Kasomi
JT Founder
Shirika la usafiri wa umma mjini Wiesbaden, magharibi mwa Ujerumani, limeitaka polisi kumshtaki kijana wa miaka 15 aliyedaiwa kuiba basi na kumpeleka mpenzi wake umbali wa kilomita 130 hadi shuleni mjini Karlsruhe.
Mkuu wa kampuni ya mabasi ya NVG, Jörg Martini, aliliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kuwa hakuna aliyejeruhiwa, na basi hilo lilikutwa salama Karlsruhe kabla ya kurejeshwa Wiesbaden na dereva mwenye leseni halali.
Hadi sasa NVG haijafahamu kijana huyo alipataje funguo za basi, na imekataa utani uliotolewa na vyombo vya habari ukidai kuwa alikuwa na kipaji cha kuendesha, ikisisitiza kuwa kitendo hicho ni kosa la jinai.