Advertise here

Simulizi: Miss Peppy

Simulizi

Member
MISS PEPPYπŸ₯΅πŸ’¦πŸ”₯
SEHEMU YA 01~05
_________________________________

Linapokuja swala la kukimbia Mimi ni zaidi ya upepo πŸ˜‚, No! ni zaidi ya kasi ya risasi.....najikubali sana kuliko kitu chochote wala sihitaji maoni yenu 🀸

Jina langu naitwa Manuu watu wengi wanapenda kuniita Miss peppy πŸ₯°
Najua unajiuliza maswali mengi kwanini wana wa ulimwengu walinipa hili jina πŸ™„

Jibu lake ni simple tu, nguvu niliyonayo mikononi mwangu inauwezo wa kusafarisha Mlima Kilimanjaro kutoka Africa hadi Ulaya πŸ‘Œ

Nadhani sasa tumeelewana kwanini naitwa hivi, tuachane na hiki ki introduction

Juzi kati nilimwambia Mama huu mwaka ni wa kuforce lakini yeye pamoja na mifugo yake walinicheka 🧐 nilikubaliana na ule msemo usemao nabii hakubaliki kwao ingawa iliniuma sana why Mama ana mchukulia poa miss Peppy πŸ₯° kubwa la maadui linalo ogopeka hadi na upepo πŸ˜€

Nilitamani kumuambia kuhusu simu kutoka Kampuni la Coca-Cola ikinialika kushiriki shindano la kukimbia linalofanyika Kitaifa Jijini Odes, lakini moyo wangu ulisita nilizingatia ule msemo usemao "acha mafanikio yaongee yenyewe" sijui ndio hivi πŸ˜‚ I don't care kikubwa mmeelewa

Duniani hakuna siri my zangu, nikiwa busy kupanga nguo mbili tatu....washikaji zangu pamoja na jamaa zao walikuja nyumbani kwetu.

Hapa ndipo niliiona aibu ya Mama pamoja na mifugo yake 🀸 Yeye na Kuku zake walitukana mamba kabla ya kuvuka mto I feel sorry for them 🀣

Lakini tukiachana na Mama, washikaji zangu pamoja na marafiki zao wana sifa sana kushinda lile kabila πŸ˜…, nilitarajia wangekuja pekee yao tu lakini walialika kila kaya hapa kijjini kwetu....dakika 20 zilikuwa nyingi uwanja wetu ulifurika watu kana kwamba tuna kikao cha dharula.

Ilinilazimu ni kae juu ya mti ili kila mtu aweze kuniona, sikutaka kuvunga sana nilimruhusu Mama na mifugo yake walie 🀣 kwa sababu hawakuamini kama naenda Jijjni Odes

Washkaji zangu waliweka kapu chini, kila mtu alianza kuweka alichonacho. Watu wa kijjji hiki wana balaa huwezi kuamini, nilipewa kuku, mitego ya panya, mahindi, cement pamoja na hirizi kubwa ya kuleta bahati 😩

"Jiji la Odes halina tofauti na Ulaya....sina hakika kama nitapata gari la kuweka vitu hivi" Nilijikuta ni kiongea

"Hizi ni baraka kutoka kwa watu wa Kijiji hiki, naomba usikatae zawadi zao...."Mama aliniambia

Sikuona sababu ya kubishana na watu waliokula chumvi.....niliingia bafuni kuoga kisha ni kabebewa begi langu.
Mimi kama Mimi sikuruhusiwa kutembea, niliwekwa begani kwa Hawafu mwenye nguvu πŸ˜…

Njia zima walishangilia Miss peppy πŸ₯°, Miss peppy πŸ₯° my cupcakes hakika nilijiona dhahabu kwa namna nilivyopewa heshima na watu hawa.

Gari linaloelekea Jijini Odes lilisimama, vitu vyote nilivyo zawadiwa viliwekwa

"Hakikisha unarudi na ushindi....Miss peppy πŸ₯°" Mshikaji wangu wa karibu kuliko wote alizungumza

"Kuwa makini Jijini Odes kuna wanaume wazuri kama dhahabu ✨.....lakini ni waongo wakubwa, usije kumuamini hata mmoja, Hawafu mwenye nguvu ana kusubiria pindi utakaporudi na ushindi mtafunga ndoa" Mama aliongea huku akiachia tabasamu πŸ˜‡

Nilimchungulia Hawafu mwenye nguvu nione anasemaje, Mwanaume huyu ni kichaa aki πŸ˜… alinitunishia msuli kuonesha ananiweza

Niliwaaga watu wote kisha ni kamruhusu dreva aondoe gari, Oyooo Miss peppy πŸ₯° naenda zangu Odes..... nilijikuta ni kipiga kelele za furaha
Itaendelea πŸ”₯

*MISS PEPPYπŸ₯° 02*

Kitendo cha kuliona Jiji la Odes akili ziliniruka 😩 nilisahau zawadi zote nilizopatiwa kwenye gari, haikuniuma sana coz sikuvutiwa navyo

