolea muda kufika kwake, alifika na kupitiliza ndani bila ya salamu ingali Mkewe alikuwepo nje akimfulia nguo zake.

"Mume wangu umerudi?" Paulina alipomuoana mume wake aliacha kufua na kumfata mume wake ndani alipoingia kwa fujo, lakini Brison alikuwa kama hamsikii ingawaje aliondoka usiku wa jana.

"Mume wangu! mume wangu! mbona uko hivyo lakini!" Paulina aliongea kwa sauti kumsimamisha mume wake lakini bwana Brison hakuwa hiari kusimama aliingia chumbani kwao na kuanza kuchagua nguo kwa kuzitenga zake na za Paulina.

"MUME WANGU UNAFANYAJE MBONA SIKUELEWI??" Paulina aliuliza baada ya kuona mumewe akivuruga amani ndani mle.

"WE NANI MUME WAKO? MI SINA MKE" Brison alijibu kwa ukali huku akiendelea kutoa vitu ovyo ovyo!

"Lakini Mume wangu!!!" kabla hajaongea kitu chochote Paulina, Brison alimzuia kwa kofi zito, kofi liliomplekea Paulina kukaa kimya kabisa.
"NIMESHAKWAMBIA UNYAMAZE!!" alimsukumizia neno huku akimtizama kwa jicho kali, Paulina alishika shavu na kuendelea kulia maskini! Nguo zote za Paulina zilizokuwa kwenye begi Brison alizitoa zote na kumfungia kwenye vitenge vyake mafurushi matatu kisha akatoka nje na. kumtupia.

"NGUO ZAKO ZISHATANGULIA NJE NA WEWE UTOKE HAPA!" Brison alirudi ndani na kuongea huku akimsukuma Paulina mgongoni atoke nje.

"KOSA LANGU NINI??" Paulina aliuliza

"SITAKI KELELE TOKA HAPA" Brison aliongea kwa ukali.

ITAENDELEA.....

We unafikiri Bwana Brison ameamua haki kumfukuza Paulina kisa Ziada??
 
SIMULIZI___ MAMA MKWE MCHAWI
SEHEMU YA KWANZA (02)

ILIPOISHIA..........

"NGUO ZAKO ZISHATANGULIA NJE NA WEWE UTOKE HAPA!" Brison alirudi ndani na kuongea huku akimsukuma Paulina mgongoni atoke nje.

"KOSA LANGU NINI??" Paulina aliuliza

"SITAKI KELELE TOKA HAPA" Brison aliongea kwa ukali.

ENDELEA NAYO.........

"Kwa hiyo mume wangu, haya ndio malipo ya wema wangu wote niliokutendea?" Paulina aliuliza kwa masikitiko huku macho yake yasiweze kuvumilia maumivu yale yaliyo ndani ya moyo wake, aliangusha chozi mfululizo binti huyo aliezeeshwa ingali ni binti mdogo tu wa miaka ishirini na Nne (24)

"WEMA GANI? NAKUULIZA WEMA GANI? WEWE ULIOUFANYA MPAKA USEME WEMA? NIMESEMA HIVI SIKUTAKI UENDE KWENU TENA UNACHELEWA ONDOKA HAPA" Brison aliongea huku akimsukuma sukuma Paulina atoke nje.

"Mume wangu ninaekupenda! ninaekuthamini! ninaekuheshimu unanifukuza kama mbwa?! nimekukosea nini mume wangu hadi unifanyie unyama huu! kisa kuwa mgumba mume wangu? nimiaka mingapi tumeishi pamoja mume wangu? wangapi kwenye ndoa zao wanadumu hata miaka kumi hawapati watoto? hufati hata vitabu vya Mungu vinavyozungumza mume wangu??" Paulina alijitahidi kuiamsha akili ya mumewe lakini wapi!,

Brison alikuwa kama katia chuma kwenye tundu za sikio zake asisikie kile anachokizungumza Mkewe, na aliziba kabisa kwa mikono kwani aliona nikelele tu anazoendelea kuzisikia

"NIMESEMA SITAKI STORI TOKAAAAA" aliongea tena kwa msisitizo.

