Advertise here

Simulizi: Moyo wa Kweli

Simulizi

Member
MOYO WA KWELI
1-5

01

(Baada ya kukutana na Ava, alisahau kama safari ya mapenzi ni udanganyifu mtupu....🥂)

Karibu 🖐️

Si kila mtu unayekutana naye katika maisha ni mdanganyifu, wengine ni faraja ilioletwa duniani kuwa tabasamu kwa watu wengine. Ni wachache sana wanaoamini katika huu kweli.

Asilimia kubwa ya watu wanaamini katika mapenzi kuna udanganyifu wa hali ya juu na si ukweli, Easton ni miongoni mwa wanaume wanaoungana na asilimia kubwa ya watu wengine kudai katika mapenzi kuna udanganyifu.

"Watu watakuheshimu zaidi endapo utauthibitishia ulimwengu kuwa upo kwenye mahusiano, mtangaze mpenzi wako siku ya kesho....niamini Mimi hata maadui zako watakuheshimu" Secretary Jo alizungumza kwa ushawishi

"Sivutiwi na mahusiano kwa sasa.... kitendo nilichomtendea Sophia bado kina jirudia kichwani mwangu ingawa ni miaka 7 sasa imepita" Easton (CEO wa Kampuni ya Penfolds inayojihusisha na utengenezaji wa wine aina ya Shiraz) alizungumza

"Sitaki kusikia kuhusu miaka 7 iliyopita, kuna uvumi umezagaa kuwa huenda wewe ni shoga au rungu lako halisimami" Secretary Jo aliongea kwa sauti ya chini

"Ni wazi kabisa hata wao hawana uhakika na mashaka yao.... wachukulie hatua wote unaosikia wakiniita Mimi shoga, kama utawakalia kimya basi watahisi wewe ndio mwanamke wangu" Easton aliongea

"Vipi kuhusu rungu lako ni kweli halina nguvu?" Secretary Jo aliuliza

Easton alifungua zipu ya suruali yake, mashine ilikuwa imesimama kiasi kwamba Secretary Jo alifumba macho

"Sitaki kusikia uvumi wa aina yoyote ile....naamini kila kitu umejionea" Easton aliongea huku akifunga zipu ya suruali.

Ukweli ni kwamba Secretary Jo ana chukizwa na namna boss wake anavyokaa pekee yake kwa muda mrefu bila mahusiano. Na hii ndio sababu ameamua kutunga maneno ya uongo apate faraja ya moyo

Shughuli za hapa na pale ziliendelea katika Kampuni ya Penfolds, Easton alipita huku na kule kukagua namna wafanyakazi wake wanavyotenda kazi

"Nadhani tunahitaji kuajiri wafanyakazi wapatao 200, Kampuni letu limekuwa kwa kasi. Ina mlazimu mtu mmoja kufanya kazi za watu kumi ili kufikia malengo....na hii ndio sababu inayopelekea watu kuja wamechelewa kazini" Secretary Jo alitoa ripoti

"Andaa tangazo la kuajiri wafanyakazi wapya....pia tengeneze ratiba itakayowapa nafasi wafanyakazi kupumzika tukiwa tunasubiria wafanyakazi wapya" Easton alimuachia maagizo Secretary Jo kisha akaingia ndani ya gari lake

Alielekea Supermarket kuchukua vitu muhimu kwa ajili ya Mama yake.
Hakutumia muda mrefu kwa sababu alikuwa anajua ni kipi anaenda kuchukua.

Wakati wa kurudi ilimlazimu kukwepa barabara kuu kuepuka msongamano wa magari hivyo aliamua kupita barabara ya mtaani iliyopo pakana na makazi ya watu.

Akiwa bize anafatilia ripoti mbalimbali kupitia simu kutoka kwa wafanyakazi wake alilazamika kufunga breki ya gari baada ya kunusurika kumgonga binti mdogo aliyekuwa amelewa

Alitaka kumpotezea lakini vurugu za binti mlevi zilimlazimu kushuka kwenye gari

"Wee paka unapata wapi ujasiri wa kumsogelea Mbwa....ulikuwa salama ndani ya gari sielewi ni nini kimekutuma ushuke" Ava aliongea huku akimgonga gonga kifuani Easton na chupa

"Paka?.... umeniita paka!" Easton aliuliza

"Wewe ni paka, tena paka mweusi aliyezeeka.... haya niambie ni kitu gani utanifanya, dunia nzima inaniogopa kwa nguvu nilizojariwa, kuua na kuzika ni swala la kawaida kwangu" Ava alifoka huku machozi yakimtoka

Easton aliachia tabasamu, hakuona sababu ya kuhangaika na mlevi anayetokwa machozi. Alirudi ndani ya gari....ile anataka kuondoa gari, Ava aligonga chupa yake kwa nguvu zote kioo cha gari kikapasuka

Moyo wa Easton ulishtuka, kama asingefumba macho basi vipande vya chupa vingeingia machoni kwake

Ava ndio kushtuka kuwa ameharibu kioo cha gari la watu.

Easton alitaka kuchukua hatua lakini muonekano wa Ava ulitosha kumueleza kama atampeleka Polisi basi atafia gerezani.

Kwa hasira aliondoa gari lake akaelekea nyumbani.

Selena (Mama Easton) baada ya kuliona gari la kijana wake katika hali ile alishika mdomo wake.

Hakutaka kufikiria mara mbili alishika simu akampigia Pacco (Baba mdogo wa Easton)

"Ifike mahala umuache mwanangu apumue.....hakuna kitu utapata kwa kumchanganya na matukio ya hovyo kila siku. Naomba usisahau kama yeye ndio CEO wa Kampuni ya Penfolds.....kura za washirika ndio zimemuweka hapo alipo kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi, endapo utaendelea kumfatilia nitachukua hatua" Selena alizungumza kisha akakata simu hakutaka kusikia upande wa pili unasemaje

"Mlevi alipasua kioo cha gari na chupa yake na si Pacco" Easton alizungumza kwa ufupi

Selena aliziba mdomo wake na mkono baada ya kujua amekurupuka

Siku iliyofuatia, Ava alikuwa wa kwanza kuamka....alipita pita mtandaoni ndipo akafanikiwa kukutana na tangazo la kazi kutoka Penfolds

"Wafanyakazi kazi 200?....kwa wakati huu nitaenda kwa mganga sipo tayari kukosa nafasi pale....ndoto yangu ni kunywa wine ya Shiraz, hapana si kunywa tu nataka niwe miongoni mwa watu nitakao husika kutengeneza...." Ava alijisemea huku akipiga miayo, alikuwa na njaa kali sana