Kizunguzungu cha ghafla kilinishika kutokana na kugeuka huku na kule....majengo yalikuwa marefu sana misili ya ngazi za kuzimu πŸ˜€

Kila mtu aliyepita mbele yangu nilimfananisha na katuni ya Cinderella πŸ˜‹ My zangu watu wa Jijini Odes walikuwa ni wazuri kupita kiasi

"Welcome, jina langu naitwa Sasha karibu katika hotel ya little star ujipatie chakula kizuri sawa na cha Mfalme" Binti mrembo aliyevalia sare alizungumza na Mimi

Tangu ni zaliwe sikuwahi kukaribishwa kula kwenye hotel za kifahari, poor me ukarimu wa watu wa Odes ulinichanganya sana....ule msemo usemao mwenye nacho atazidi kuongezewa uliwafaa watu wa hili Jiji πŸ˜‡

Nilikaa mezani nikaletewa chakula, Manuu Mimi nilijikuta nikila kila chakula nilichokuwa naletewa.

Tumbo lina ukomo, nilinyoosha mikono juu kumaanisha nimetosheka πŸ–οΈ

"Utalipia shilingi laki nne hapo mlangoni...." Kauli hii ilipasua ngoma ya sikio langu πŸ˜“

Nilijikuta nikilia bila kukoma kwa sababu pesa yangu haikutosha kulipa gharama niliyotajiwa

"Piga simu Polisi haraka iwezekanavyo waje kumchukua huyu panya😏...." Mwanaume aliyevalia suti alizungumza akionekana kukosa huruma

Nilikuwa tayari kukamatwa bila kufanya fujo yoyote but why this crazy man aniite panya.... nilijikuta ni kimpiga ngumi moja iliyopelekea apoteze fahamu

"Kamwe usije kumuita binadamu mwenye meno 32 panya....ukirudia nitakuua kisha nitakuzika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, pengine hamjui Mimi ni nani.....naitwa Miss peppy πŸ₯° kubwa la maadui" Niliongea kwa mkwara

Watu wote walionekana kunywea, nilitumia udhaifu huu kuomba nifungashiwe vyakula.....kila kitu kilifanyika haraka, niliondoka kwa kukimbia sikutaka kukamatwa πŸ˜‚

Nilisimamisha tax nikaomba nipelekwe kwenye Kampuni la Coca-Cola. Cha ajabu dreva aliondoka....sikuelewa kwanini kanipuuzia pengine ni kutokana na mavazi niliyovaa

"Stupidity...." Nilijikuta ni kitukana, pengine hata nyie mnanichukulia poa lakini hiki kichwa kimesoma....nipo vizuri kwa taarifa yenu πŸ˜…

Nilishika simu yangu nikaipigia namba iliyonipa mualiko.
Nilitoa maelekezo sehemu niliyokuwa nimesimama..... niliachia tabasamu baada ya kuelezwa gari la ofisi litakuja kunichukua

Nikiwa nimekaa hapa, niliwashuhudia wanaume wanne wakihangaika kusukuma gari lililokwama kwenye tope.

Nilitikisa kichwa changu kwa namna walivyokuwa wanahangaika 😁
Nilihitaji kuwa sehemu ya msaada, nilisogea nikasukuma gari kwa mkono mmoja

"Naitwa Manuu a.k a Miss peppy πŸ₯° kubwa la maadui..." Niliwaambia baada ya kuwasaidia

"Kampuni la Nike linatafuta bodyguard kwa ajili ya kumuwekea ulinzi CEO fika haraka ofisini kwetu please usipitwe na hii bahati" Mmoja wa Wanaume hawa alizungumza akionekana kunikubali kinyama

Niliachia tabasamu baada ya kuona wamenikubali.....nilirudi kusimama nilipokuwa.

Muda ulizidi kwenda, nilirudia kupiga simu tena, bahati nzuri gari lilifika kunichukua

Ushuzi ulitaka kunipita baada ya kukutana macho kwa macho na Mwanaume niliyempiga ngumi katika hotel ya little star kwa kosa la kuniita panya 😫

"A big looser.....rudi Kijijini kwenu nafasi hii nitampa mwingine" Mwanaume huyu aliongea kisha akaondoa gari

Manuu Mimi limenikuta 😩, niliwageukia wale wanaume niliowasaidia....bahati mbaya hawakuepo

Ni mwaka wa kuforce huu siwezi kurudi nyumbani kwa aibu 😭....nilisimamisha tax nikaomba nipelekwe kwenye Kampuni la Nike

Nikiwa nimetulia kwenye seat, nilipatiwa jarida nijisomee huku safari ikiendelea....ukurasa wa tatu ulikuwa na picha ya Kijana mzuri kupita maelekezo sikutaka kujua habari inaongelea nini nilichana huo ukurasa kisha nikautia kwenye mfuko wa suruali yangu πŸ˜…
Mapigo ya moyo wangu yalizidi kwenda juu kila ni kifikiria muonekano wa kijana kwenye picha