"Sawa mume wangu natoka, lakini ujue wazi Paulina anakupenda sana"

"KAWAPENDE WENGINE HUKO, MI NIKAE NA MWANAMKE AMBAE HAZAI NAFAIDA GANI? KWANI NIMEOA MWANAUME MWENZANGU, SIBORA UENDE, KWENDA KABISA HUKO" Brison alimsukumizia maneno mazito Paulina.

Maskini Paulina furaha yake iligeuka kilio, na aliemfanya alie ni mtu aliemthamini aliemuamini hata kukubali kufunga nae ndoa kisa ugumba Brison aliamua amtimue kabisa, Paulina alitikisa kichwa mara nyingi akijutia kuwa na tatizo lile hasa alivuta taswira ni wataalam wangapi walishindwa kulitatua tatizo hilo, aliona sasa tatizo lake amkabidhi Mungu tu ndie asieshindwa na jambo, kwa unyonge sana aliendea nguo zake nje ziliporushwa na Brison na kuzikusanya pamoja akageuka nyuma kuungalia mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hio akatikisa tena kichwa, na hapo Brison alikuwa amesimama mlangoni akishuhudia mkewe anavyoondoka kwa masikitiko lakini baada ya hatua kadhaa Paulina alirudi nyuma na kuviachia virago vyake nakurudi hadi pale aliposimama Brison, aliivua pete kwa uchungu huku akiiongea.

"Pete hii ulinivisha siku ile ya harusi mbele za watu tena ukitabasamu, leo imekuwa chachu kidoleni mwangu, pete hii inanifanya niaibike mbele za watu, Alhamdulilah mume wangu, nilibadilisha dini yangu kisa wewe niliekupenda ukanifanya baadhi ya ndugu zangu kunitenga kisa wewe, leo mbele za watu unanitimua tena kwa aibu, Mungu ananiona na hili atalilipa siku moja, Naivua pete hii mbele za watu wakishuhudia na kukabidhi pete yako utafute yule ataekufaa Brison"

Paulina aliongea kwa uchungu machozi yakimdondokea kifuani mwake, hakuona sababu ya kuyafuta machozi yale, alilia hadi mengine kugandiana nakuacha alama usoni mwake, macho yalimvimba Paulina hakuamini kwa mara nyingine tena kama ndio mume wake anamfukuza, Majirani walioliona tukio lile wengine walisikitishwa sana na unyama alioufanya kijana huyo, kwani Paulina alikuwa ni binti mpole alieshiba maadali ya Dini na aliishi vyema na majirani zake hao.

"Leo maskini anaondoka? wanaume hawa mbona makatili hivi? hivi kweli Paulina ndio wakufukuzwa hivi?" Mmoja katika wale walioshuhudia tukio lile aliuliza kwa uchungu huku akimtizama Paulina akiburuza mizigo yake.

"Kila siku tulikuwa tunasikia makelele leo katimuliwa acha aende, kwanza kana maringo kweli" Dada mmoja aliongea upuuzi mbele ya watu waliompenda Paulina nusu wamtoe pua kwa kumshambulia vikali.
_____________________

Baada ya Bwana Brison Aidan kuhakikisha Paulina amepotelea alirudi ndani huku akiacha lile jopo la watu waliokusanyika likitawanyika.

"Deal Done! nimeifukuzia mbali taka taka ile" Brison aliongea kwa shangwe huku akijitupia kitandani na mda huo simu ikiwa sikioni mwake akiwasiliana na Ziada,

"Waoooooh!!! unasema kweli??"

Upande wa pili ziada alipokea pia kwa shangwe aliitika kwa furaha kumdhirishia Brison kuwa amefanya jambo la maana kumtimua Paulina.

"Sasa mi na muda wakupoteza? nakujia sasa hivi bwana uje tuishi kwenye jumba kubwa hili" Brison aliongea kwa shangwe ya ajabu.