Wakati anashuka kitandani aone nini Mama yake kamuandalia alikumbuka tendo alilolifanyia gari la Easton

*02*

"Halikuwa lengo kupasua kioo cha gari lake...." Ava aliongea pekee yake akaelekea jikoni

"Huoni aibu kuamka saa tano asubuhi, nikupe pole kwa sababu hakutakuwa na chai siku ya leo" Jessica aliongea

"Nimekuja tusalimiane na si kutafuta chai" Ava aliongea

"Kabla hujanywa pombe hakikisha una akiba ya pesa vinginevyo utashikwa vidonda vya tumbo...." Jessica aliongea akijitahidi kuficha maandazi

"Nimeona tangazo la kazi mtandaoni kutoka Penfolds, watu wanao hitaji ni 200 natamani niwe miongoni mwao" Ava aliongea

"Safari hii unahitaji msaada wangu, bila kuoga maji ya baharini hautaambulia chochote....kabla hujatuma maombi ni lazima tufanye kitu," Jessica aliongea

"Kwahiyo unataka nifuate maji baharini? nitaonekana kichaa mbele za watu" Ava aliongea huku pua zake zikinusa maandazi

"Nitakusindikiza ukaoge ndani ya bahari pindi jua litakapo zama, inaweza kuwa hatari lakini faida yake ni kubwa" Jessica aliongea

"Hukuwa na haja ya kuficha maandazi, weka kwenye sahani tule wote.... tofauti na hapo sitakuwa na nguvu ya kuongea na wewe" Ava aliongea

Kwa pamoja walicheka, wawili hawa wanapendana sana

"Naamini Elon (Kaka yake Ava) huko aliko atakuwa sawa....siamini mwanangu kama alikufa ni swala la muda tu kila kitu kitarudi kwenye hali yake" Jessica alijipa natumaini

"Huna haja ya kukaa una mtaja mara kwa mara.....sijisikii kulia asubuhi hii" Ava aliongea huku machozi yakimlenga.

Walianza kula maandazi kwa pamoja wakaachana na habari ya Elon

Upande wa Easton akiwa na Secretary Jo walielekea katika Kampuni la BMW AG kununua gari lingine

"Nipe muda nimtafute mtu aliye husika kuharibu gari lako...." Secretary Jo aliongea kwa sauti ya kujipendekeza

"Yule ni panya mdogo kama ni kijaribu kutengeneza mtego nimnase nitaonekana kichaa, ni kajitu kadogo wala usisumbue akili yako, aliharibu kioo cha gari tu si vingine....kama utalihitaji ruksa kutumia" Easton aliongea

Secretary Jo aliachia tabasamu pana usoni mwake, akiwa kafumba macho alijikuta akiona idadi kubwa ya wanawake wakimshobokea kisa gari

"Nyie siyo hadhi yangu ondokeni...." Secretary Jo aliongea kwa sauti akiwa katika kufikiria

"Nina dakika 30 za kuwa hapa acha kufikiria upuuzi" Easton aliongea baada ya kugundua fikira za huyu kiumbe zipo mbali

Secretary Jo ndio kushtuka, kwa pamoja walianza kukagua gari zilizokuwa zinauzwa

Baada ya jua kuzama, Ava pamoja na Mama yake walielekea baharini.

"Hii ni bahari kuu ya Mini, kwa muonekano inatisha lakini kama utaoga maji yake matatizo yako yote yataondoka...." Jessica aliongea huku ndani ya moyo wake akiwa na uoga

"Ni kweli bahari hii inatisha....kama nitaogopa sitaweza kufanikiwa, naomba ugeukie upande mwingine sitaki unione namna navyooga" Ava aliongea

Baada ya kukubaliana alivua nguo zake kisha akaanza kusogea tararibu....ujasiri wa kukamilisha tambiko lake ulimvaa. Alijikuta akioga bila uoga...wakati anaosha miguu yake aliona mkufu, tamaa ya kuuchukua ilimuingia.

"Mkufu? una uhakika huu mkufu ulikuwa usawa wa miguu yako" Jessica alimuuliza binti yake huku akiukagua

Ava alitikisa kichwa kuashiria ndiyo

"Kamwe usije kuutupa wala kuugeuza bidhaa ya kuuza, hii ni ishara tosha kuwa tambiko lako limejibiwa.....Malkia wa bahari hii kakupa mkufu kama zawadi" Jessica aliongea huku machozi yakimlenga

Mida ya usiku Ava akiwa kavaa mkufu shingoni, alianza kutuma maombi ya kazi kupitia email iliyokuwa imewekwa kwenye tangazo.

Upande wa Easton akiwa chumbani kwake ana kunywa wine, aliikumbuka siku aliyomnyonga Mpenzi wake (Sophia) mpaka kufa.

Vitu vyote vizuri alivyowahi kumpatia alivitupa baharini ikiwemo mkufu aliokota Ava.

Katika zawadi zote alizompatia Sophia, mkufu ndio ulikuwa na gharama kubwa kuliko hata magari japo kwa muonekano ni wa kawaida sana.

"Sikuwahi kufikiria kama ulikuwa mdanganyifu.... sitamani kukumbuka kuhusu wewe, nachukia pale napo kukumbuka" Easton alizungumza huku akikunja ngumi

Ndani ya moyo wake hajawahi na hana kama atakuja kujutia kumuua Mpenzi wake.

Kulivyo pambazuka asubuhi, Ava aliingia mtandaoni. Moyo wake ulilipuka baada ya kukutana na ujumbe wa kuitwa kwenye usahili

Alipiga kelele za furaha kabla hata hajapata kazi, Mama yake aliingia bila hodi kujua kitu gani kinaendelea.