"Tumefika.....sogea hapo getini Walinzi watakupa maelekezo" Dreva aliongea

Nilishuka haraka ni kihofia kudaiwa ukurasa wa gazeti niliouchana

Cha ajabu sura iliyokuwa kwenye gazeti nilikutana nayo kwenye bango kubwa lililoandikwa "just do it" ⛸️

Moyo wangu ulilipuka hasa nikimtazama Mwanaume huyu aliyeshikiria kiatu mkono wake wa kulia πŸ˜€

"Can you marry me?" Nilijikuta nikiiuliza pich

*MMISS PEPPY πŸ₯° 03*

"Wee ng'ombe sogea hapa, kulitazama tu hilo bango pesa inasoma do hurry please usikie bill unayotakiwa kulipa" Sauti iliyojaa dharau iliniita,

Nilianza kutembea haraka tena nikiwa na uoga wa hali ya juu lakini baada ya kukumbuka nimeitwa ng'ombe nilishikwa na hasira 😬 ni kapunguza mwendo

"Umekuwa kobe mara hii!....fanya haraka kukaribia hapa au ni kufungulie Mbwa" Mlinzi huyu alizidi kunipanda kichwani

Mara nyingi nikiwa na hasira na sina cha kufanya huwa nalia 😭, watu wote waliokuwa hapa walinigeukia kwa namna nilivyokuwa nalia kwa sauti

Kama nitasema nimuadhibu mtu huyu kwa kuniita ng'ombe sitaruhusiwa kuingia getini..... kwahiyo my zangu msishangae kwanini Manuu Mimi nimechagua kulia πŸ˜€

Nikiwa katika kulia, gari kali aina ya Rolls_Royce Sweptail ilisimama getini, poleni ndugu zangu naelewa mmezoea kusikia majina kama Suzuki, Prados na mengineyo πŸ˜‚ semeni ahsante kwa kuwatajia gari jipya though it's my first time kuliona gari pia

Macho yangu yalitekwa 😱 baada ya kumuona Mr. Handsome aliye changanya akili yangu kiasi cha kuchana ukurasa kwenye gazeti....sijui aibu ilitoka wapi nilichukua begi langu ni kajificha πŸ˜€.....harufu ya marashi yake yalidumu puani kwangu.

Aliacha maelezo getini kisha akaingia kwenye gari lake

Nilimsogelea Mlinzi aliyeachiwa maelekezo
"Nipo hapa kuwania nafasi ya bodyguard....nipeni fomu haraka nijaze 😁" Niliongea huku nikionesha haraka

Nilikula kibao cha kichwa ni wazi kabisa niliongea upuuzi

"Hii sehemu inaogopeka na kila mtu. ..umepata wapi nguvu za kuleta pua lako hapa, ondoka haraka kabla sijakasirika sahau kuhusu deni nililotaka kukutajia....kama unataka kazi lifuate hilo gari" Mlinzi huyu alizungumza huku akinipandisha kwa kunikadiria 🧐

Nilisikia uchungu mkali kupita kiasi kwa jibu nililopatiwa, poor me 😭 nimepoteza nafasi ya kushiriki shindano la kukimbia masafa marefu sababu ya ujinga wangu, sipo tayari kuipoteza hii nafasi pia.

Sikutaka kujua habari kuhusu begi langu, nilifunga vizuri kamba za viatu vyangu.....nilivuta pumzi kidogo kisha nikatoka mbio mfano wa risasi πŸ˜‚

Nilianza kulifukuzia gari lilitoka hapa dakika 10 zilizopita ni kiamini nitapata kazi

Sura ya Mr. Handsome aliyekuwa kwenye bango ilinichanganya.....sitaki kujua kama yeye ni ghost au an Angel nachotaka Mimi ni kumuwekea Ulinzi....kadiri nilivyozidi kukimbia ndivyo nilipata nguvu ya kujiona nastahili kuwa bodyguard.....nilifanikiwa kulifikia gari

Nililitangizia kwa mbele huku mapigo ya moyo wangu yakienda juu πŸ₯΅

Kioo cha gari kilishushwa....kwa mara nyingine tena nilimuona Mr. Handsome

"Nipo na haraka ondoa hiyo takataka" Mr. Handsome aliongea, moyo wangu uliumia 😭 being rubbish inauma aisee, why aniite takataka

Walinzi wake watatu walinisogelea, hii ndio ilikuwa nafasi pekee ya Mimi kulitangaza jina langu kama Miss peppy πŸ₯°

Niliwasalimu πŸ–οΈwote kwa ngumi moja moja kisha ni kamsogelea Mr. Ni Handsome

"Naomba niwe bodyguard wako....." Niliongea nikiwa nimetazama chini 😌, uzuri wake ulinifunga kumzoea πŸ˜€


*MISS PEPPY πŸ₯° 04*

"Naomba tuzungumze siku nyingine kuhusu kazi...kuna sehemu moja muhimu sana nawahi" Mr. Handsome aliongea

Jibu lake lilinikatisha tamaa 😩 do you know what unaweza kuwa mzuri wa sura lakini si moyo....mtu huyu anaonekana kuwa na roho mbaya, sikusita kumtupia ukurasa niliouchana kwenye gazeti
6
Huwezi kuamini mlango ulifunguliwa kisha Mr. Handsome alinipa ishara ya kuingia.