Hidaya alikuwa ni mwanamke wa kipekee sana, na aliitumia vizuri akili yake zile fedha alizoachia kwa ajili ya matumizi alizikata mafungu kidogo, na baadhi alizihifadhi kwa ajili ya maendeleo yake, kujipamba kununua nguo na kadhalika, hivyo siku hiyo haikumpa tabu kutoa fungu katika fungu alilojiandalia kupata hela ya nauli ya kumrudisha kwao.
_______________________

Njia nzima alibubujikwa na machozi, watu walimtizama vile alivyomzuri hawakupata picha kwanini analia vile! maskini Paulina mpaka anashuka basi na kushika njia kuelekea kwao ni majira ya saa mbili usiku, nyumbani hali si shwari sana, mama yake pia ni mkubwa ingali si sana umri ni kati ya miaka hamsini hadi stini, aliutizama mlango wa Nyumba yao vile ulivyokuwa umechoka, alisimama nakulia tu nje Paulina kwani aliamini kupitia ndoa yake angeweza kumsaidia Mama yake pamoja na wadogo zake wawili wanaosoma kwa tabu, Sauti ya kilio chake ilipenya ndani, Mama yake alisikia kilio chake alitoka nje na Mdogo wake mmoja wakiwa na chemli (taa ya kandili) na kumkuta Paulina akiwa nje amekaa chini akilia tu.

"HIDAYA MWANANGU!! HIDAYA!" Mama yake alimuita lakini Hidaya (Paulina) alishindwa kuitika kutokana na uchungu aliokuwa nao. (Hidaya ndio jina lake halisi kabla ya kulibadilsha)

"KIMEKUPATA NINI HIDAYA MWANANGU?" Mama yake bado alizidi kumuuliza huku akimnyanyua na kumkumbatia.

"MAMA NAKUPENDA MAMA YANGU"

"Najua mwanangu usilie mizigo yako tayari imeshanipa jibu la kutosha, sikuulizi swali mwanangu, hebu ingia ndani na uache kulia" Mama alizidi kumuonyesha upendo mwanawe, nae alimkumbatia kwa nguvu mama yake kisha akajikakamua nakuamka.

"Amekufukuza??" Mama aliuliza

"Ndio Mama" Hidaya alijibu.

"Yani Anakufukuza!!" Alirudia tena swali Mama yule.

Kauli ile ya mama ilimtia nguvu hidaya na aliamini mama huenda atapanga kwenda kwa mume wake kumuombea msamaha.

********

"Hapa ndio kwangu sasa nilipokwambia utaishi mwenyewe kwa kujinafasi" nilizungumza kwa furaha, kwani niliona yuke alienibana sasa amenipa nafasi ya kujiachia kwa kumpa adhabu kali ya kumtimua.

"Aaaagh!!! pazuri kweli!! nimepapenda bure" Ziada aliongea kwa furaha huku akifungua fundo lake kifuani la kitenge na kumshusha mtoto wake mdogo wa miaka mitano, nilikatizama katoto kale kaliposhushwa kisha nikakaita lakini kaligoma hadi mama yake akafoka hakuipenda picha ile alioionyesha mtoto yule.

"WE SIUNDE KWA BABA YAKO UNAITWA" Ziada aliongea kumuamuru mtoto yule lakini wapi alikuwa ni kama anatwanga maji kwenye kinu, mtoto aligoma! aligoma kabisa tena nilivyozidi kumsogelela ili nimbebe ndio alizidi kujificha nyuma ya miguu ya mama yake kunikwepa nisimshike.

"Aagh!! hakataki" nilisema na kulipotezea jambo lile lakini mama yake alichutama kidogo kisha akaongea nae kikabila na hapo yule mtoto alianza kunisogelea, nilishtuka sana kuona tukio lile lakini sikuwa na mda wakulijadili kiundani nilipuuzia badala yake nikacheka kisha nikauliza.

"eeh! hakajui kswahili?"

"KANAJUA MBONA SEMA NIKISARANI TU MTOTO NAKIBURI HUYU" Ziada alidakia njiani hata kabla sijamalizia kauli yangu.

"haya nisalimie!" nilikaambia baada yakuwa kamekubali kukabeba mikononi mwangu, na nilipokabeba kalitulia tuli utafikiri sio yule akiokuwa ananiogopa mwanzo.

"We Nyangindu siusalimie yani hili litoto" ziada aliongea kwa hasira huku akimtizama mwane kwa jicho baya ajabu! ilinishtua lakini bado nilihisi huenda kwa vile ni mtoto bado hajaniozea nilikaangalia kisha nikaanza kukiambia kanisalimie.