Alifumba macho yake baada ya kumfuma binti yake akiwa uchi na mwenye msitu wa kutosha

*03*

"Unawezaje kupata usingizi na hilo pori!....sikuwahi kufikiria kama wewe ni mchafu namna hii" Jessica aliongea huku akilaani kwanini ameingia bila hodi

"Hili pori ni mali yangu kwanini ukasirike!...nimeitwa kwenye usahili, kesho saa mbili asubuhi nitakuwa katika geti la Kampuni la Penfolds. Kuliko ufikirie nawezaje kuishi na hili pori, fikiria ni nguo gani nitavaa" Ava aliongea akiwa kajifunika blanket mwili mzima, ni wazi alikuwa anaona aibu

"Huna haja ya kuchanganyikiwa kuhusu mavazi, vaa kawaida ili usiwe kivutio au kituko cha kila mtu kukutazama, kama Elon angekuepo nadhani angeamua uvae nini....japo ni wa kiume lakini alikuwa bora sana kwenye swala la mavazi" Jessica aliongea kisha akaondoka

Ava alijitoa ndani ya blanket, alirudia kuutazama ujumbe uliotumwa kwenye email yake kutoka Penfolds

"Nimechoka kukaa muda mrefu bila kazi, naamini nitafanya vizuri siku ya kesho" Ava aliongea pekee yake

Upande wa Easton akiwa ofisini kwake alipitia orodha ya majina ya watu walioitwa kwenye usahili

"Katarina yupo mapokezi anahitaji kuonana na wewe.... usijaribu kumpuuzia kwa sababu figo yake inaishi ndani ya tumbo lako" Secretary Jo aliongea

"Familia yangu ilikuwa na uwezo wa kununua figo kwa gharama yoyote ile, ni ujinga wake wa kutaka kuonekana anajali sana kuhusu Mimi hivyo naomba usisumbue akili yangu mwambie nipo bize" Easton aliongea akiendelea kupitia orodha ya majina

Secretary Jo alibakia kukodoa macho, hakutarajia kama boss wake anaweza kuwa na roho ngumu namna hii

"Ni kama tumezoeana sana, kila nikitoa amri zangu hushtuki badala yake unaanza kunipangia nini nifanye....nitatafuta Secretary mwingine" Easton aliongea

"Ni...ni... samehe" Secretary Jo aliongea akarudi mapokezi kurudisha majibu

"Easton yupo bize sana lakini kaahidi kukutembelea nyumbani kwako atakapo punguza foleni ya mafaili" Secretary Jo aliongea kwa kutabasamu

"Huna haja ya kuongea uongo kwa ajili yake, ni miaka 10 imepita sasa lakini bado hajabadilika.... ahsante kwa kurudisha majibu" Katarina alizungumza kisha akaondoka

Kama si Elon (Kaka yake Ava) kumshika basi angedondoka kwenye ngazi kutokana na mawazo

"Umefanikiwa kuonana naye?" Elon aliuliza

"Easton niliyemuacha miaka 10 iliyopita hajabadilika....." Katarina aliongea huku machozi yakimlenga lenga

"Naelewa namna unavyojisikia, lakini ningefurahi kama ungeacha kumpa umuhimu mkubwa katika maisha yako.... kuna watu wengi sana wanatamani kuwa na wewe, tafadhali sana fungua moyo kwa ajili yao" Elon aliongea

"Ili Mimi na wewe tuendelee kuwa boss na mfanyakazi wake, naomba uache kuongea kitu chochote kuhusu huyo Mwanaume, pengine ulikuwa hujui lakini yeye ndio sababu ya Mimi kutafuta pesa kwa nguvu, ili niwe na msaada kwake ni lazima niwe na pesa" Katarina aliongea kisha akaingia kwenye gari

Elon hakuwa na namna aliingia kwenye gari pia, mapenzi yake kwa mwanamke huyu ni makubwa sana kiasi kwamba hakujali kukaa mbali na familia yake kwa miaka 10

Upande wa Ava akiwa chumbani kwake alimwaga nguo zake zote sakafuni lakini hakuona nguo inayomfaa kuvaa siku ya kesho.

Aliachana na nguo akaelekea kwenye kabati la viatu, moyo wake ulishtuka baada ya kila kiatu alichokuwa anagusa kukuta kina meno ya panya, bahati nzuri au mbaya alifanikiwa kumkuta panya akiwa ndani ya kiatu alichokuwa ana kiamini kuliko vyote.

Kwa hasira alizokuwa nazo alimng'ata kichwa chote akakitema sakafuni.

Jessica aliingia bila hodi tena macho yake yalitua sakafuni moja kwa moja.... alijikuta akipiga kelele hakutarajia kama binti yake anaweza kuwa na roho ngumu namna hii

"Nitafuata ushauri wako, siku ya kesho ni sawa na siku nyingine sina haja ya kuhangaika" Ava aliongea akiwa kakata tamaa

"Elon alikuwa na suti nzuri pamoja na viatu vizuri.....hakuna ubaya kama utavaa nguo zake" Jessica alimuambia binti yake kisha akaondoka

Upande wa Selena (Mama yake Easton) alifurahi ndani ya moyo wake baada ya kumuona Katarina

"Nisamehe kwa kuja nyumbani kwako bila taarifa" Katarina aliongea

"Na kumbuka mara ya mwisho nilikuambia hapa ni sawa na nyumbani kwako....nafurahi kuhusu mafanikio yako, nitajitahidi kuunga mkono ndoto zako kadiri ya uwezo wangu, niambie ni kitu gani hicho unataka nami nitakutimizia" Selena aliongea

Katarina alipiga magoti bila kujali uwepo wa Elon

"Nampenda kijana wako, naomba unisaidie niwe mke wake.... sihitaji moyo wake, kitu pekee nachohitaji Mimi ni kuhakikisha yupo salama" Katarina aliongea

Selena alijiziba mdomo wake na mkono, hakujua aseme nini, alimnyanyua magotini Katarina kwa kisingizio cha baridi

Siku iliyofuatia, Ava alivaa suti ya Elon (Kaka yake) viatu vyote vilikuwa vikubwa kwake. Hakutaka kupata taabu aliweka karatasi kwa mbele ili mguu wake ukae vizuri.

Baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa alivaa cheni ya marehemu (Sophia) aliyoiokota baharini kisha akaondoka.

Alifika katika malango ya Kampuni la Penfolds, alitaja namba yake ya usahili baada ya Walinzi kujiridhisha walimpa kitambulisho akaingia ndani.
Alijiamini kupita maelezo....alikaa kwenye kiti kisha akakunja nne

"Elon...." Kijana mmoja aliyekuwa karibu yake alimuita
Ava ndio kushtuka koti la alilovaa limeandikwa jina la Kaka yake.

"Hakuwa na haja ya kuandika majina nguo zake" Ava alijisemea kisha akajiweka bize, hakuwa tayari kuzungumza chochote na Mwanaume huyu

Akiwa hapa ametulia alimuona Elon kwa mbali akiwa kabeba pochi ya Katarina. Alifumba na kufumbua lakini hakumuona tena....aliamini wenge ndio lina msumbua lakini ukweli ni kwamba macho yake yalikuwa sahihi

Tangazo lilitolewa watu wote wasimame kwa ajili ya kumkaribisha CEO wa Kampuni ya Penfolds.