My cupcakes, sitaki kujua naenda kufa au kutupwa kusikojulikana πŸ˜€ kitendo cha kuruhusiwa kuingia kwenye gari kilinipa nguvu sana.
Nilitegemea kuulizwa hey Mama panya kwanini ulichana huu ukurasa? But haikuwa hivyo 😁 guess am lucky

Walinzi wake waliingia pia, safari iliendelea....kila mtu niliyemtazama alionekana kuwa bize na simu yake kuliko kawaida.

Muda wote Mr. Handsome alikuwa na kazi ya kupokea na kukata simu.
Kwa muonekano tu alikuwa amechoka sana.... kujipendekeza siyo dhambi au mnasemaje washikaji πŸ˜‚ nilinyoosha mkono wangu ni kaanza kumkanda kanda mabega wazungu tunaita massage

Mwanzo alinikatalia, nikataka kukata tamaa lakini Mlinzi wake mmoja alinipa ishara ya kuendelea

Guys! niliendelea na hili zoezi mpaka tulipofika uwanja wa ndege

Tulishuka kwenye gari kisha tukakaa kwenye6 viti vilivyokuwa hapa airport special kwa kusubiria wageni

Niliendelea kujipendekeza kwa Mr. Handsome 😍 kwa kumfutia viatu vyake na kitambaa changu japo havikuwa vimechafuka

Ghafla tu nilimuona akiachia tabasamu πŸ˜‡, mwanzo nilihisi anafurahia huduma yangu lakini baada ya kuchunguza niligundua hanitizami Mimi,

Kuna sauti iliniambia Manuu turn about
Niliitia hii sauti, niliacha kufuta viatu ni kageuka nyuma

My zangu 😭....nilikutana na Binti mrembo kuliko hata Mr. Handsome....mwendo wake wa maringo ulitosha kutengeneza upepo mwanana

Sijui Mr. Handsome alisimama saa ngapi kwenye kiti chake.... kufumba na kufumbua nilishuhudia watu wamekumbatiana 😭

"Axel hukuwa na haja ya kuja hapa, sitaki kuamini umeharibu ratiba zako just for me" Binti mrembo kuliko wote duniani alizungumza kwa kudeka πŸ˜…

Nilitumia nafasi hii kujipendekeza zaidi ingawa roho yangu ilikuwa inauma, nilimbebea begi lake dogo ambalo Walinzi wengine hawakuliona πŸ˜… sijui walifeli wapi

"Naitwa Manuu, call me Miss peppy πŸ₯° itapendeza zaidi ni bodyguard wa Axel" Nyie watu nilitumia nafasi hii vizuri kujiajiri bila ruhusa ya Mr. Handsome πŸ˜‚...

*MISS PEPPY πŸ₯°5*

"Naitwa Babeth....nimefurahi kuona my man kaajiri bodyguard wa kike" Babeth aliongea huku akiachia tabasamu πŸ˜‡

Aki! kuna watu wazuri duniani, kama ni kiwatumia picha yake am sure mtaigeuza kuwa hirizi ya bahati πŸ˜‚

Mapigo ya moyo wangu yalisimama 😴 baada ya kusikia Babeth yupo Jijini Odes kushiriki shindano la Marathon lililoandaliwa na Kampuni ya Coca-Cola

Nilijikuta ni kiikumbuka ile siku nimepigiwa simu kuhusu kushiriki pia..I don't know nani alinifanyia application, maybe ni washikaji wangu😭 niliomboleza ndani ya moyo wangu

"Kila kitu nitasitisha siku ya kesho, ni lazima nije kuku support" Axel au Mr. Handsome alimuambia sukari wa moyo wake kisha akanigeukia Mimi

"Bado sija kuapprove kuwa bodyguard wangu for the time being siyo mbaya ukiambatana na Mimi" Axel aliniambia

Nilitikisa kichwa ni kijua kabla siku tatu hazijaisha atanikubali

Axel alimpeleka Babeth katika hotel ya kifahari kwa ajili ya kupumzika....kuna namna moyo wangu ulikuwa unawaka moto mwekundu πŸ”₯ kwa wivu

Nilitaka kumfuata lakini alinizuia, guys niliambiwa nibaki kumsaidia Babeth....in short niligeuka kuwa maid wake 😩

Mrembo huyu hakuwa anajua chochote zaidi ya kuremba uso wake, siyo kwamba alikuwa anaigiza...na si kwamba namchongea πŸ₯΄