"Nisalimie baba eti" Nikidanganya ili katoe salama lakini ndio kama vile nilifungulia koki ya kuitoa sauti yake nje, alifungua mwano mkubwa wa kilio kisha akaanza kutupa tupa miguu yake ishara nimshushe chini, nilijitahidi nimbembeleze lakini nguvu ya sauti ya mtoto yule iliyashinda masikio nguvu na nilimshusha haraka kisha nae kwa haraka vile vile akakimbia kwa mama yake na alipofika tu alifumba domo lake na hakuendelea kulia tena.

"Eeeh!! huyu mtoto...!!" kabla sijaendelea kusema lolote Ziada aliingilia kati na kunizuia kwa kupitisha maneno mengine tofauti.

"Yani hili litoto ndio maana huwa naliacha kwa shangazi yake eeh!!" alisema huku akimbeba na kumtweka nusu ya kiuno chake ambapo dogo alitulia na kuizungusha miguu yake kama mkanda kiunoni.

"Aaah!! achana nae ni mtoto huyu" niliongea huku nikikatizama katoto kale kalikoanza kunitia mashaka na moyo ukaanza kuwa juu juu kwa mda mfupi tu tokea wafike nyumbani pale.

"Okey! usiku umeshaenda sana! twende tukapumzike" niliongea kisha nikalisogelea sanduku lake moja la mbao ambalo alikuja nalo, ili nimsaidie kuliingiza chumbani.

"AAAH!! AAH!! ACHA NITALIBEBA MWENYEWE" aliongea kwa kuniwahi pindi alipoona mkono ukilikaribia sanduku lile, alinizia kabisa na kuusukuma mkono haraka.

"Okey!! sawa utaliweka chumbani sasa" nilimjibu kisha nikabeba baadhi ya mabegi ya nguo zake aliyokuja nayo, Tuliingia ndani kisha nikamuonyesha sehemu ya kupaki mabegi yake na sehemu ambayo katika ramani niliombwa kiwekwe chumba kwa ajili ya kulala mwanangu kama atazaliwa lakini ndio ikawa vile! hatukufanikiwa kabisa kumpata mtoto nikiwa na Mke wangu Paulina nikamuambia Ziada amuweke mwanawe.

"Halafu karibu! yani mlango na mlango hata akilia namsikia" alisema Ziada baada tu ya kukikagua chumba atachokuwa analala Nyangindu mwanae, haikuwa mbali kutoka chumba chetu na kile atapolala mtoto huyo, vilikuwa vinatazamana yani chumba kwa mlango wa chumba ndani ya chumba tutachokuwa tunalala.

Baada ya yote na kuhakikisha Nyangindu amelala tuliiacha taa ikiwaka huku tukihakikisha tunamkinga na mbu kwa kumuwekea chandarua ili mbu wasifanikiwe kuijua ladha ya damu yake, tulitoka na kurudi chumbani kwetu kwa furaha huku tukionyeshana utani wa hapa na pale ikiwa ni sehemu moja ya mapenzi kama vile ndio tunaanza kupendana, tulipanda kitandani kwa furaha macho yakatazamana kwa huba upepo uliotoka puani ndio ulitafsiri kilichopo mbele yetu shuka na mito iliopamba kitanda ilibidi tuisogeze pembeni taratibu na hapo midomo ilijiramba kwa mda ilikutana katikati kisha kilichofata nikitendo cha kubadilishana ladha ya mate huku tukipeana lita kadhaa.

Lakini wakati nikiwa najiandaa kuanza kufanya tendo ghafla nilishtuka vitu vizito vikitoka ndani uume kupitia tundu lile dogo la sindano nikishtuka na nilistaajabu kuona tukio lile kwani tokea nianze kufanya mapenzi haijawahi kunikuta hali ile bado sijapata muafaka kwanini hali ile imenikuta hapo hapo uume ulianza kupunguza makali na baadae ukalala kabisaa.

"Mbona huingizi??" Ziada aliuliza baada ya kusubiri huduma lakini akaikosa na tayari mwili wake ulikuwa umepamba moto akisubiri huduma tu.

"TAYARI" nilijikuta nikiropoka huku nikijitahidi kuitikisa ili iamke.

"TAYARI NINI??" Ziada aliuliza kwa hofu.

ITAENDELEAA.....

Kumekuchaaaaa! Brison kimemkuta nini tena? Tukutane kesho.
 
SIMULIZI___ MAMA MKWE MCHAWI
SEHEMU YA TATU (03)

ILIPOISHIA........