Macho ya Ava yalishtuka baada ya kumuona Easton akiwa na jopo la watu waliovaa suti kali pamoja na vitambulisho shingoni mwao

*04*

"Nimefurahi kuona nyie wote hapa mpo kwa nia ya kufanya kazi na Mimi.... huenda wengi wenu mkawa hamnifahamu, naitwa Easton ni CEO wa hili Kampuni" Easton aliongea kisha akaachia tabasamu

"Laiti ningejua huyu panya ndio CEO wa hili Kampuni nisingeji sumbua kutuma maombi" Ava aliongea pekee yake akionekana kukata tamaa

"Easton si mtu wa kuendeshwa na migogoro binafsi....sijui ni kitu gani umemkosea lakini usivunjike moyo kwa sababu hatakukumbusha kosa lako" Binti aliyekuwa amekaa jirani yake alimsaidia kumtoa hofu

"Kosa nililofanya ni la jinai, siwezi kuamini katika matumaini yako" Ava aliongea

"Kitu pekee ambacho hawezi kusamehe ni udanganyifu tena katika mapenzi....kuwa na amani" Binti huyu alizungumza....ni wazi kabisa kabla ya kuja kwenye usahili alifatilia sifa za Mwajiri wake

Ava alikaa kwa kutulia baada ya Binti huyu kumpa matumaini.

Baada ya watu wote kupata chai, usahili ulianza.
Asilimia kubwa ya watu waliamini katika uwezo wao, tofauti na Ava aliamini katika tambiko alilofanya pamoja na mkufu aliovaa.

Hatimaye aliitwa katika chumba cha usahili.
Moyo wake ulilipuka zaidi baada ya kukutana macho na Easton.

Yule Binti alikuwa sahihi, Easton alionesha dalili zote za kutomfahamu Ava.

"Nahitaji kusikia ni kitu gani utafanya kuhusu Kampuni letu pindi utakapopata nafasi" Easton aliuliza

"Nitafanya vitu vilivyo nje ya uwezo wangu" Ava alijibu

Watu wote walimshangaa kwa jibu lake, Easton alimpa ishara aelezee maana ya jibu lake

"Nitahakikisha nafanya maamuzi magumu kuliokoa Kampuni endapo litakuwa katika wakati mgumu..." Ava aliongea

Secretary Jo alimruhusu aondoke, ni wazi hakufurahishwa na majibu yake hivyo aliweka alama x kwenye jina la Ava.

Baada ya usahili kumalizika, Secretary Jo aliwasogelea wasahili wote

"Nipo hapa kwa niaba ya CEO, tunashukuru kwa ushirikiano wenu mzuri, leo saa sita kamili usiku kila mtu aingie kwenye email yake kuona matokeo ya alichofanya, kuanzia sasa na kuendelea naomba msipige simu wala kuja ofisini kuulizia majibu kwani kila kitu kitamalizika kwenye email" Secretary Jo aliongea kisha akaondoka

Mapigo ya moyo wa Ava yalikuwa juu sana, ni wazi hakuwa na uhakika na kitu alichokifanya.... alijikuta akivua koti la Kaka yake baada ya kuhisi joto. Akiwa anatembea taratibu macho yake yalitua kwenye kioo kilichokuwa ukutani....alijicheka mwenyewe kwa namna alivyoonekana kituko kwa mavazi aliyovaa.

Upande wa Penfolds alianza kupitia majina ya watu walionekana kufanya vizuri....alimtazama kwa macho makubwa Secretary Jo baada ya jina la Ava kuonekana limewekwa mkasi

"Namkumbuka huyu binti vizuri, nguo alizokuwa amevaa pamoja na viatu vinatosha kumuonesha hana nidhamu..... muonekano wake ni mbaya, kitu kingine kilicho muangusha ni aina ya jibu alilotoa, ni kama anatamaa ya kuwa CEO na si Mfanyakazi" Secretary Jo aliongea

"Kwa upande wangu anafaa, ni watu wachache sana wanaweza kufikiria kufanya maamuzi magumu kuhusu Kampuni ambalo si lake, na kuhusu muonekano hivyo ndivyo alivyo watu wengi wamekuja na mionekano bandia lakini yeye kajikubali alivyo, hivyo nampitisha.... hakikisha siku ya kesho anafika hapa ofisini kuanza kazi" Easton aliongea

Secretary Jo alitaka kupinga lakini macho ya Easton yalimnyamazisha.

Ava hakwenda nyumbani badala yake alielekea ufukweni mwa bahari kuu ya Mini, alitandika koti lake akajilaza. Kichwa chake kilikuwa tupu, hakuwa na kitu cha kufikiria zaidi ya kufumba macho.

Baada ya kuchoka kukaa mahali hapa aliondoka akasahau koti

"Koti la Elon...." Ava aliongea pekee yake baada ya kukumbuka
Alirudi ufukweni kwa kukimbia, bahati nzuri au mbaya aliparamiana na Elon (Kaka yake)

"Elon?..." Ava aliita kwa sauti ya uoga asiamini anachokiona

"Umenifananisha pole kwa hilo" Elon aliongea kisha akaondoka
Hakuwa tayari kurudi kwa familia yake sababu ya Katarina, hakuwa tayari kujua watu hawa kwa sasa wanaishije bila yeye kwa sababu ndio alikuwa mhimili mkubwa.

Ava hakutaka kuelewa, alimkimbilia Kaka yake kisha akakagua alama iliyokuwa kwenye mkono.
Machozi yalimdondoka baada ya kugundua mtu huyu ni Kaka yake wa damu kabisa

"Sitakuuliza wala kukuomba urudi nyumbani, nitajifanya sijaona chochote" Ava aliongea kisha akaondoka, hakutaka kufatilia kuhusu mkoti tena

Alifika nyumbani akiwa amelowa machozi, Jessica alimkumbatia binti yake akiwa mwenye hofu

"Elon anaishi...kwa haraka tu ana maisha mazuri, kuanzia sasa na kuendelea acha kumfikiria wala kuumia moyo kisa yeye" Ava aliongea akizidisha kulia

Jessica alikaa kimya hakujua ni maneno gani anapaswa kuongea.

Upande Easton baada ya kurejea nyumbani, aliachia tabasamu kutokana na chakula kilichokuwa mezani.

Hakusubiria kukaribishwa, alikaa akaanza kula

"Tabasamu lako usoni linatosha kuniambia Katarina ni Mpishi vizuri" Selena aliongea

Easton alidondosha kijiko, tabasamu lilipotea usoni mwake

"Kuanzia sasa nitakuwa na kula hotelini.
 