Just Imagine hata kufungua chupa ya maji ni mahangaiko tu....niliamua kutumia nafasi hii kujipendekeza, always Miss peppy πŸ₯° huwa hakosei hivyo nilinyoosha kila kitu kama rula

Hakika uchawi upo bwana, sijui ni nini kilitokea ule ukurasa niliouchana kwenye gazeti la dreva wenye sura ya Mr. Handsome 😍 ulidondokea miguuni kwa Babeth πŸ˜‚

Isome yote kwa kulipia Tsh 1000

WhatsApp 0742133100
 
MISS PEPPYπŸ₯΅πŸ’¦πŸ”₯
SEHEMU YA 06~10
_________________________________

Haikuwa ugomvi hata, sikia nilichoambiwa πŸ‘Œ

"Watu wengi wanampenda Axel.....ni mzuri naturally hivyo sioni ajabu wewe kutembea na huu ukurasa" Babeth aliongea huku akiachia tabasamu πŸ˜‡

Hakuishia hapo aliniwekea ukurasa wote mdomoni akaniamuru niutafune 🀣

Nilifanya kama atakavyo....nilitamani ukurasa nilioumeza ugeuke kuwa Axel anitie mimba huko tumboni πŸ˜‚ lakini haikuwezekana

Sijui nililala saa ngapi lakini nilishtuliwa na sauti ya Babeth 😩 kulikuwa kumepambazuka

"Beba hilo begi....make sure hakipotei kitu hata kimoja, nitafurahi kama utakuja uwanjani kunishangilia" Babeth aliongea huku akinywa maji

Nilimfuata nyuma huku nikiwa nahisi usingizi bado....Axel na Walinzi wake watatu walikuwa wanatusubiria tuliingia wote kwenye gari

Kwa namna fulani moyo wangu uliumia kwa sababu nilipaswa niwe miongoni mwa washindani lakini nilipoteza nafasi hii πŸ˜“

Babeth pamoja na washiriki 89 walianza kukimbia....japo hakajui kufanya kazi lakini miguu yake ilikuwa miepesi sana. Axel alikuwa ana mshangilia.....ilinilazimu kujipendekeza pia πŸ˜‚ nilianza kushangilia

Kuzimaliza kilometa 42.195 haikuwa rahisi..... huwezi kuamini Babeth alikata utepe kwa kuwaacha watu 89 nyumaπŸƒ

Furaha ya Axel ilikuwa kubwa sana I can't explain it kwa sababu nilishtukia tu akinikumbatia πŸ˜‚

Mwili wangu wote ulikufa ganzi....ni raha sana kukumbatiwa na mtu unayemuelewa 😘....nilitumia nafasi hii kumkumbatia pia 🀣 keep in mind bahati haijagi mara mbili

Kila kitu kilifanyika haraka, Babeth alikabidhiwa kombe la dhahabu πŸ† pamoja na kiatu cha dhahabu

Ilikuwa ni furaha sana kwa Axel na Babeth....machozi ya uchungu yalinitoka, niliamini watu wa Kijiji changu watakuwa katika wakati mgumu kuhusu Mimi 😭

Nilishika simu yangu ni kamtumia ujumbe Mshikaji wangu nikiamini atawasomea watu wote πŸ˜“

I promise kabla sijaondoka Jijini Odes nitabeba kombe la dhahabu....ni lazima nitengeneze nafasi by any means 🧐

Sherehe kwa ajili ya kumpongeza Babeth iliandaliwa na Axel
Watu wengi walihudhuria..... niliendelea kuwa Maid wa Babeth

Niacheni nilie kwanza 😭, kitu alichofanya Mr. Handsome kilikuwa ni tishio kwa moyo wangu....my zangu Mwanaume huyu alimvika pete ya uchumba Babeth, infront of everyone alimtangaza kama mchumba wake 😴

Watu wote walishangilia....what hurts me most ni pale watu hawa wawili walipo kiss 😘

Wakati furaha inaendelea kwa wawili hawa, Chui mkubwa aliyeonekana kutoroka katika banda lake alikuja kwa kasi usawa wa Babeth na Mr. Handsome 😩

Walinzi walianza kuachia risasi hovyo huku watu wengine wakikimbia.

Nilihitaji Axel anipitishe haraka kama bodyguard wake wa kudumu.... being Miss peppy πŸ₯° siyo sifa hili jina linanifaa.