"TAYARI" nilijikuta nikiropoka huku nikijitahidi kuitikisa ili iamke.

"TAYARI NINI??" Ziada aliuliza kwa hofu.

ENDELEA NAYO.......

"TAYARI NINI WE NAE??" Ziada aliuliza kwa hofu huku akiunyanyua mwili wake ili aone na ajue kwanini nimesema tayari ingali sijafanya lolote.

"Hee umeshamwaga??" Aliuliza kwa mshituko baada ya kuona vitu vizito na tayari uume ukiwa umelala kabisa tena tofauti na hapo mwanzo.

"Ndio nini Brai?" aliuliza tena huku akinyoosha mkono na kuanza kuufikicha kama utasimama lakini jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa hali ilibaki vile vile,

"Mi..!! ssii..!! mi..mi si..!! jui kabisa haijawahi kunitokea hali ya namna hii!!" niliongea kwa hofu na mashaka huku mapigo ya moyo yakienda mrama sikuamini kabisa kile kilichonitokea siku hiyo, aibuu!! aibuu ilioje mbele ya Ziada kushindwa kufanya nae mapenzi.

"Imeanza lini hii! mbona tulikuwa tunafanya mapenzi vizuri siku za nyuma??" Swali la Ziada ndio lilizidi kunichochea mawazo na kunitumbukiza katika dimbwi hilo zito la mawazo, ulibaki mwili tu juu lakini akili haikuwa pale, niliwaza huenda ni Paulina ndio ameamua kunifanyia vile lakini nilitikisa kichwa baada ya kugundua Paulina asingeweza kunitendea vile.

"WE BRAI" Sauti ya ziada aliyoniita na kunitikisa ndio iliniokoa na kunitoa dimbwini humo kisha nikamtizama kwa unyonge.

"LIMALAYA LAKO HILO NDIO LIMEFANYA HAYA" Ziada aliongea yani kama vile alikuwa ubongoni mwangu mda mfupi uliopita na kauli yake iliniingia zaidi akilini mwangu sasa ndio nikapata uhakika nikahisi kabisa ni kweli huenda Paulina ndio ameamua kulipa ubaya ule.

"NI KWELI PAULINA! PAULINAAAAAAA!!!" Niliita kwa nguvu ya kulaani jina Paulina kwani niliamini ndio msababishi mkuu wa tatizo hilo, lakini Ziada alinishika mkono na. kunipa maneno ya matumaini huku akinipa maelezo kesho ikifika niamke nakwenda hadi kwao Paulina nikamchimbe mabiti nami nilikubaliana na ushauri wake kisha pumzi na mapigo vikarudi sawa kufuatia kupozwa kwa maneno mengi ya busara kutoka kwa Ziada, Nilila macho siku hiyo, jicho moja likiwaza kesho na jicho lingine likiwaza mwisho wa usiku huo niliouona mrefu na mchungu kupindukia.

Nilipitiwa na usingizi ingali sikujua ni mda gani lakini kwa makisio ilikiwa hata saba usiku nilipopitiwa na usingizi, nilikuja kushtuka baadae baada ya kusikia kishindo kizito kilichotua nje ya nyumba, na nilipoamka nilikisikia tena kishindo kile moyo ulianza kuingia na waswasi.

"Ziadaa! Ziada! We ziada!!" nilianza kuita taratibu na baadae nikaongeza sauti huku nikiutingisha mwili wa Ziada lakini hakuamka nilihisi huenda ikawa ni uchovu hivyo nilimuacha na nikasimama taratibu na kujisitiri kwa kuvaa pensi kisha nikasogea taratibu iliposwitch ya taa na kuibonyeza, na mwanga ukasambaa kwa kasi ndani na. kukiangazia chumba kizima, jicho lilibadilisha muelekeo na kuelea dirishani ambako usawa huo ndio nilisikia vishindo vile vizito vilivyonifanya kuzinduka.