*MOYO WA KWELI*
*6-10*
*_____________________________________*

*06*

"Macho ya watu wengi hapa yapo kwa Easton, ni kama wanasubiria afanye kosa dogo tu wamuondoe katika nafasi yake" Secretary Jo aliongea baada ya kufuma Ava akimuangalia Katarina na Elon

"Kwanini unaniambia haya maneno" Ava aliuliza

"Hujamaliza hata mwezi hapa lakini tayari umeonekana machoni kwa Easton...sikuamini hata kidogo hivyo usijaribu kumuingiza kwenye matatizo....nimekusikia ukikiri kuharibu gari lake, naomba uwe makini sana usije kuharibu moyo wake" Secretary Jo aliongea

Ava alimsogelea, wakawa pua na mdomo

"Hili Kampuni lina CEO mmoja tu naye ni Easton, ni kawaida ya kila mfanyakazi kujituma kwa bidii ili apate upendeleo kutoka kwake. Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuonekana...nipo hapa kutafuta pesa na si kuharibu sifa za Kampuni hili" Ava aliongea kisha akaondoka

Secretary Jo aliishia kukunja ngumi kwa majibu aliyopatiwa.

Upande wa Katarina alizidi kutengeneza Mlima wa majarida lakini Easton hakutokea

"Naomba tuondoke, unaonekana kutia huruma machoni kwa watu....kila mtu anayepita ana kuangalia wewe" Elon alishauri

"Leo sitaondoka bila kuonana naye....kama umechoka unaweza kuondoka" Katarina aliongea

Elon alikaa kimya, hakutaka kumkera Mwanamke huyu.

Muda ulizidi kwenda bila wao kupatiwa huduma, wakiwa katika hali ya kukata tamaa, Easton alipita.

Katarina alimkimbilia kisha akasimama mbele yake

"Hii ni ofisi na si sehemu ya kufanya maongezi binafsi...." Easton aliongea akitaka kuondoka, lakini Katarina alimzuia kwa kumkumbatia

"Nafurahi kuona unaendelea vizuri...." Katarina aliongea kisha akajitoa kifuani kwa Easton

"Mara ya mwisho Mimi na wewe kuzungumza nilisema ukae mbali na Mimi....nitarudia kukuambia haya maneno leo, kaa mbali na Mimi" Easton aliongea kisha akaelekea kwenye gari lake

Secretary Jo aliomba radhi kwa niaba ya boss wake.

"Elon, naomba uniletee picha ya mwanamke anayempa kiburi Easton" Katarina aliongea

"Nimemchunguza kwa muda mrefu sana hana mahusiano.....kubali huna nafasi kwake" Elon aliongea

"Rudia kuchunguza tena, huenda ikawa kazi ngumu kwako lakini ni kutoe hofu kwa sababu nitakusaidia" Katarina aliongea kisha akaelekea kwenye gari lake pia

Baadhi ya wafanyakazi walioshuhudia namna Easton alivyomkatili Katarina walicheka.
Elon alipata hasira lakini hakuwa na kitu cha kuwafanya.

Mida ya jioni, Ava akiwa bafuni alioga haraka haraka....alivaa nguo yake anayoiamini pamoja na viatu vya kazini.
Secretary Jo alimpigia simu akampa maelekezo ni hoteli ipi aende kwa ajili ya dinner.

Ava alipanda tax kisha akatoa maelekezo, baada ya kufika Secretary Jo alifika haraka akamlipa dreva

"Hivi viatu ni sare ya kazini na si vya kutembelea mtaani....kama vitaisha haraka sitaingia jukumu la kutafuta viatu vingine, umewahi kufikiria kwanini tunawapa nauli siku za kazi?...lengo ni viatu visiishe kabla ya miezi mitatu" Secretary Jo alizungumza

Kabla Ava hajajieleza ushuzi ulimpita, macho yalimtoka kwa sababu halikuwa lengo lake

"Endapo utafanya hili tukio mbele ya Easton hautasamehewa" Secretary Jo aliongoza njia akiwa kaziba pua

Ava aliona haya ndani ya moyo wake lakini alijikaza kwa sababu hakudhamiria.

Easton akiwa anasoma gazeti, aliachia tabasamu kwa kumuona Ava.

Secretary Jo alikasirishwa na kitendo cha boss wake kumfurahia Ava

"Nisamehe kwa kuchelewa...." Ava alijitetea huku akikaa

"Unajua kwenda na muda, hujachelewa" Easton aliongea kisha akampa ishara Secretary Jo ya kuondoka

"Unanifukuza?" Secretary Jo aliuliza kwa ishara

Easton alitikisa kichwa kuashiria ndiyo, Secretary Jo aliondoka akiwa haamini macho yake.

"Agiza chakula chochote unachotaka nitalipa..." Easton alimpa uhuru Ava

Ava si mtu wa kuigiza, baada ya kupatiwa ruhusa aliandika oda ya vyakula alivyokuwa anataka.

Easton aliachia tabasamu baada ya kuona wahudumu sita wakileta chakula mezani kwao, udogo wa meza ulifanya waongezewe meza tatu.

"Unaweza kuniambia ni kwanini unahisi itapendeza zaidi kama radha ya wine ya Shiraz itabadilishwa" Easton aliuliza huku akila

"Naomba ni kujibu kwa swali, kwanini wali unapikwa mtindo tofauti?...bila shaka umepata jibu, watu wanapenda radha tofauti na siyo ile ile iliyozoeleka" Ava aliongea

Walizidi kupiga stori za hapa na pale, ingawa ni kwa masaa machache lakini Easton alifurahishwa na ubongo wa Ava.

"Nitakupeleka nyumbani kwenu...." Easton alizungumza baada ya dinner kumalizika

"Hakika....najihisi nimekuwa mzito ghafla, hii hoteli wanajua kupika" Ava aliongea

Wakati wanatoka ndani ya hoteli, Easton alikutana macho kwa macho na Pacco (Baba mdogo wake). Alitoa heshima kishingo upande kisha akapiga hatua aondoke

"Naamini sasa umemsahau Sophia..." Pacco aliongea kwa unafiki wa hali juu

Easton hakujibu kitu, alijizuia kujaza watu eneo hili kwa kuondoka na Ava.

Pacco aliachia tabasamu lililojaa dharau kwa muonekano wa kishamba wa Ava.

Easton aliendesha gari kwa umakini mpaka alipofika nyumbani kwao Ava

"Ahsante kwa lifti...." Ava aliongea

"Subiri kwanza...." Easton alimzuia baada ya kuuona mkufu aliowahi kuutupa baharini miaka 7 iliyopita ukiwa shingoni kwa Ava.

