Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupitia ripoti ya National Accounts of Mainland Tanzania 2024, pato la wastani la mtu mmoja (GDP per capita) Tanzania Bara ni Tsh 3,058,847 kwa mwaka 2023.
Hata hivyo, mikoa kadhaa bado ipo chini ya kiwango hicho ikionesha changamoto za maendeleo ya kiuchumi, uwekezaji, na huduma za kijamii.

Hii ndio mikoa 10 masikini zaidi Tanzania mwaka 2023:

Kagera — kiwango cha chini zaidi nchini

Simiyu — uchumi mdogo unaotegemea kilimo

Katavi — changamoto za miundombinu na uwekezaji

Rukwa — uzalishaji mdogo na usafirishaji mgumu

Singida — uchumi unaotegemea kilimo cha msimu

Tabora — uwekezaji mdogo wa viwanda na biashara

Dodoma — ongezeko kubwa la watu limepunguza wastani wa pato

Pwani — bado haijafikia wastani licha ya ukaribu na Dar es Salaam

Mara — shughuli ndogo za viwanda na huduma

Kigoma — uchumi mdogo wa biashara na uzalishaji

Mikoa hii inatajwa kuwa chini ya wastani wa kitaifa kwa pato la mtu mmoja, ikionyesha tofauti kubwa ya maendeleo kati ya mikoa.

Sababu kuu zinazotajwa ni:
▪︎Ukuaji mkubwa wa idadi ya watu
▪︎Uwekezaji mdogo wa viwanda
▪︎Changamoto za miundombinu
▪︎Kutosambaa kwa shughuli za kiuchumi
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) – National Accounts of Mainland Tanzania 2024