Taratibu kwa tahadhari nilitembea kwa kuvizia huku jicho likipenya upande wa nje kuchungulia kama kuna kitu chochote kilichoanguka, mara puuuuuff!!! moyo uliripuka miguu ikaanza kutetemeka kwa uoga kwa kile nilichokiona nje kikiendelea, kulikuwa na kundi kubwa la watu waliovalia sare za rangi mbili nyeusi na nyekundu wakizunguka nje ya nyumba, nilihisi ni ndoto inayonitokea pale, haraka nilifikicha macho niangalie tena lakini nilipotupia macho lile kundi sikuliona tena zaidi vilibaki kusikika vicheko vingi vya kike.

"Wale si wachawi??" nilijiuliza na tayari ngozi ya uso wangu iliruhusu kukiachia kimiminika cha uoga, nikirudi haraka nimuashe Ziada lakini hata nilipofika na kumtingisha Ziada hakumka! ilizidi kunitia hofu kubwa na kuzidi kuuchukia usiku ule, Nilitamani hata nitoke nje nikimbie lakini ningeanzia wapi kuikimbia nyumba niliojenga kwa mikono yangu? lilinijia swali hilo na kabla sijawaza kujijibu swali langu mlango wa chumba alicholala Nyangindu ulianza kufunguka na kujifunga wenyewe pasina kuwepo mtu wa kufanya lile.

"Nyangii??" niliita huku nikiutizama mlango ule, "Kuna mtu hapo??" niliita na kuanza kukanyaga hatua nikimuacha ziada aendelee kulala nami nikienda kuchungulia kwenye chumba hicho alicholala Nyangi lakini kabla sijaufikia mlango huo nilishtuka nikiguswa begani kwa kitu chenye uashiria ya kiganja kigumu.

"AAAAAH!!!" nilipiga kelele na tayari nilikuwa nimejirusha pembeni kwa uoga na kuanza kutembelea makalio kwa kujivuta kufatia kile nilichokiona sio kitu cha kawaida, niliona Ziada akiwa nilimzimu la kutisha tena lilovaa nguo zilizosarambuka na kuraruka vikali isijulikane rangi ya gauni ile mdomo wake ulikuwa umechakaa hata meno yasijulikane ni mangapi na mpangilio wake upi, Alitishaa!! alitishaa kabisa kumtizama, nikirudi kinyume nyume hadi nilipofika kikomo kwa kukutana na ukuta na hapo ndio ikawa kikomo cha mbio za sakafuni, Lilinyoosha mkono wake kuikaba shingo yangu.

"Hapana!! hapanaaa!!" niliongea kwa sauti kubwa.

"HAPANA NINI BRAI??" ghafla nilishtuka na kuangaza huku na kule hakuwa mzimu wala shetani alikuwa ni Ziada wa kawaida kabisa.

"Makelele ya nini Brai usiku wote huu?" aliuliza Ziada.

"Ndoto Ziada nimeota ndoto mbaya sana" niliongea kwa uoga, yote ni baada yakugundua bado nipo juu ya kitanda na nilikuwa sijashuka na kwenda sehemu yeyote ile.

"Aah!! we nae sindoto za kawaida hizo kuota au ndio mara ya kwanza unaota?" aliuliza Ziada huku akinivuta tuendelee kulala.

Nilirudi kulala lakini picha mbaya ilianza kujijenga juu ya ujio wa Ziada ndani ya nyumba yangu kwani ni masaa tu tokea atie kiguu ndani mle lakini kama miezi mingi na nyumba imekosa utulivu kabisa.

Licha yakuwa nililala macho lakini asubuhi ilipofika sikuwa na amani kabisa, licha ya kuwa Ziada alinitoa wasiwasi kwa kuniambia ile ni ndoto, nilikaa nje nikiwa na mswaki mdomoni nisiweze kusugua meno kwa ajili ya kujiandaa kwenda Nyumbani kwa kina Paulina, mswaki ulibaki kinywani hadi ukaanguka bila kujitambua na mda huo Ziada nae alikuwa akitoka nje aliniona vile nilivyoteswa na mawazo hivyo alisogea taratibu kisha akachutama na kuukota mswaki ule na kuusafisha kisha akanikabidhi huku akinitizama kwa unyonge.

"Hivi bado unamaswali juu ya ndoto ulioiota??" aliuliza Ziada huku akinitizama usoni vile nilivyokuwa na uoga juu yake.

"Yaa.. ni we acha tu!! si.. si.. sjui ni nini tu" Nilimjibu kwa kitete huku meno yakiumana kwa hofu.