Ni kweli baada ya kuukagua vizuri aliugundua, kumbukumbu mbaya za Sophia zilijaa kichwani kwake alijikuta akimkaba Ava huku akimuita mdanganyifu

Itaendelea



*07*

Ava hakuwa mzembe alijitutumua akamng'ata mkononi Easton

"Ni...ni...samehe sikudhamiria kukukaba" Easton aliongea baada ya kung'atwa

"Huna haja ya kujitetea, ni kawaida binadamu kushikwa na mapepo bila kujalisha ni masikini au tajiri" Ava aliongea

"Huo mkufu ni mali yangu....niliutupa katika bahari kuu ya Mini miaka saba iliyopita, naomba unipatie nitautupa sehemu ambayo hautaokotwa tena" Easton aliongea akiwa kanyoosha mkono

Ava alitaka kupinga lakini macho ya Easton yalimtisha aliuvua haraka akakabidhi

"Ahsante kwa uelewa wako, ni kutakie usiku Mwema" Easton aliongea kisha akamfungulia Ava mlango wa gari

Jessica alifungua mlango kwa pupa akamdaka binti yake

"Hata hujamaliza mwezi umeanza kuletwa na gari! hii si dalili nzuri naomba uwe makini..." Jessica aliongea

Ava hakuongea chochote kutokana na shibe aliyokuwa akiihisi. Aliingia chumbani kwake akavua nguo zote. Jessica aliingia bila hodi, alistaajabu baada ya kulikosa pori sehemu za Ava

"Maana yake ni kwamba kwa sasa upo kwenye mahusiano....si kawaida yako kukaa bila pori" Jessica aliongea

"CEO wa Kampuni ya Penfolds ni mmiliki wa mkufu uliokuwa shingoni kwangu, nimemrudishia" Ava aliongea

Jessica aliziba mdomo wake na mkono

"Huna haja ya kuogopa iliandikwa mkufu utarudi kwake kupitia wewe....hivyo acha kuchanganyikiwa" Jessica aliongea

"Kuhusu Elon nadhani katusahau sisi sababu ya mwanamke...." Ava aliongea akiukumbuka uzuri wa Katarina

"Naomba ulale...." Jessica aliongea kisha akaondoka, ni wazi hakuwa tayari kuzungumza kuhusu Elon

Ava aliishika shingo yake, alikumbuka namna Easton alivyomuita mdanganyifu. Hakutaka kufikiria sana alipanda kitandani akalala

Kulivyo pambazuka asubuhi alikuwa wa kwanza kuripoti kazini, Secretary Jo alizidi kukasirishwa na namna Ava anavyojituma

Kwa makusudi alimtega mguu, kabla Ava hajafika chini Easton alimdaka

"Sa... samahani" Ava alijitetea

"Miguu haina macho, kuwa na amani" Easton aliongea kisha akaendelea na safari yake

Mabinti wote walimgeukia Ava, hakuna hata mmoja aliyeamini kama kweli ilikuwa bahati mbaya. Alionekana kama mtu anayemtaka CEO kwa nguvu.

Wakati Easton anapitia mafaili, alijishika mfukoni akatoka na mkufu mpya

"Niitie Ava..." Easton alitoa amri

"Naenda kumuita, lakini naomba kujua huo mkufu unatafuta nini mkononi mwako" Secretary Jo alijikuta akiuliza

Easton alimuangalia kwa macho makubwa kwa swali aliloulizwa.

Secretary Jo alitambua kosa lake aliondoka kwa kukimbia. Dakika 10 hazikupita Ava aliingia ofisini

"Huu mkufu ni kwa ajili yako.... nisamehe kuhusu tukio la jana, siku nikiwa na muda nitakueleza kila kitu" Easton aliongea

"Hajamaliza hata miezi mitatu tayari ushafikiria kuzungumza siri zako kwake hakika kuna uchawi upo" Secretary Jo aliingilia mazungumzo

"Mimi siyo mke wako kwanini unanifatilia sana! kabla mwezi hujaisha naomba uoe" Easton alifoka

Secretary Jo aliinamisha kichwa chake kumaanisha anaomba samahani.

Ava alichukua mkufu kisha akaondoka kwa kisingizio cha kubanwa mkojo.

"Naelewa hofu yako ni nini, lakini naomba uyaondoe mawazo machafu kichwani mwako....nafurahishwa na utendaji wake wa kazi na si kingine" Easton aliongea kwa kumaanisha

Secretary Jo alitikisa kichwa kuashiria ameelewa.

Upande mwingine Pacco (Baba mdogo wa Easton) alimtembelea Selena (shemeji yake)

"Ni kitu gani kimekuleta nyumbani kwangu tena bila taarifa" Selena aliuliza

"Mgeni hukaribishwa kwa tabasamu, bila kujali uhusiano uliopo kati yake na mwenyeji wake" Pacco aliongea huku akimpatia simu

Selena alipokea simu, alishtuka baada ya kukutana na picha ya Ava

"Naomba uniambie maana ya hii picha" Selena aliuliza

"Ni msichana aliyekuwa na Easton siku ya jana katika hoteli ya Rhino" Pacco aliongea

"Easton si mtu wa kuambatana na wasichana, na kama itatokea ni sawa lakini si kwa aina hii ya kituko unacho nionesha" Selena aliongea akirudisha simu

"Kwanini usimuulize Secretary Jo" Pacco alichochea

"Naomba tuongozane wote....nina muda bila kutia mguu wangu katika Kampuni ya Penfolds" Selena aliongea

Kwa pamoja walikubaliana, wakati wanatoka ndani waingie kwenye gari...Katarina alifika. Walikubaliana kuondoka wote

"Nahitaji kubadili radha ya wine ya Shiraz...hivyo nitaandaa shindano miongoni mwa wafanyakazi lengo ni kupata wine nzuri na si kingine" Easton aliongea na Washirika wakubwa wa Kampuni lao.

Kila mtu alifurahishwa na wazo lake jipya ambalo halijawahi kuzungumzwa na CEO yoyote.

Tangazo lilitolewa kwa wafanyakazi wote, Ava aliachia tabasamu baada ya kuona Easton kashawishika na wazo lake.

Akiwa anapanga matunda kwenye boksi, alikutana macho kwa macho na Elon (Kaka yake) akiwa kaambatana na Katarina, Selena pamoja na Pacco.

