Kasomi
JT Founder
Anaitwa Luciano Re Cecconi, Huyu Alikuwa ni Mchezaji Maarufu wa Timu ya Taifa ya Italia na Klabu ya Lazio. Hii Ndio Simulizi Yake ya Kuhuzunisha Ambapo Mwaka 1977 Akiwa na Miaka 28 Alifariki kwa Kuuwawa Kisa Kikiwa ni 'Utani'. Huu Ulikuwa ni Msiba wa Kuhuzunisha Zaidi Katika Soka la Italia kwa Wakati Huo.
Ilikuwa ni January 18, 1977 ambapo Cecconi kiungo wa klabu ya soka ya Lazio na timu ya taifa ya Italia alitoka kwaajili matembezi na rafiki yake Pietro Ghedin (pia mchezaji wa Lazio), ambaye alitaka waingie kwamza katika duka la vito vya thamani linalomilikiwa na rafiki yake Bruno Tabochini wamsalimie.
Kabla marafiki hao wawili hawajaingia kwenye duka hilo walikubaliana kwamba wamfanyie rafiki yao huyo utani kidogo, hivyo walipoingia tuu chapu wakavaa vinyago usoni na Cecconi akapiga kelele, "Mikono juu, tuko hapa kuiba, toa kila kitu!."
Kwa bahati mbaya mwenye duka hilo (Bruno) alikuwa ametoka kuibiwa vitu vyake dukani hapo siku chache tuu zilizopita, hivyo akaitoa bunduki haraka na kumfyatulia risasi Cecconi kifuani bila kujua ni rafiki yake na hapo alikua anamfanyia utani tuu.
Cecconi alikufa nusu saa tuu baadaye hospitalini kutokana na risasi hiyo akiwa na umri wa miaka 28, ambapo maneno yake ya mwisho yalikuwa, "Ni utani, ulikuwa mzaha tu." Hili Ilikuwa janga kubwa sana katika jamii ya soka huko Italia na klabu ya soka ya Lazio kwa ujumla.