"PAULINA! PAULINA NAKWAMBIA NDIO ANATAKA KUKUANGAMIZA KAMA UTACHELEWA ATAKUUWA MUME WANGU" Ziada aliongea na kunichochea hasira sikuwa na muda wakupoteza tena kila neno lililotoka kinywani mwa binti yule nililiamini sana sijui kwanini, nilinyanyuka haraka kisha nikarudi ndani bila kuoga nikafakamia begi la nguo nakuchagua suruali haraka haraka nikaivaa na kuufunga mkanda haraka niliusukuma mlango na kutoka nje njia ni moja tu nikwenda nyumbani kwa Paulina.

"Mchawi huyu sa ngoja nikukute huko!" niliongea kwa jabza na kutoka nje bila kumpa taarifa Ziada, akili ilikuwa ikiongozwa na hasira tu.

"Kwa hiyo ndio unaenda?" Ziada aliuliza huku akiwa amesimama mlangoni na purukushani zote aliziona toka nimetoka nje hata nilipoingia ndani nakuvaa nguo haraka.

"KAMA UNAVYONIONA" nilimjibu haraka kisha nikapachika ufunguo kwenye gari langu dogo aina ya RAVA4 haraka niliiwasha kisha mwendo wa haraka nilikanyaga mafuta, barabara ilikuwa kama yangu siku hiyo sikuzingatia matumzi yeyote ya sheria za barabarani, tena bahati nzuri barabara ile haikuwa kubwa kivile hata trafic hawakuzengea zengea maeneo yale.

Spidi niliotembea nayo siku hiyo halmanusura nimgonge mwanafunzi mmoja na mzazi mmoja aliekuwa akimvusha ili ampeleke ng'ambo ya barabara Mtoto yule, bila kufunga breki ya ghafla ilioburuza tairi ningemgonga maskini na ndio ingekuwa mwisho wa safari yake baada ya kunusurika na ajali hiyo haikunipa shaka au kunizuia nisiendelee na safari yangu, ndio kwanza nilikanyaga spidi ile ile tena niliongeza mara dufu zaidi hata ya ile ya mwanzo kwa masaa kadhaa nikafika mtaa wa kwao Paulina yapata saa sita mchana, nilipofika karibu na nyumba yao nililiegesha gari pembeni nikahakikisha nimetia lock kisha kwa hasira nikashuka nikukanyaga hatua kuelekea nyumbani hapo ambapo kwa nje hakukuonekana dalili za kuwepo na mkazi kutokana na mzingira yalivyokuwa hovyo!

Hata uwanja ulikuwa haujafagiliwa, nilipogeuza shingo niliona kijumba cha tope kidogo kwa ndani kikiwa kimetapaa alama za moshi kwa haraka niliona baadhi ya vyombo nikajua ile ni sehemu ya jiko na nilipoona kuni zikiishilia nilijua wazi wametoka kupika mda si mrefu.

"WE PAULINA! PAULINA!! PAULINAAAA!!" niliita nikiwa nimeukaribia mlango ule wa kuingilia ndani lakini kabla sijatia mguu mmoja alitoka mama yake nje nakusimama mlangoni.

"We!! we! we!!! acha wehu hii sio sehemu ya kufuga wehu" Mama alitoka nje na kunizuilia mlangoni alitanda kabisa nisiingie ndani.

"Mama samahani sikukusalimia! Shikamoo mama"

"Eti shikamoo mama!! ipi shida yako?" mama badala ya kuitika salamu alinikata kwa kauli haikutika kabisa badala yake aliniuliza swali.

"Nashida na Paulina Mama" niliongea kwa upole ili mama yule aniruhusu niingie ndani nimpashe ukweli Paulina na nilipochungulia nilimuona Paulina akiwa amekaa kwenye kigoda na aliniona lakini alinitizama kama hanijui kisha akanyanyuka taratibu na kuja upande ule, alipofika alisimama nyuma ya mama yake na macho yake yalitosha kunijulisha amelia kwa kiasi kikubwa kwani macho yalionyesha kuvimba.

"KIMEKULETA NINI HAPA?? KWANZA MIE NI HIDAYA NA SIO PAULINA" aliuliza huku akinitizama kwa jicho kali.