"Tumeonana tena mahali hapa" Pacco alimuongelesha Ava

"Ndiyo, na kumbuka tulionana katika hoteli ya Rhino" Ava alijibu kwa nia njema akihisi ni wateja

Selena alimuangalia kwa macho ya upelelezi bila kummaliza

Secretary Jo alikuja kwa kukimbia kupokea msafara

"Karibuni sana, japo Easton yupo bize lakini hawezi kuacha kuzungumza na Mama yake" Secretary Jo aliongea

Ava ndio kushtuka kama mwanamke aliyepo mbele yake ni Mama wa Easton.
Aliwasindikiza kwa macho, hakuelewa kwanini Kaka yake anaambatana na watu wenye pesa

Easton akiwa bize ofisini kwake, alishangazwa na ugeni wa watu wanne

"Hii ni ofisi na si mgahawa kwanini unaniletea watu wote hawa" Easton alimuuliza Secretary Jo kwa ishara

"Huna haja ya kunilaumu, nadhani unaelewa Mama yako ni mtu wa aina gani" Secretary Jo alijibu kwa ishara pia

"Kuna kazi ndogo sana nahitaji kuimalizia niongee na wageni, niletee Ava" Easton alimuagiza Secretary wake

Dakika 10 hazikupita Ava aliingia ofisini,
"Nitafurahi kama utaniandikia kidogo kuhusu wazo lako la jana....kuwa huru nitalinunua" Easton aliongea akiachia tabasamu
Hakuishia hapo alimpisha Ava kwenye kiti chake akae, lengo lake ilikuwa atumie kompyuta yake

"Haiwezekani....." Secretary Jo aliongea kwa sauti
Watu wote walimgeukia, tangu aanze kufanya kazi na Easton hajawahi kutumia kompyuta anayopatiwa Ava

Itaendelea

*08*

Easton alimuangalia Secretary Jo kwa macho makavu

"Ni ajabu Mfanyakazi wa chini sana kutumia Kompyuta ya CEO, kuna hatari ya kuvujisha taarifa kwa maadui... Secretary Jo yupo sahihi lakini kama ni mtu unayemuamini ni rukusa" Selena aliongea akijaribu kuzuia hisia zake

"Tangu ni zaliwe sijawahi kuona aina hii ya kompyuta.....niwe muwazi tu siwezi kuitumia, nitaandika kwenye kompyuta yangu kisha nitakutumia kwa njia ya email" Ava aliongea, uwezo wa kuitumia kompyuta ya Easton alikuwa nao lakini hakutaka kuwakwaza wageni

"Hakikisha unanitumia kwa wakati" Easton alimuambia Ava kisha akamruhusu aondoke

Watu wote walimsindikiza kwa macho, kila mtu alijaribu kuutafuta uzuri wake lakini hawakuuona.

"Nafikiria kumrudisha kazini Pacco....kosa alilowahi kulitenda siku za nyuma haliwezi kujirudia tena, hivyo nipo hapa kuomba msaada wako.... kuhusu Katarina kwa sasa ni Mwanamitindo maarufu, vipodozi vyake vinashika namba tatu sokoni, ana sifa na vigezo vyote vya kuwa Mshirika wa Kampuni hili" Selena aliongea

Pacco na Katarina walimgeukia kwa sababu hawakuwa wamezungumza hizi habari

"Linapokuja swala la maendeleo ya Kampuni hili huwa naweka pembeni mambo binafsi, kuhusu Baba mdogo nitajua ni namna gani nitamrudisha kazini, kwa upande wa Katarina naomba uandike barua ya kuomba kuwa Mshirika.... Secretary Jo ni mzoefu atakusaidia endapo utakwama" Easton aliongea huku akiachia tabasamu

Watu wote walishusha pumzi hawakutarajia kama Easton atakuwa mwepesi wa kuelewa

"Ni muda wa kazi hatutaki kuwa mzigo kwako....uwe na kazi njema" Selena aliongea kisha akaondoka na msafara wake

"Shemeji, sikufikiria kama nina nafasi kubwa namna hiyo moyoni mwako.." Pacco aliongea kwa kujichekesha

"Wewe ni panya mdogo sana kwa Easton, na ndio sababu nimekurudisha kazini ni kifahamu fika huwezi kumsumbua" Selena aliongea kwa sauti ya chini kisha akaondoka, kabla hajaingia kwenye gari lake alimsogelea Katarina

"Nina maana kubwa sana kutaka wewe ufanye kazi na Easton, ukiwa unaonekana machoni kwake kila siku ni rahisi kuuteka moyo wake... tofauti na ukiwa mbali" Selena aliongea

Katarina alimkumbatia, hakutarajia kama Mwanamke huyu anajali kuhusu yeye kupita kiasi.

Upande wa Ava baada ya kumaliza kuandika wazo lake alimtumia CEO

"Njoo ofisini kwangu...." Easton alimtumia Ava ujumbe kupitia email

Secretary Jo akiwa ana chapa barua alishangaa kumuona Ava

"Hukuwa na sababu ya kuja hapa kila kitu ungemaliza kwenye email, boss wangu ana akili nyingi sana asingepata shida kuuelewa waraka wako" Secretary Jo aliongea

"Nimemuita Mimi...." Easton aliongea kisha akampa ishara Secretary Jo ya kwenda nje

Secretary Jo aliondoka akiwa mwingi wa hasira

"Wazo lako ni la kipekee sana, kwanini tusifanye jaribio la kutengeneza wine yako baada ya watu wengine kwenda nyumbani?" Easton aliuliza

"Mimi pia nina shauku ya kulileta wazo langu kwenye uhalisia....nitafurahi kama tukifanya hivyo" Ava aliongea

Kwa pamoja walikubaliana, baada ya wafanyakazi wengine kuondoka....Ava na Easton walijifungia katika chumba maalumu cha kutengeneza wine

Kila kitu walifanya kwa kushirikiana mpaka walipomaliza

Ava alikuwa mwenye hofu kubwa sana, ndani ya moyo wake alisali wine waliyotengeneza iwe na ladha tofauti na iliyozoeleka

Easton aliweka kidogo kwenye glass akanywa, bila kufikiria mara mbili mbili alimkumbatia Ava

"Hii ladha ni ya kipekee sijawahi kukutana nayo tangu ni zaliwe...." Easton aliongea

Ava alikunywa kidogo pia, alijikuta akipiga kelele kwa utofauti wa radha aliyoionja

Kwa mara nyingine tena walipata dinner kwa pamoja, Easton alimrudisha Ava nyumbani akiwa mwenye furaha moyoni mwake.
Alishindwa kuzuia furaha yake, alimbusu mkononi kama ishara ya ahsante.