Nilikusanya nguvu zangu zote, kabla chui hajawafikia wapenda nao.
Nilimpiga teke moja lililompelekea apoteze fahamu

"I cannot kill mali ya serikali just nimemzimisha tu....waite wahusika waje kumchukua" Niliongea huku ni kiachia tabasamu 😊
Watu wote walipiga magoti yao wakanisujudu as if ni Malkia Elizabeth wa II πŸ˜‚


MISS PEPPY πŸ₯° 07

Macho ya Axel yalitosha kuniambia kanipokea rasmi

Isingekuwa rahisi kuendelea na sherehe nina uhakika kuna watu mahali hapa wamejinyea kama si kujikojolea πŸ˜‚ siyo kazi yangu kuwabaini try to guess ni kina nani πŸ‘Œ

Guys! sikuamini macho yangu pale Mr. Handsome 😍 alivyo ni kumbatia mbele ya honey wake πŸ˜‚

"Kama si msaada wako sina uhakika kama tungekuwa tuna zungumza hivi.... kuanzia sasa na kuendelea utaishi nyumbani kwangu, wherever I go utanifuata.....in a simple way utakuwa kivuli changu, juhudi zako ndizo zitalinda nafasi yako" Axel aliongea

Nilimgeukia Babeth nione kama ana feel jealous lakini nilikutana na tabasamu 😊 kumaanisha yupo okay

"Nitarudi kuishi Jijini Odes rasmi kabisa baada ya mwaka mmoja.....naamini utamlinda my man kwa nguvu zote " Babeth aliniambia huku akitabasamu 😊

Nilitabasamu pia kuashiria najali kuhusu Axel

Wawili hawa walilala hotelini chumba kimoja.....nilisimama mlangoni kuhakikisha nothing bad inawapata 😭

Namshukuru mmiliki wa hii hotel kwa design ya milango aliyoweka vyumba vyote, pamoja na kuegemeza masikio sikusikia chochote thanks unknown mmiliki pengine ningekufa kwa presha πŸ˜‚

Kulivyo pambazuka asubuhi, Babeth alipelekwa airport tayari kwa kurudi China kisha Mimi na Axel pamoja na Walinzi wake watatu tulielekea nyumbani kwa CEO wa Kampuni ya Nike πŸ˜… hiyo kiatu anayo vaa boyfriend akiwa katika uwanja wa mpira huyu mwamba ndio anapendezesha hiyo miguu

Nilipatwa na kifafa cha macho😱 baada ya kuiona nyumba ya Axel....kwanza let me apologize makazi ya huyu mwamba hatuwezi kuita nyumba. Ni Kasiri a.k.a Mansion 🀣

Kulikuwa na utitiri wa Wafanyakazi mahali hapa as if ni kiwanda cha maziwa

Sikuvunga kuokota mapera yaliyokuwa yamedondoka chini nikayaweka tumboni kwangu πŸ₯΄

"Huyu anaitwa Manuu ni bodyguard wangu mpya....hakikisha mnampa heshima zote" Axel alitoa maagizo πŸ–οΈ

Supervisor wa Wafanyakazi wote wa hii Mansion alinikabidhi funguo ya chumba changu

"Ukiwa ndani ya mansion hii naomba usisahau kama Mimi ndio boss wako hata Axel hawezi kuingilia katika hili.....kwahiyo soma sheria zote nilizoandika humu ndani ili twende sawa" Supervisor aliyejitambulisha kwa jina la Lady Oh alizungumza akaniwekea vitabu πŸ“š kisha akaondoka

Nilifunua kitabu cha kwanza, guys sikuweza kusoma.... Mimi si mtu wa kupenda kusoma vitabu visivyo na picha 🀣

Nilikiweka pembeni kisha ni kajitupa kitandani....cha ajabu kitandani kilinirusha huku kikiongea enter password πŸ˜…

Nilijikuta ni kikodoa macho 😩 tangu ni zaliwe sikuwahi kusikia hizi mambo za kuweka neno la siri kwenye kitanda ili ulale πŸ˜…

Nilifunua kwa mara nyingine kitabu nikakutana na Password....jina la Axel ndio lilikuwa password ya kitanda.

Baada ya kujaza password nilijitupa kitandani.....niliwish Mr. Handsome 😍 akuje tulale wote na si kumuweka tu kama password kwenye kitanda nacholalia πŸ˜‚

Sikumbuki ilikuaje lakini nilikuja kushtuliwa na kengele

Guys! nilichanganyikiwa baada ya kusikia ndani ya Mansion hii kuna parade..,a.k.a morning assembly 🀣

Poor me! sikuwa nimeoga wala kufanya chochote.... moyo wangu ulilipuka πŸ”₯ kumuona Supervisor Lady Oh akiwa kavaa sare utadhani Askari wa jeshi la Palestine

"Muonekano wako unatosha kuniambia hujasoma vitabu vyangu...." Lady Oh alifoka, cheche za mate yake ziliniruikia

Wakati na shangaa shangaa kauli ilitolewa

"Askari wa zamu kamata huyu mtu....arrest her at once 😡" Lady Oh alizungumza akiwa amefura


MISS PEPPY πŸ₯° 08


Najua mnaweza kucheka but haikuwa movie aisee πŸ˜… nilikamatwa. Sikutarajia kuona gereza kwenye hii Mansion 🀣

Sikuwa mfungwa pekee yangu nilikutana na sura zingine zikiwa zimelala, tena walikuwa wamevaa sare kabisa πŸ˜‚