"MCHAWI WEWE! KISA NIMEKUACHA NDIO UNIROGE??" niliongea kwa kujiamini lakini wao walibaki kimya wakinisikiliza kwa makini, na hakuna mtu aliefungua mdomo kujibu zaidi walinitizama tu na kuniacha nitambe kwa kupiga kelele mwenyewe, nami ndio niliona fursa ya kuwapa makavu laivu! tena niliipaza sauti haswaaa nikijiona mimi ndio bingwa niliifungua sauti nani ambae hakusikia?

"WACHAWI WAKUBWA NYIE MNANIROGA MIMI WEWE MAMA MKWE GANI MCHAWI YANI HAPA KWANGU MMEKWAMA MIMI NDIO BRISON!! BRISON MTI MKAVU" niliongea kwa kujiamini huku nikijipiga kifua kwa kujigamba wao hawakujibu lolote lile walinitizama vile nilivyopiga makelele na kuwakusanya wanakijiji kwa mda mfupi.

Nikiwa bado naendelea kutia makelele nilishuhudia wadogo zake Paulina wakitoka nje Miiko sikujua ile miko wametoka nayo ya kazi gani, niliacha kupiga kelele na kuwatizama watoto wale hadi waliponifikia, waliponifikia tu walianza kunipiga kwa nguvu kwa miko ile, ilikuwa kama wametoa ishara kwa wanakijiji walianza kuja kwa kasi na wengi kama nyuki na kunishambulia vikali wengine wakiwa na mifagio ya njukuti wengine na masufuria na sijui waliyatoa wapi kwa mda mfupi vile, niliambulia kipigo kizito nilikimbia hata gari niliikuta ikiwa imepasuliwa vioo kabisa, nikiwa na manundu kila kona niliwasha vile vile na kugeuza njia, nilijuta hata kilichonipeleka pale.

"AAH!! USHENZI HUU WACHAWI HAWA WANATETEWA HIVI??" niliongea na kuigeuza gari haraka nirudi nilipotoka bila kupenda.

"Mpumbavu huyo kama alikutesa ni huko kwao huku ni kwetu tena umefanya la maana kumnayamizia" Mama Hidaya aliongea kumsifu utulivu aliouonyesha Hidaya licha ya kusikia maneno yale machafu ya Brison.

"Litahangaika sana kama halijielewi ipo siku atakuja kukuomba msamaha mwanangu yani wanaume wengine sijui wakoje! yani msichana kigori mnyenyekevu kama wewe, mstarabu uliemvumilia tabia ya ulevi bado anakutimua na katu hatopata wanawake wa aina yako kwa ulimwengu huu wa leo nakuapia" Mama aliongea kauli nzito iliompa matumaini mapya Hidaya na. kuanza kumsahau taratibu adui wa moyo wake katili Brison,
*****************************

Nilirudi kwa mwendo wa taratibu sana tofauti na vile nilivyoenda huku mwili ukitawaliwa na maumivu kila kona kufuatia kipigo kikali nilichokipokea kwa wananchi wale wenye hasira kali.

"Lakini huenda nikawa mkosefu haiwezekani bwana wanipige vile wale wananchi! huenda hapa kuna jambo nalikosea sana" moyo mwingine ulianza kuniingia na nilipoijenga ile taswira na kile kipondo ndio kilianza kunipa majibu taratibu, nilipotezea na kurudi home usiku totoro!! ikiwa ni saa tatu kasoro hivi, nilipiga honi ili Ziada atoke kunipokea lakini sikuona majibu yeyote nilishuka na kuifunga gari kisha nikapanda ngazi kuelekea ndani Hatua kadhaa ulipo mlango wa chumba changu nilishtuka kuona viatu vya mwanamume vikiwa vimeegeshwa ukutani na mlango ulikuwa umefungwa.

"WE ZIADA??" niliita kwa hasira huku nikivinyanyua viatu vile nakuanza kuupiga mlango wa chumba changu uliokuwa umefungwa na ndani ilifunguliwa sauti kubwa ya mziki.

ITAENDELEA......

Malipo ni hapa hapa we unafikiri nini kitachojiri iwapo itagundulika kuna mtu ndani ya chumba chake?
 
Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

dawnacuna314@gmail.com
 
Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

dawnacuna314@gmail.com
Stori nzuri na ingependeza ungeiandikia uzi wake kabsa
 
Back
Top