Mapigo ya moyo wa Ava yalivurigika ingawa alijionesha yupo sawa.

Mida ya saa sita usiku akiwa kitandani kwake, alihangaika kutafuta usingizi bila mafanikio, hakuona haja ya kujilazimisha...kwa mara ya kwanza kabisa alimpigia Easton usiku

Easton hakuwa amelala, alipokea haraka simu ya Ava akihisi pengine kuna shida.

Kila Easton alivyojaribu kujua lengo la simu kupigwa hakulipata....si mtu wa kupenda kuongea na simu lakini kwa kuwa Ava alikuwa ana bandua na kubandika hadithi alijikuta akicheka

Selena akiwa kaegemea kwenye mlango wa mwanae alisikia kicheko kila baada ya sekunde kadhaa.

Alipiga simu ya Katarina asikie kama inatumika lakini haikuwa hivyo.

Aliondoka akiwa anajiuliza ni mtu gani huyo anayemfanya kijana wake acheke namna hiyo.

Siku iliyofuatia Easton hakutaka kwenda kazini moja kwa moja badala yake alimtanguliza Secretary Jo.

Aliingia kwenye duka la urembo akamnunulia Ava marashi pamoja na lipstick. Alifanya hivi kwa nia njema tu hakuwa na wazo lingine.

Ava akiwa ofisini kwake alishangaa akiwekewa mfuko mezani na Easton.

Alifungua kwa haraka aone nini kaletewa, alishtuka baada ya kukuta zawadi za kipekee

"Ahsante...." Ava aliongea huku akiachia tabasamu

"Naomba ushiriki pia kwenye shindano la ubadilishaji wa ladha mpya ya wine....kama utashinda nitakupa zawadi yoyote utakayotaka" Easton aliongea akiwa kamkazia macho

Moyo wa Ava ulienda mbio, aligeukia pembeni kuepuka kuzimia kabisa

Itaendelea

*09*

"Unapokuwa unaongea na Mimi jitahidi uniangalie machoni tofauti na hapo nitahisi huvutiwi na uwepo wangu" Easton aliongea

Ava alimgeukia wakawa wanatazamana

"Endapo utashindwa kuitumia lipstick usisite kuja ofisini kwangu" Easton aliongea kisha akaondoka

Ava aliifungua lipstick, kila alipojaribu kupaka mdomoni kwake haikuacha rangi, alijikuta akitabasamu kwa kushindwa kuitumia

"Kwani hii lipstick ina neno la siri? kila nikijaribu kupaka siambulii kitu" Ava alimtumia ujumbe Easton

"Baada ya muda wa kazi kuisha njoo ofisini kwangu nitakufundisha" Easton alimjibu Ava akiwa ana tabasamu

Secretary Jo alijitahidi kuchungulia kwenye simu ya Easton aone nini kinamfanya atabasamu lakini
hakuambulia kitu mwisho wa siku alidondokea kwenye bega la boss wake

"Ni...ni... samehe, lakini kama hautajali niazime simu yako kwa dakika chache nimtumie ujumbe Mama yangu" Secretary Jo aliongea

"Simu yako ina shida gani? usiniambie Mama yako kazuia namba yako tena msiwasiliane" Easton aliongea

Secretary Jo alitikisa kichwa kuashiria ndiyo, baada ya kubidhiwa simu alianza kufatilia kila kitu kuhusu Ava na boss wake

"Mmefikia hatua ya kununuliana lipstick yenye neno la siri!" Secretary Jo alijikuta akiongea kwa sauti, ndipo Easton aligundua lengo lake halikuwa kuongea na Mama yake kama anavyodai

"Kwanini unateseka sana kuhusu Ava, ni binti wa kawaida sana lakini naona anakunyima amani ya moyo" Easton aliongea huku akimnyanganya simu

"Na hofia yupo hapa kuwa CEO wa moyo wako....kitu hiki kinaninyima amani ya moyo na hata natamani kumfukuza" Secretary Jo aliongea

"Linapokuja swala la mapenzi wanawake wote wanaopita mbele ya macho yangu ni wadanganyifu, nipo karibu na Ava sababu ya ubongo wake....siku atakayoanza kuwa na akili nyingine sitamruhusu kuwa karibu yangu hivyo acha kuchosha ubongo wako" Easton aliongea

Secretary Jo hakujibu chochote badala yake alimkabidhi barua ya Katarina

"Kaandika vizuri barua yake, nitaifanyia kazi...muambie awe na amani. Andaa pia ofisi kwa ajili ya Pacco....kitengo chake kitakuwa kile kile cha Afisa manunuzi" Easton aliongea

"Tuna majina 120 ya Wafanyakazi wenye nia ya kushiriki kwenye shindano la ubadilishaji ladha ya wine yetu" Secretary Jo aliongea

Easton alitikisa kichwa kuashiria ameelewa, upande wa Ava aliona masaa hayaendi....akili yake iliwaza kufundishwa namna ya kutumia lipstick na si kingine

Hatimaye masaa ya kazi yaliisha kila mtu alishika njia yake isipokuwa Ava aliwahi ofisini kwa Easton

Bahati mbaya CEO alikuwa na foleni ya mafaili...

"Usijali nitakufundisha kwa wakati mwingine...." Easton aliingia

"Nitasubiria mpaka utakapomaliza...kama hautajali naweza kukusaidia nimewahi kufanya kazi ya kukagua mafaili nilipokuwa chuo" Ava aliongea

"Kaa hapo nione unachofanya, huenda siku moja ni kakuachia ofisi ukaimu nafasi yangu" Easton aliongea

Kwa pamoja walianza kufanya kazi, akili ya Ava ilikuwa juu sana katika kuamua changamoto zilizokuwa kwenye mafaili. Easton alijikuta akimuangalia Ava kwa uwezo wa akili aliyojaliwa

Ava alishtuka baada ya kukutana macho na Easton, kwa mara ya kwanza kabisa kwikwi ilimshika

"Usiwe na hofu itaisha baada ya kufanya hivi" Ava alizungumza kisha akachana karatasi kidogo akailowanisha na mate kisha akaiweka kwenye paji la uso,

Easton alijikuta akicheka, yeye pia alichana karatasi kidogo akailowanisha na mate akaibandikiza kwenye paji la uso wa Ava.

Baada ya kazi kuisha alimfundisha namna ya kutumia lipstick

"Kabla hujaifungua tamka neno CEO, ukijfanya hivyo utafanikiwa....nilisahau kukuambia lakini ni lipstick ghali sana huenda ukawa ni mwanamke wa tatu kuitumia ka
 
Back
Top