I come to realize, katika hii dunia kuna watu wana maisha kiasi cha kujenga magereza kwenye nyumba zao I believe hata jehanamu itakuwa kwa hii area ni vile bado sijawa mwenyeji πŸ˜…

Nililetewa sare za mfungwa, without hata kujitetea😁. Nguo zenyewe zilikuwa oversize sikuona hata sababu ya kuvua nilizokuwa nimevaa

Wafungwa waliokuwa humu walikuwa ni wakali as if wana Malaria kwenye brain yao. Walitaka kunipanda kichwani lakini sikuwa tayari, niliset example kwa kumtegua mkono mmoja wao 😠

Heshima ilipatikana, nilitega sikio kusikia story kuhusu Lady Oh, Supervisor wa Wafanyakazi wote

Guys nilisikia kutetemeka πŸ˜‚ huyu mwanamke ni best friend wa Undertaker legend wa WWE.... inasemekana mshipa wa huruma ulivunjika akiwa na miaka 15 , hivyo baada ya kuajiriwa tu kwenye hii Mansion alisuggest kujengwe gereza 😩

Watu wote tulikaa kimya baada ya kumuona Askari.... geti lilifunguliwa kisha ni katolewa nje

Nilishtuka baada ya kumuona CEO, my Axel a.k.a Mr. Handsome 😍. Msinionee wivu kila mtu ana namna yake ya kumuita crush wake 😌

"Nimelipa faini utoke gerezani....make sure haufanyi makosa tena. Hili kasiri ni la kwangu but sheria zinanifunga kuingilia majukumu ya Lady Oh. Badilisha mavazi yako haraka iwezekanavyo twende kazini" Axel aliongea

Nilimshukuru kisha ni kaondoka kwa kukimbia, poor me nilijikuta ni kizunguka huku na kule nisione mlango wa kuingilia 🀣 nilijikuta ni kirudi pale pale

"Unanichelewesha nifuate...." Sauti ya Axel ilinishtua

Nilimuomba msamaha kwa kujiona mwenyeji kwenye jengo hili 😫

Nilivaa nguo haraka bila kuoga, ile natoka na CEO nilishtukia nimekamatwa na Askari wawili wakiwa na Lady Oh 🀣

Guys nilivuliwa nguo kisha ni katupwa bafuni.. nywele za sirini zilifyeka haraka haraka kama wanakata mboga ya majani πŸ˜…

Hellow are you there πŸ–οΈ dakika 20 zilitosha kubadilisha muonekano wangu. Nilijikuta nikikodoa macho kwenye kioo

"Hivi ndivyo unapaswa kuwa.... hakikisha unasoma vitabu vyangu otherwise utaregret kuwa hapa 😠" Lady Oh aliniambia kisha akaondoka

"Unafanya nini time is running out πŸ₯΄" Sauti ya Axel ilinishtua nikiwa bize na kioo

My zangu 🀣 halikuwa lengo lakini niliteleza bahati mbaya.... uwezo wa kuzui miguu yangu isianguke nilikuwa nayo because am Miss peppy πŸ₯° but nilitaka nidakwe na hii Crush yangu πŸ˜…


MISS PEPPY πŸ₯° 09


Hebu nilie kwanza 😭, Axel alinikwepa ni kaanguka chini
Ilikuwa ni aibu kubwa kwangu na hata nilishuhudia avocados zikinizomea πŸ₯‘

Tuliingia kwenye gari nikiwa nimefura I can't explain.... hasira yangu ilikuwa juu kupita maelezo 😑

Sijui kuendesha gari but since ni bodyguard wa huyu Kichaa niliomba niendeshe gari 🚘 lengo langu lilikuwa ni kufa na Mr. Handsome 😍

Kitendo cha kukabidhiwa gari tu watu wote walipiga kelele 😡 sikutaka kusikia gharama ya injini ya gari lake....tulianza kupaa, najua huwezi kuamini but hata gari kuna muda zinapaa like aeroplane πŸ›©οΈ especially dreva akiwa kavurugwa πŸ₯΄

Kama nilivyosema mwanzo lengo langu ni kufa na CEO nililiacha gari likaingia kwenye bahari, nilifumba macho kusubiria mazishi yetu lakini 🀣....sijui hata nisemeje but hili gari liligeuka kuwa meli

Likiwa ardhini ni gari but likiwa baharini ni Meli πŸ˜….... ni technology mpya huko kwenu nahisi itafika siku ya kihama

"Sababu ya ujinga wako nimechelewa kikao.... naomba usirudie kufanya huu utoto tena 😠.... hakikisha unajifunza kuendesha gari, ndege, meli na vyombo vyote vya injini ambavyo sijakutajia" Axel alizungumza kisha akampa ishara Mlinzi mwingine akae usukani

Aliendesha gari_meli tukatokea Nchi kavu.... ndani ya moyo wangu sikujuta kwa lolote πŸ˜‚ wala kujipendekeza kusema sorry

Ofisi ya Axel haikuwa tofauti na hoteli....hakika sijuti kuwa bodyguard wa huyu mtu 😌

Mezani kulikuwa na chai, nilitaka kujipimia lakini Axel alinipiga stop 😫 alinipatia kazi ya kumsogezea mafaili

Nilimaliza hii kazi kwa haraka nadhani hata yeye hakutarajia....nilinyoosha mkono ni chukue apple🍎 kutuliza tumbo langu lakini nilipatiwa kazi nyingine

Nilisikia kukasirika 😠 ina maana hivi vyakula,matunda na bites zote zilizopo hapa ni mapambo? au ni kwa sababu sijaomba msamaha kwa kosa nililofanya dakika chache zilizopita? Noo! huyu mtu ana roho mbaya πŸ˜‚ sikuona sababu ya kuhangaika naye tena

Nikiwa nimekata tamaa ya kula chochote nilirushiwa vitabu πŸ“š

"Hivyo vitabu ni sheria na kanuni kuhusu bodyguard.....kumzimisha chui siyo tiketi ya kukaa karibu yangu the moment utashindwa kumatch na hizo sheria nitakufukuza kazi πŸ–οΈ" Axel aliongea kisha akaendelea na kazi zake

Nilifunua kitabu cha kwanza kilikuwa na maandishi madogo madogo, sikuweza kuendelea nacho....kitabu cha pili kilikuwa hakina mchoro hata mmoja nilikiweka pembeni pia.....kitabu cha tatu kilikuwa na michoro inayoonesha namna ya kukabiliana na hatari....nilitaka kukisoma lakini michoro yake ilikuwa na rangi mbaya πŸ˜… sikukisoma pia

Axel aligonga meza kwa hasira ni wazi kabisa alikuwa ananitazama, nilishtuka kiasi cha kutaka kukimbia πŸ˜‚


MISS PEPPY πŸ₯° 10


"Kwanini hupendi kusoma vitabu?" Axel aliniuliza

"Ni kwa sababu siyo hobby yangu.... napenda kusikiliza na si kusoma, kama inawezekana naomba uviweke hivi vitabu kwenye mfumo wa audio.... please" Niliongea nikiachia tabasamu 😁

Kwa mara ya kwanza kabisa nilikisikia kicheko cha Axel πŸ˜…
Alionekana kufurahishwa na jibu langu.... kabla hajaongea chochote Mlinzi alikuja

"Sorry Boss, farasi wako anaonekana kuchanganyikiwa.....watu wanashindwa kufanya kazi kwa sababu anakimbia hovyo" Mlinzi aliongea

"Kwahiyo mnataka Mimi ndio ni kamtulize farasi....kwani mmesahau kama hili ni jukumu lenu 😑" Axel alifoka kiasi cha kumtisha Mlinzi

They say grap an opportunity pale mijitu mingine ikiwa imelala πŸ˜‚

Sikutishwa na urefu wa hili jengo being Miss peppy πŸ₯° si mchezo....nilipitia dirishani I believe kila mtu aliamini nimekufa but haikuwa hivyo

Nilimkimbilia farasi aliyekuwa tishio kwa watu.....ngoja niwaambie my zangu, kila mtu hapa alimtafsiri farasi kama kachanganyikiwa but haikuwa hivyo it was a heartbreak 😭 huyu farasi alionekana kumkumbuka fiance wake....am sure hapa kulikuwa na farasi wa kike I wonder where alipelekwa

Nilimkimbiza farasi huku ni kimuambia it's okay not to be okay πŸ˜‚....hakuwa na haja ya kuwa tishio kwa watu.

Nilifanikiwa kupanda mgongoni kwake...

"Najua upo na maumivu ndani ya moyo wako, lia kadri uwezavyo huna haja ya kufanya fujo....kilio pekee kinatosha kutibu moyo wako" Nilimuambia kwa kumbembeleza

My Cupcakes 😍 hamuwezi kuamini farasi alitulia

Axel pamoja na Wafanyakazi wengine walikuja kujua nini nimefanya mpaka farasi akatulia

"Mrudishe farasi wa kike aliyekuwa haya maeneo πŸ˜…" Niliongea

"Una maanisha nini" Axel aliuliza

"Farasi ana hisia pia kama binadamu.....kamkumbuka fiance wake so bring her back ili amani idumu mahali hapa" Niliongea

"Usiku wa leo nitakuhadithia kwa ufupi sheria zote zilizoandikwa kwenye vitabu vya Lady Oh na vyangu, hii ni zawadi yangu kwa kumtuliza farasi" Axel aliongea kisha akaondoka akiwa na tabasamu 😊

"Hakikisha unamleta fiance wa farasi" Nilimsisitiza huku nikifurahia zawadi aliyonipatia

Watu wote walionekana kunikubali kwa msaada niliotenda πŸ‘Œ

Itaendelea πŸ’₯
 
Back
Top